Ashuwey Farmers and welfare group

Ashuwey Farmers and welfare group Ashuwei ni mji unaopatikana katika eneo la kiunga katika wilaya ya lamu.

Inakadiriwa kuwa maeneo haya yote wakaazi wao ni takriban 8000, kulingana na utafiti katika miaka ya tisaini(90s).

20/04/2025

*TANGAZO LA MKUTANO WATU WA ASHUWEI*

ASALAM ALAIKUM

NINGEPENDA KUWAJULISHA KUTAKUWA NA MKUTANO WA WATU WA ASHUWEI.

*SIKU* JUMA TANO
*TAREHE* 07.05.2025

*WAKATI* SAA TANO ASUBUHI (11AM)

*PAHALI* AMU TOWN(MWANANA ARAFA HALL)

*AGENDA*
1.KAMATI RASMI ITAKAYOCHAGULIWA KUSIMAMIA ARDHI.

UMOJA NI NGUVU TUJITAHIDINI TUFIKE KWA WINGI TULIMALIZE JAMBO HILI.

*TUWAJULISHE WALIO NJE YA UKUMBI*

*SHUKRAN*

27/10/2024
17/10/2024
17/10/2024
17/10/2024

WAKATI WA KUTAHIRIWA ASHUWEYI
1.SHEREHE KUANZA KUANZA BAADA YA SWAL ALASIRI
2.NGOMA HUANZA KUPIGWA KWAO ANE TAHIRIWA NA KUELEKEA MJI MWINGINE WA KARIBU
3.KABLA YA KUINGIA MJI MWINGINE HUWA KUNA WAZEE LAZIMA WAIPE RUHUZA NGOMA INGIE.

KWA MFANO;
Bibi mwana tele na mzee ba suo walipoenda na ngoma yao kwaajili ya kumtahiri watoto wao ngoma yao haikupokelewa.bibi mwana tele akatoa shairi hili

“Nalikun’wa vuruu na nkacheani na banguu
Kaya kutembedha shani pamoya na’nyi dh’udhanguu
Moyi hafundi duru kwaherini nd’adhanguu.”

“Vadh’ee v’echu kudhimu havakuya kuchudoyaa
Dhikosekene r’uhuma hata kwa vachu vya moyaa
Mwana wa k**asi mbili hakupacha hata moyaa.”

Hapo maan ya k**asi mbili ni kuhusu bahero adi Familia yake kwa upande wa babake(alomzaa babake na mamake walitoka mvundeni ) na hawakuja kwenye shere ya kutahiri.

“Naliabiri I’yiini nalipochia niya
Kahora utemeduni ushobo kaumbiriaya
Yeo huvicha muomwe kuyakumwangaliya”

MASHAIRI YA SIZI BAHERO NA FATIMA SHEMAKA WALIPO TAHIRI WATOTO WAO.

Ali sema Fatima shemaka;

“Sizi bahero nalikend’a sinadhoo
Kiyatinanga mashaka si hofu si yoo
Licha ya jadi nkandaa utoke mashakuoo”

ARABIA SHEMAKA NAE AKAIMBA:

“Sizi na mwanae valishuka wakipanda
Sikufanya unukuu sikupepecha ntanga
Sifuni nchandaa eyo kunipamba”

SHALI OBO WA SHEMAKA ALIPO TAHIRIWA SHAIRI LILITOLEWA NA BIBI SOMOE WA ALI(ALOMZAA OBO SHEMAK NA WENGINE)

“Hunena dh’ee obo im maovu sipendi
Hatua dh’inishishie ndimi mwana wa va’tendi
Ndooni muone mbayo iti’ndievyo mishe’ndi”

“Kadha’nya mwanangu shali siketi ukashangaa
Nami nataka kuchend’a wala siyesha tamaa
eyo hutedh’a na mbayo jadi letu watandaa”

MWANATELE WA BAHERO AKIMUIMBIA SHALI WA OBO SHEMAKA

“Nalikwend’a limani buge likanichambaa
Unga kala wa dhifuko wala sikwisha ndaa
Eyo hutedha na mbayo jadi letu watandaa”

“Mwanagu shali siketi ukashangaa
Sikushika m’simenyo sikutoma mbavaa
Eyo hutedha na mbayo jadi letu watandaa”

