Hospitali Ya Rufaa Ya Mkoa,Bukoba BRRH

Hospitali Ya Rufaa Ya Mkoa,Bukoba BRRH Huu ni ukurasa rasmi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba. Karibu kwa huduma bora

WATUMISHI WASISITIZWA UMUHIMU WA KUZINGATIA MIONGOZO YA IPCWatumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba, wameendelea ...
28/08/2026

WATUMISHI WASISITIZWA UMUHIMU WA KUZINGATIA MIONGOZO YA IPC

Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba, wameendelea kusisitizwa umuhimu wa kuzingatia miongozo ya Kinga na Udhibiti wa Maambukizi (IPC) katika utoaji wa huduma za afya ili kuhakikisha usalama wa wagonjwa pamoja na watumishi.

Rai hiyo imetolewa na Dkt. Chrisogone German Kutoka Wizara ya Afya wakati akiwasilisha taarifa kwa watumishi wa hospitali hiyo baada ya kukamilika kwa zoezi la ufuatiliaji IPC lililosimamiwa na Timu ya kutoka Wizara ya Afya kwa kushirikiana shirika la CIHEB Tanzania kupitia Mradi wa Usalama wa Afya Duniani.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, amesisitiza watumishi kuzingatia matumizi sahihi ya vifaa kinga binafsi (PPE) wakati wa kutekeleza majukumu yao, akieleza kuwa matumizi hayo ni muhimu katika kujikinga dhidi ya maambukizi na kulinda usalama wa wagonjwa wanaopatiwa huduma.

Aidha, ameishukuru Timu ya Uboreshaji Ubora (QI) ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba, kwa kuendelea kusimamia kwa karibu shughuli za kila siku za hospitali na kuhakikisha utoaji wa huduma unazingatia miongozo na viwango vinavyotakiwa.

Ameitaka Timu hiyo kuendelea kusimamia utekelezaji wa miongozo ya IPC katika maeneo yote ya hospitali na kuhakikisha watumishi wanaendelea kuzingatia taratibu hizo ili huduma za afya ziendelee kutolewa kwa usalama na ubora zaidi.

Kwa upande wake, Afisa Tawala na Rasilimali Watu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba, Simon Njeya, akitoa neno kwa niaba ya Mganga Mfawidhi, ameishukuru Timu ya IPC kutoka Wizara ya Afya kwa kuendelea kutembelea hospitali hiyo na kutoa ushauri wa kitaalamu unaolenga kuboresha utoaji wa huduma.

Njeya ameahidi kuwa uongozi wa hospitali utafanyia kazi ushauri na maeneo yote yaliyoainishwa kuwa yanahitaji maboresho, huku akisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya watumishi na timu mbalimbali katika kuhakikisha miongozo ya IPC inatekelezwa ipasavyo.

Zoezi hilo limekuwa sehemu ya juhudi za kuimarisha Kinga na Udhibiti wa Maambukizi .

WATUMISHI WA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA, BUKOBA WATEMBELEA IRINGA RRH NA DODOMA RRH KWA AJILI YA KUBADILISHANA UZOEFUWat...
23/08/2026

WATUMISHI WA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA, BUKOBA WATEMBELEA IRINGA RRH NA DODOMA RRH KWA AJILI YA KUBADILISHANA UZOEFU

Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba (BRRH) wamefanya ziara katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Iringa (Iringa RRH) na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma (Dodoma RRH), kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kujifunza mbinu mbalimbali zinazotumika katika kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.

Katika ziara hiyo, watumishi hao walipata fursa ya kutembelea idara na vitengo mbalimbali vya hospitali hizo, ambapo walijifunza namna watumishi wanavyotekeleza majukumu yao, kutoa huduma kwa wagonjwa na kuboresha mifumo ya utoaji wa huduma.

Ziara hiyo pia ilitoa fursa kwa watumishi kutoka pande zote mbili kubadilishana uzoefu, mawazo na mbinu mbalimbali za kiutendaji zinazoweza kusaidia kuongeza ufanisi na ubora wa huduma zinazotolewa kwa wananchi.

Akitoa neno la shukrani baada ya ziara hiyo, Dkt. Renatus Francis, ambaye alikuwa Mkuu wa Msafara wa watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba waliotembelea Iringa RRH, ameushukuru uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Iringa pamoja na watumishi wote kwa mapokezi mazuri na ushirikiano walioutoa wakati wa ziara hiyo.

Dkt. Francis amesema ziara hiyo imekuwa na manufaa makubwa kwa watumishi wa Bukoba RRH, kwani wamepata fursa ya kujifunza namna hospitali hiyo inavyotekeleza majukumu yake na kubaini maeneo mbalimbali ambayo wanaweza kujifunza na kuyatumia katika kuboresha huduma katika hospitali yao.

Kwa upande wake, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Iringa, Dr Pamela Mosha amewashukuru watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba kwa kuichagua Iringa RRH kuwa miongoni mwa vituo vya kujifunza na kubadilishana uzoefu.

