08/09/2026
WASIRA: HAKUNA MTU 'ALIYESHUGHULIKIWA' KWA KUWASEMEA WATANZANIA
Na MWANDISHI WETU
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM - Bara), Stephen Wasira, amesema hakuna mtu anayeshughulikiwa kwa sababu ya kuwasemea wananchi, akisisitiza kuwa kauli yoyote ya kukosoa inapaswa kuungwa mkono na utafiti na ushahidi.
Wasira amesema kauli kwamba mtu anaweza kushughulikiwa kwa sababu amezungumza kwa niaba ya wananchi si sahihi, akimtaka kila anayetoa madai hayo kufanya utafiti kabla ya kuzungumza.
Amesema hayo leo Septemba 8, 2026 katika mkutano wa wadau wa kitaifa wa kitafakari kutafakari hali ya siasa nchini, jijini Dar es Salaam.
Amesema wasomi wana wajibu mkubwa wa kufanya utafiti, kwa kuwa utafiti ni sehemu muhimu ya usomi na humsaidia mtu kutoa taarifa na hoja zenye msingi.
“Usipotafiti utasema chochote tu, utakuwa k**a mitandao ya kijamii ambayo haina control, (udhibiti)” amesema Wasira.
Kwa mujibu wa Wasira, hakuna aliyesema kwa niaba ya wananchi kisha akaondolewa au kushughulikiwa kwa sababu hiyo, amesisitiza kuwa viongozi na wananchi wote ni sehemu ya jamii moja.
Amesema kauli kwamba mtu fulani anazungumza kwa niaba ya wananchi inapaswa kuangaliwa kwa kuzingatia ushahidi wa wananchi hao ni akina nani na walitoa wapi mamlaka ya kuwakilishwa.
Wasira ametoa mfano wa suala la Katiba Mpya, akisema CCM iliahidi katika Ilani yake ya Uchaguzi kuhusu suala hilo, huku akieleza kuwa utekelezaji wake unahitaji kuangalia mazingira na changamoto zilizopo.
Amesema hata Katiba ya mwaka 1984 ilitokana na Katiba ya mwaka 1977, akieleza kuwa mabadiliko ya katiba yamekuwa yakitokana na mahitaji na changamoto zilizojitokeza katika vipindi tofauti.
Ameongeza kuwa wakati wa kuandaa mipango ya utekelezaji, baadhi ya matukio hayawezi kutabirika mapema, hivyo muda na mazingira vinaweza kulazimisha kufanya marekebisho ya hatua zilizopangwa.
Wasira amesema suala la Katiba Mpya halijaachwa, bali mchakato wake unapaswa kuendelea kwa kuzingatia uamuzi na mipango iliyowekwa.
Amesema mtu anapowataka wananchi “wapambane,” ni muhimu pia kujiuliza wanapambana na nani, kwa kuwa wakati mwingine changamoto zinazozungumziwa zinahitaji juhudi za pamoja badala ya kuonekana kana kwamba kun