17/10/2024

HISTORIYA YA MZEE BWANA KALE
Mzee Bwana kale alizaliwa Ashuwey na alikuwa ni mtoto wa kwanza kwa Javo obo miaka ya kuzaliwa kwake haikuweza kunukuliwa.Katika kuinukia kwake alikuwa ni kijana mwenye upendo na alikuwa na ukarimu sana.
Mzee bwanakale ndio mzee alioishi sana ndani ya mji wa Ashuwey ukilinganisha na ndugu zake wengine kwa alozaliwa nao pamoja na wale wa upande wa mama. Ndugu zake kwa baba na mama walikuwa mwanase na Isheka wa kale na kwa mama walikuwa bahero sizi, shemaka sizi,shali sizi,bwanaheri wa sizi,ngunya wa sizi.
Na ndio watu walioshirikiana sana kujenga msikiti wa Ashuwey kwa mara ya pili. Msikiti kajengwa na watoto wa Shali, watoto wa shemaka na Bahero na mzee bwana kale alikuwa pia walikuwa pamoja kuwendeleza huu msikiti Kwa mara ya pili.
Mzee bwanakale alioa wake wawili, Mwanatosha mke wake wa kwanza na kujaliwa kuwazaa Fatima, Halima, Shebwana, Bibi wa bwana, Javo wa bwana,shali wa bwana,mohamed wa bwana(madi bwana mweusi) na mke wake wa pili alikuwa Mwabule wa Adi alijaliwa nae kuzaa mtoto mmoja akiitwa Mohamed bwana(madi bwana mwehukundu).
Masha Allah katika tumbo la Bwana kale ndio tulojaaliwa wa vyuoni K**a walofanya kazi kubwa katika Nyanja ya elimu ya dini akiwa Mwalimu shamu na mwalimu bwana (Mungu wakundulie kaburi lao na awatanganye na wema).Na mapaka sasa wanao wa walimu hawa wameshikilia gurudumu la kuifundisha dini.
Mzee bwana kale kwa mda mwingi wakukaa Ashuwey family yake iliamua kwenda mwazi kubadilisha maisha, baadhi ya watoto wake walikuwa wakiishi huko. Basi pia hakutaka kuwaacha ndugu zake alovokuwa amekaa nao kwa upendo na ruhuma za wazee. Bwanakale hakuandama msafara alibakia hapo Ashuweyi kwa kauli yake siwezi kuwambiria ndudhangu.
Aliishi nao mpaka umri wake ukawa sasa amekuwa mzee watoto wakaja tena kumchukua alilia Sana bwanakale kusema “imi ntanga wangu ni wahapa Ashuwey hunipeka kwapi inni?”
Bwana kale alipoondoka Ashuwey kwenda mwazi alikaa huko na ndugu zake wa Ashuwey wakiwa humpitia kila mda kwa sababu tayari alikuwa amekuwa mzee.
Kuna wakati kukawa na sherehe kubwa Ashuwey. Alikuwa hutahiriwa mzee shemaka sizi mungu amrehemu. Jamaa wakenda mvundeni kwanza wakenda na ngoma Kisha wakarudi wakaenda mwazi kumtapia mzee bwana kale, walipofika mwazi mzee bwana kale alilia sana. Akatolewa kiti nde na kuanza kumuimbia shemaka sizi. Mzee bwana kale akaimba nae na mashairi yake:
“Sina lakuvachendeaa, nivachendee vanangu?
“Mungu avaondolee, husuda na mato ya kilimwengu”
Hii ni mila ma desturi za wazee wakiimba wakati K**a wa kutahiriwa, harusi, kuvuna au kuchema wakifurahika na kutungiana mashairi.
Kwa mda ukizidi kusonga mbele mzee wetu bwanakale mungu alimpa umri mrefu masha Allah, lakini Kwa kadri ya umri kupita afya yake pia ikawa imekuwa dhaifu na wakati wake ulifika, Mzee bwanakale alifariki ndani ya mwezi wa Ramadhani kwa riwaya wanaosema ilikuwa kumi la pili.
Mzee wetu bwana kale wakati wake ulifika alitaka sana kaburi lake liwe Ashuwey lakini mtanga wake mungu uliliqadiria liwe mwadhi.
Katika kauli yake ya mwisho aliwahi kumuusia mwanae Mohamed bwana kale musinizike mpaka nduzangu waje wanizike kutoka Ashuwey. Na hakuzikwa mpka jamaa waliondoa chombo mzee shali na sizi bahero na jamaa wengi walikowa Ashuwey kwenda kumzika mzee wetu Bwanakale.
Kwa mujibu wa tarehe ya kufa bwanakale ni sawa na siku alozaliwa shangazi yetu mmoja. Kufa kwa bwana kale kwa siku ya tatu yake ndio alizaliwa mwanamina mwenye shangazi anae ishi watamu.

