Bukoba water supply and sanitation Authority

Bukoba water supply and sanitation Authority Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Bukoba water supply and sanitation Authority, Government Organization, BOX 81, Bukoba.

21/07/2026
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bukoba (BUWASA) Ndugu John Sirati jana tarehe 16/07/202...
16/07/2026

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bukoba (BUWASA) Ndugu John Sirati jana tarehe 16/07/2026 alifanya kikao na Watumishi wote wa Mamlaka kwa lengo la kuimarisha ushirikiano, kuongeza ufanisi wa utendaji kazi na kujadili mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka.

Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji aliwataka watumishi kuendelea kuzingatia maadili ya utumishi wa umma, kufanya kazi kwa weledi, uwajibikaji na uadilifu, huku akisisitiza umuhimu wa kutoa huduma bora kwa wananchi na kuhakikisha wateja wanapata huduma za maji safi na usafi wa mazingira kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.

" *Sitasita kumchukulia hatua Mtumishi yoyote anayekiuka taratibu za kazi ikiwemo Watumishi wasiowaaminifu wanaoshirikiana na wateja kuihujumu Mamlaka "alisema Bw, Sirati.*

Aidha, alisisitiza ushirikiano kati ya idara na vitengo mbalimbali ili kuongeza tija, kufanikisha malengo ya Mamlaka na kuimarisha mahusiano mazuri na wateja.

Kwa upande wao, watumishi walipata nafasi ya kutoa maoni, kuuliza maswali na kutoa mapendekezo yaliyolenga kuboresha mazingira ya kazi pamoja na utoaji wa huduma.

Mkurugenzi Mtendaji aliahidi kuyafanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa kwa manufaa ya Mamlaka na wananchi wanaohudumiwa.

Kikao hicho kilihitimishwa kwa wito kwa watumishi wote kuendelea kufanya kazi kwa bidii, kushirikiana na kudumisha mshik**ano ili kuhakikisha BUWASA inaendelea kutoa huduma bora, endelevu na zenye kukidhi matarajio ya wananchi.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO NA UHUSIANO BUWASA
16/07/2026

Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bukoba (BUWASA), ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Bw. ...
27/06/2026

Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bukoba (BUWASA), ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Bw. Samora Lyakurwa imefanya kikao chake cha mwisho cha kipindi cha uongozi wake kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano BUWASA.

Kikao hiki kililenga kupitia utekelezaji wa mipango, maendeleo ya miradi pamoja na utendaji wa Mamlaka katika kuhakikisha huduma za majisafi na usafi wa mazingira zinaendelea kuboreshwa kwa wananchi.

Katika kikao hicho, wajumbe walipitia taarifa mbalimbali za utekelezaji wa miradi ya maendeleo, wakajadiliana kuhusu mafanikio yaliyopatikana, changamoto zilizojitokeza pamoja na mikakati ya kuendeleza maboresho katika utoaji wa huduma. Bodi ilieleza kuridhishwa na hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa miradi na kusisitiza umuhimu wa kuendelea kusimamia miradi hiyo kwa ufanisi, uwazi na kuzingatia thamani ya fedha.

Akihitimisha kikao hicho, Mwenyekiti wa Bodi, Bw. Lyakurwa aliwashukuru na kuwapongeza wajumbe wote wa Bodi kwa ushirikiano, kujituma na mchango wao mkubwa katika kusimamia maendeleo ya BUWASA katika kipindi chote walichohudumu.

Aidha, aliipongeza Menejimenti na watumishi wa BUWASA kwa ushirikiano waliouonesha katika kutekeleza maamuzi ya Bodi na kuhimiza kuendelea kufanya kazi kwa weledi, ubunifu na uwajibikaji ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata huduma bora, salama na endelevu za majisafi na usafi wa mazingira.

"BUWASA itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuimarisha utoaji wa huduma bora, ikiwa ni sehemu ya dhamira yake ya kuboresha ustawi wa wananchi na kuchochea maendeleo" aliongeza Bw Lyakurwa.

