06/07/2026
Mnamo tarehe 1 Julai 2026, tulipata fursa ya kutembelea ofisi ya Mhifadhi Mkuu wa Tarangire na kubadilishana mawazo kuhusu fursa ya kufungua lango litakalounganisha watalii kati ya Randilen WMA na Tarangire NP kupitia eneo la Lemiyoni (Serengeti Ndogo).
Katika majadiliano hayo, ilikubaliwa kuanzishwa Lango la Muda (Temporary Gate) ili kuanza kuhudumia wageni haraka iwezekanavyo wakati maandalizi ya ujenzi wa lango la kudumu yakiendelea. Aidha, ilikubaliwa kuwa lango hilo litaitwa Lemiyoni Gate.
Tunatoa shukrani za dhati kwa Mkurugenzi mstaafu na mwanzilishi wa Honeyguide kwa kuonyesha utayari wa kusaidia ujenzi wa lango la muda pamoja na kutoa ushauri katika kila hatua ya utekelezaji. Shukrani za pekee pia ziende kwa Menejimenti ya TANAPA na Mkuu wa Hifadhi ya Tarangire kwa kutambua umuhimu wa mradi huu.
Mwisho, tunampongeza Mkuu wetu wa Wilaya, viongozi wa Randilen WMA na wawekezaji wetu kwa ushirikiano wao katika safari ya miaka mitano ya kufanikisha ndoto ya kupatikana kwa lango hili muhimu.