17/10/2024

HISTORIA YA MSIKITI WA ASHUWEYI
Huu msikiti history yake kwanza ulijengwa na mzee sizy fakii ukiwa ni wa udongo, ulijengwa pamoja na watoto wake takriban miaka 1700.
Msikiti ulijengwa Kwa mara ya pili Kwa mawe na watoto wa sizi fakii, kipindi hicho shemaka sizi na bahero sizi walikuwa tayari wamekufa.Inasemekana vifo hivi viwili vilikuwa karibu sana kwa mda wa takriban miaka minne. Ukajengwa na watoto wa Shali, watoto wa shemaka na Bahero na mzee bwana kale alikuwa hai pia walikuwa pamoja kuwendeleza huu msikiti Kwa mara ya pili.
Masha Allah msikiti ukajengwa chini ya mzee Shali wa sizy akiwa yeye ndie kiongozi katika mipangilio ya ujenzi wa msikiti na watu wa mji wote wakashikana pamoja. Inasemekana mara ya pili msikiti ukajengwa na watu wa mji mzima kwa harambee mpaka watu wa mvundeni walikuja kwa harambee ukaasimama tena.
Mwenye kutia maji kwa msikiti wa Ashuwey alikuwa malau shelali na suo wa lali.Malau ndie alimuoa bibi yetu Arabiya shemaka wakamzaa shemaka na Nuru. Kifo cha mzee malau shelali kilitokea ghafla wakati wa alfajiri akitiya maji alianguka ghafla na kufariki. Kifo chake kilishtua mji mzima manake yeye ndio mwenye k**imamia msikiti na nduguyake suo walali, inasemekana mzee Suo alipata mshtuko Sana kwa kuondokewa na ndugu yake, rafiki yake na msaidizi wake. Kifo chake chasemekana ni ugonjwa wakuanguka yaani kifafa. Lakini siku yake ilifika akiwa kwenye kazi ya mungu akundue kaburi lake.
Imam alikuwa ni mzee shali wa sizi akisaidiana na sizi bahero wa sizi, Muhammad bwana kale, Obo shemaka na Sizi wa shali hao ndio wakipanda membari kuhutubu ijumaa. Na muadhin nae alikuwa Muhammad sharif ambae ndugu yake somoe obo, mwana nuru wa suo kwa mama yao akiitwa Bule wa adhuman akisaidiyana na ntikuu adi.
Kisha walikuwa wakiadhini wakisaidiyana ni watoto wao wadogo hapo Mjahid suo, shali wa obo shemaka, Muhamad sizi na shemaka sizi hao wakiadhini wakiwa bado ni vijana mungu awarehemu walioko mbele ya haki.
Kisha kulikuwa na madrasa hapo ubavuni mwa msikiti mwalimu akiwa mzee Shali sizi hapo akisaidiyana na mwanae sizi wa shali hao walijuwa ndio walimu hapo. Sizi wa shali aliwahi kusoma Rasini kwa mwalimu Omar Sidiq alipomaliza
Baada ya mda mzee shali sizy alistaafu akawa hasomeshi tena Na mtoto wake sizy wa shali akasafiri kwenda Mombasa na kuajiriwa port ya kilindini na hapo madrasa ikawa imefungwa kwa mda kidogo.
Mzee shali sizy kabla hajakufa aliwai kutoa wasia kuwa imamu wa msikiti awe ni Muhammad sizy wakimsubiri amelize kusoma kutoka ndau aje amkabidhi msikiti hapo ndipo alifariki akiwa niya yake ampe majukumu Muhammad sizy aendeshe msikiti wa Ashuwey na kushikila madrasa lakini kwa bahati mbaya mji wetu wa Ashuwey tukaugura
Hapo ndio mzee Muhamad sizy akaendeleza madrasa kwa mda masha Allah. Mpaka watu wakaondoka ikiwa madrasa iko mikononi mwa Al maghfur biidhin Llah muhamad sizy mungu amrehemu na alikundue kaburi lake.
Akiwa akisaidiyana na Ntikuu wa adi akiwa ndio muadhini wa hapo msikitini wazee wetu waliishi maisha ya yakiswahaba wakieeneza dini ndani ya mji wetu wa Ashuwey mungu awarehemu wote.
Masha Allah Bwanakale mungu alimpa umri huyo alikuwa nimkubwa wa wote lakini alichelewa kufa albahatika kuishi miaka mingi na ndugu yake kwa mama Ngunya sizi alikufa kipini pia aliwahi kuishi sana baada ya shemaka na bahero ndugu zake kufa. Na bwanakale nae alikufa mwadhi waligura huko kutoka Ashuweyi. Lakini hakuenda huko mpka alipokuwa ashakuwa mzee ndio wanawe wakaja kumtukua pia alikuwa hataki lakini alienda Kwa nguvu za watoto wake. Na bwanakale alipokufa hakuzikwa mpaka akisubiriwa ndugu yake shali wa sizy na watoto wa nduguzake sizi bahero na Muhammad wa bwana kale mtoto wake.
Mzee Obo shemaka alikuwa headman baada ya wazee kundoka kisha na pia akawa na duka lake hapo Ashuweyi.