Bodi ya Wakurugenzi BUWASA inatarajiwa kumaliza muda wake tarehe 30,June 2026 baada ya kutumikia Bodi hii kwa muda wa miaka mitatu.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO NA UHUSIANO BUWASA
26/06/2026

Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Nishati na maji( EWURA) imefanya ziara ya ukaguzi katika Mamlaka ya Majisafi na Usafi w...
31/05/2026

Mamlaka ya udhibiti wa huduma za Nishati na maji( EWURA) imefanya ziara ya ukaguzi katika Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bukoba(BUWASA) kwa lengo la kutathmini utendaji kazi wa Mamlaka hiyo na kuona k**a imefikia vigezo na viwango vilivyowekwa na EWURA katika utoaji wa huduma za maji safi na usafi wa Mazingira.

Kikao hicho kilifunguliwa rasmi na Mkurugenzi Mtendaji wa BUWASA Bw.John Sirati kwa kushirikiana na timu ya EWURA, ambapo Mhandisi Joseph Ngeleja alisema kuwa ukaguzi huo unalenga kupima ufanisi wa Mamlaka katika maeneo mbalimbali ikiwemo utoaji wa huduma kwa wananchi, ubora wa maji, usimamizi wa miundombinu, ukusanyaji wa mapato pamoja na utatuzi wa changamoto za wateja.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa BUWASA aliishukuru timu ya EWURA kwa kufanya ziara hiyo muhimu, akieleza kuwa tathmini hiyo ni fursa ya kujifunza na kuendelea kuboresha utendaji kazi wa Mamlaka ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, salama na endelevu.

“Mamlaka itaendelea kushirikiana kwa karibu na EWURA katika kuhakikisha viwango vya utoaji huduma vinaendelea kuimarika. Tathmini hizi zinatusaidia kuongeza uwajibikaji, uwazi na ufanisi katika kuwahudumia wananchi wetu,” alisema Bw John Sirati Mkurugenzi Mtendaji wa BUWASA.

Aidha, kikao hicho kilihusisha majadiliano mbalimbali kuhusu namna ya kuendelea kuboresha huduma za maji safi na usafi wa Mazingira kwa wananchi wa Bukoba sambamba na kuzingatia vigezo na miongozo inayotolewa na EWURA.

Timu hii iko Mkoani Kagera kwa ziara ya siku Tatu.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO NA UHUSIANO, BUWASA
29/05/2026

Mamlaka ya majisafi na usafi wa Mazingira Bukoba (BUWASA) imefanya kikao cha pamoja na k**ati ya ushauri wa huduma za Ni...
29/05/2026

Mamlaka ya majisafi na usafi wa Mazingira Bukoba (BUWASA) imefanya kikao cha pamoja na k**ati ya ushauri wa huduma za Nishati na maji ya EWURA Consumer Consultative Council (EWURA CCC) kwa lengo la kujadili mikakati mbalimbali ya kuboresha huduma kwa wateja na kutatua changamoto za malalamiko yanayohusu huduma ya maji kilichofanyika ukumbi wa mikutano BUWASA.

Akifungua kikao hicho kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Bi Julieth Shangali aliwashukuruku EWURA CCC kwa kuona haja ya kukutana na kujadiliana namna ya kushirikiana kuboresha huduma ya maji na kutatua changamoto za wateja.

"Kikao hiki ni muhimu sana kwani kinalenga kuboresha huduma na kuweka mikakati ya kuboresha kwani EWURA CCC nyie ndiyo mko karibu zaidi na wateja naamini kupitia kikao hiki tunaenda kuweka mikakati madhubuti ya kuboresha huduma,"aliongezea Bi Julieth Shangali,Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na uhusiano BUWASA.

Katika kikao hicho,pande zote mbili zilijadiliana kwa kina namna ya kuimarisha mawasiliano kati ya Mamlaka na wateja, kuongeza kasi ya kushughulikia malalamiko pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi sahihi ya huduma za maji na taratibu za kuwasilisha changamoto zao.