Dkt. Mosha amesema ziara hiyo haikuwa na manufaa kwa watumishi kutoka Bukoba pekee, bali pia imekuwa fursa kwa watumishi wa Iringa RRH kujifunza mambo mapya kutoka kwa wenzao wa Bukoba.

Amesema kubadilishana uzoefu miongoni mwa watumishi wa hospitali ni muhimu

HABARI PICHA: Marehemu Enock Reynard Kawogo apumzishwa kwenye nyumba yake ya milele katika kijiji cha Ikisa kata ya Uwem...
19/08/2026

HABARI PICHA: Marehemu Enock Reynard Kawogo apumzishwa kwenye nyumba yake ya milele katika kijiji cha Ikisa kata ya Uwemba Mkoni Njombe.

Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa,Bukoba wakisaini kitabu cha Maombolezo ikiwa ni ishara ya kuendelea kumuenzi mtu...
17/08/2026

Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa,Bukoba wakisaini kitabu cha Maombolezo ikiwa ni ishara ya kuendelea kumuenzi mtumishi mwenzao Enock Reynard Kawogo aliyefariki tarehe 15.08.2026

Pumzika kwa Amani, Tutakukumbuka Daima
15/08/2026

Pumzika kwa Amani, Tutakukumbuka Daima

Happy 88 Day
08/08/2026

Happy 88 Day

JAMII YAKUMBUSHWA UMUHIMU WA UNYONYESHAJI WA MTOTOJamii imeendelea kukumbushwa umuhimu wa unyonyeshaji wa mtoto k**a nji...
06/08/2026

JAMII YAKUMBUSHWA UMUHIMU WA UNYONYESHAJI WA MTOTO

Jamii imeendelea kukumbushwa umuhimu wa unyonyeshaji wa mtoto k**a njia muhimu ya kuhakikisha mtoto anakua akiwa na afya njema, lishe bora na kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Rai hiyo imetolewa na Mkunga Bingwa wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba, Gloria Kagaruki, wakati akitoa elimu kuhusu umuhimu wa unyonyeshaji katika kipindi cha Wiki ya Unyonyeshaji Duniani kupitia Kituo cha Redio Mbiu kilichopo mkoani Kagera.

Bi. Kagaruki amesema mtoto anatakiwa kuanza kunyonya ndani ya saa moja baada ya kuzaliwa kwani maziwa ya mwanzo (colostrum) yana virutubisho na kingamwili muhimu zinazomkinga mtoto dhidi ya magonjwa na kumsaidia kukua vizuri.

Aidha, amesisitiza kuwa mtoto anapaswa kunyonya maziwa ya mama pekee kwa kipindi cha miezi sita ya kwanza bila kuongezewa chakula au kinywaji chochote.

"Katika kipindi cha miezi sita ya kwanza mtoto hatakiwi kupewa maji, juisi, maziwa ya kopo wala chakula kingine chochote. Maziwa ya mama yanatosha kumpa mtoto chakula, maji na virutubisho vyote vinavyohitajika kwa ukuaji wake," amesema Bi. Kagaruki.

Ameeleza kuwa unyonyeshaji wa maziwa ya mama humsaidia mtoto kupata kinga dhidi ya magonjwa ya kuhara, nimonia na maambukizi mengine, huku ukichangia ukuaji mzuri wa ubongo, kuimarisha uhusiano kati ya mama na mtoto na kupunguza hatari ya utapiamlo.

Kwa upande wa mama, amesema unyonyeshaji husaidia kupunguza damu kutoka baada ya kujifungua, huchangia mfuko wa uzazi kurudi katika hali yake ya kawaida kwa haraka, hupunguza hatari ya kupata saratani ya matiti na ovari, na pia husaidia kupanga uzazi kwa muda endapo mama atafuata masharti ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama pekee.

Bi. Kagaruki ameishauri jamii, hususan akina mama wajawazito na wanaonyonyesha pamoja na familia zao, kuzingatia ushauri wa wataalamu wa afya kuhusu unyonyeshaji sahihi ili kuhakikisha watoto wanapata mwanzo bora wa maisha na kukua wakiwa na afya njema.

Usikose kutufuatilia
04/08/2026

Usikose kutufuatilia

HABARI PICHA: Menejimenti Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Bukoba,  ikiwa katika kikao cha tathmini ya Kimatibabu (Clinical Au...
02/08/2026

HABARI PICHA: Menejimenti Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Bukoba, ikiwa katika kikao cha tathmini ya Kimatibabu (Clinical Audit) kilichoendeshwa na watumishi kutoka Wizara ya Afya ikikiwa na lengo la kupima, kutathmini na kuboresha ubora wa huduma za afya zinazotolewa kwa wananchi.

SIKU YA HOMA YA INI DUNIANI.Wizara ya Afya Tanzania
28/07/2026

SIKU YA HOMA YA INI DUNIANI.Wizara ya Afya Tanzania

Address

P. O. BOX 265
Bukoba

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Hospitali Ya Rufaa Ya Mkoa,Bukoba BRRH posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share