17/10/2024

Ashuwei ni mji unaopatikana katika eneo la kiunga katika wilaya ya lamu. Inakadiriwa kuwa maeneo haya yote wakaazi wao ni takriban 8000, kulingana na utafiti katika miaka ya tisaini(90s).Upande wa mashariki wa mji wa ashuwei kunapatikana bahari iliyo na takriban kilomita mia kaskazini kuna patikana mpaka wa somalia, magharibi na k**ini kunapatika inchi kavu(bara) iliyo na msitu wa pori, hivo wakaazi wa sehemu hizo walifaidika kwa wanyama wa mwituni k**a nyati, paa na wengine.Wakaazi wa sehemu hii wanatambulika kuwa ni watu wa waliyokuwa na mazingira ya ukulima wa hali ya juu, na uvuvi wa samaki.Ukulima ulikuwa ukifanywa kwenye nyakati za siku za k**i, na uvuvi ulikuwa unafanyika sanaa baadabya jua la masika.Sehemu ya ashuwei inapatikana mvu nyingi sana kutoka mwezi wa nne hadi wa tano na mvua katika kipindi cha mwezi wa kumi hafi mwanzo wa mwezi wakumi na mbili.Neema hii imekuwa kwa takriban miaka mingi na watu walikuwa hawana uhaba wa chakula pia. Inasemekana yoyote alokuwa ameajiriwa na mtu ashuwei wakati wa kuenda kwao alikuwa akipewa mazao yabtakriban mwaka mzima.Inasemekana sehemu hii hakujawahi kukosekana maji, hii ni kutokana na mvua ilokuwa ikinyesha kwa uzuri sana na pia maji yalokuwa kwenye visima yalisawazika kuwa k**a maji ya mvua.Kwa kizungu walijulikana k**a 'militant raiders of somali origin'. Kutokana na uvamizi wa kila mara iliwabidi wakaazi wa mjii huu kuhamia sehemu za miji iliyo karibiana.Baadhi ya ukulima wazee walokuwa wakilima na kuvunwa yalikuwa uguta, mtama, tikitiki, mahindi, peas, maharagwe, malenge. Katika hii mimea ufuta ulikuwa ukivunwa kwa wingi sana.Maisha ya wa kaazi wa ashuwei yaliingia katika babaiko la kutokuwa na usalama kutokana na uvamizi uliokiwa ikifanywa na waasi wa kisomale wanaojulikana k**a 'shifta'. Kuna wanao sema watu walikimbilia sehemu inayojulikana k**a "uso wa tavau" hapo kuna mila. Walikaa kwa mda nakuelekea sehemu za visiwani.Visiwa k**a ndau, rasini, mbwajumwali, mtangawanda na wengine walihamia malindi,Mombasa na wengine kukimbilia inchi za ng'ambo.Kutokana na usalama na utulivu walioupata katika miji waluohamia wakaazi wa ashuwei walikuja na fikra za kutaka kurudi katika ardh zao za jadi ili zumilikibsehemu za wazazi wao.Fikra iliundwa katika mwakanwa 1998 na wazee wakiwemo mzee mjahid suo, mzee suo,Ali shemaka na shemaka sizi, mohamed sizi, bahero adi, mwalimu shamu, bahero omar(Almaghufur biidhin llah). Fikra hii pia alikuwa ndugu sizi shemaka(Almaghufur biidhin llah).Vikao vya fikra hii vilikuwa vikifanywa kwa mwalimu shamu akiwa ndie kiongozi wao.Safari ilipangwa wakati huo na wazee wakaenda sehemu zao mzuri wakia na azma ya kuzirudisha kwenye umiliki wa watu wa ashuwei.Wazee waliopoenda walikuwa na azma moja, ardhi ya ashuwei iwe ni community land kwa kila mtu ambae ana asli ya ashuwei aweze kufaidika na ardhi hii iliyojaa neema.Mashallahnwazee walipambana na vizuizi vingi katika safarii hii lakini fikra yao haikuwa mwisho, baadhi ya wavamizi kutoka familia zenye nguvu waliwahai kuziregesha ardhi na title zao kuwa revoked yaani kubatilishwa.Wazee wengingi walienda mbele ya mungu ikiwa walobakia wameishiwa na nguvu.. Leo fikra hii iko mikononi sote vijana... Na tukaamua tuendeleze ukombozi wa ardhi yetu...

Send a message to learn more

Address

Lamu

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ashuwey Farmers and welfare group posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share

Category