04/09/2026
"Tunawajibu wa kutafsiri matarajio ya Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa vitendo".RC Shigela
Ameyasema hayo leo Septemba 4,2026 Mkoani Manyara baada ya kupokea Hati ya makabidhiano ya Ofisi ya Mkoa wa Manyara kutoka kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Sendiga ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
Aidha amewataka Viongozi wa ngazi zote kujipanga kukabiliana na mabadiliko ya tabia Nchi kufuatia tahadhari iliyotolewa na mamlaka ya Hali ya hewa Tanzani (TMA) kuhusu uwepo wa mvua za Elnino Oktoba 2026.
Kwa upande wake Mhe.Queen Sendiga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ameeleza kuwa Mkoa wa Manyara ni salama,pia amewataka Watumishi na Watendaji wa Mkoa wa Manyara kutoa ushirikiano kwa kiongozi huyo ili aweze kutimiza majukumu yake kikamilifu.
"Mkoa wa manyara umekuwa Chuo kwangu umenifundisha vitu vingi, nawakaribisha sana Morogoro",nimefurahi kukabidhi Mkoa wa Manyara kwa Mhe. Martine Shigela nakutakia majukumu mema". ameeleza
OFISI YA WAZIRI MKUU TAMISEMI OFISI YA WAZIRI MKUU Manyara Rs Shaaban Mpendu Msemaji Mkuu wa Serikali Maelezo News Ikulu Tanzania