Aidha viongozi waliohudhuria walisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Taasisi na wananchi katika kuhakikisha huduma za maji zinakuwa bora ,salama na za kuaminika wakati wote.Pia walieleza kuwa maoni na malalamiko ya wananchi ni sehemu muhimu katika kuboresha utoaji wa huduma.

Kwa upande wake,EWURA CCC iliahidi kuendelea kushirikiana na BUWASA katika kutoa elimu kwa watuamiaji wa huduma za maji pamoja na kufuatilia utekelezaji wa maboresho yanayolenga kuongeza kuridhika kwa wateja.

Kikao hiki kilihudhuriwa na Menejimenti ya BUWASA,Bi Anadorice Komba,Afisa Mwandamizi huduma kwa wateja EWURA CCC (M),Bw.Najim Bwanika Mwenyekiti wa k**ati ya Watumiaji wa huduma za Nishati na maji (M) ,pamoja na Bw.Lenas Katabazi Mjumbe wa Kamati ya Watumiaji wa Huduma za Nishati na maji Mkoa wa Kagera.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO NA UHUSIANO, BUWASA
29/05/2026

Mamlaka ya majisafi na usafi wa Mazingira Bukoba (BUWASA)imeendelea kutoa elimu kwa wakazi wa Manispaa ya Bukoba  kuhusu...
23/05/2026

Mamlaka ya majisafi na usafi wa Mazingira Bukoba (BUWASA)imeendelea kutoa elimu kwa wakazi wa Manispaa ya Bukoba kuhusu utunzaji na ulinzi wa miundombinu ya maji.

Akiongea kwenye Mkutano wa mtaa uliofanyika mtaa wa Bulibata Kata ya Buhembe Mkuu wa kitengo cha mawasiliano na uhusiano BUWASA Bi Julieth Shangali aliwafahamisha wadau hawa kuwa kumekuwa na wimbi la wizi wa dira za maji na tape za maji ambao umetokea kwenye baadhi ya kata za Manispaa ya Bukoba.

"Hivyo kupitia kikao hiki tumekuja kuwatahadharisha na kuwataka kuchukua hatua za kulinda dira na miundombinu ya maji kwa ujumla kwani endapo mteja ataibiwa dira ya maji atalazimika kulipia dira mpya ili aweze kuendelea kupata huduma ya maji".

Aidha Bi Julieth aliwaasa wadau kujenga tabia ya kulipia bili ya maji pindi anapoipata kwani kwa kufanya hivyo atakuwa amechangia katika kuboresha huduma na kuifanya iwe endelevu kwani kupitia bill za maji Mamlaka inaweza kumudu gharama mbalimbali za uendeshaji ikiwemo za umeme na madawa.

"Kwa upande wa vilula vilivyofungwa kutokana na madeni Ofisi inaenda kuweka utaratibu wa kuvifungua ikiwa ni pamoja na kufuatilia wadaiwa waliokuwa wanavisimamia kwa kumtumia Mwanasheria wa Mamlaka ili madeni haya yaweze kulipwa na wananchi waendelee kupata huduma hii kwani vilula hivi vilijengwa kwa lengo la kusaidia wananchi wenye kipato cha chini ili waweze kupata huduma hii kwa gharama nafuu na kwa umbali mfupi" ,aliongeza Bi Julieth Shangali.

Akiongea kwenye kikao hiki Bi Devotha Koy Kaimu Mkurugenzi wa huduma kwa mteja aliwaomba wadau kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za uvujaji wa mabomba ikiwa ni pamoja na kulipa bill zao kwa wakati kwa kutumia namba ya malipo inayotumwa kwenye bill zao na siyo kumpatia fundi hela

"Kwa wateja wenye madeni Ofisi iko tayari kuwarudishia huduma wanaodaiwa kwa kuingia mkataba wa kulipia deni kidogo kidogo huku wakiendelea kupata huduma ya maji", aliongezea Bi Devotha Koy.

Kikao hiki kilihudhuriwa na viongozi wa mtaa wa Bulibata ,Watumishi kutoka BUWASA pamoja na wakazi wa mtaa wa Bulibata.

IMETOLEWA NA KITENGO MAWASILIANO NA UHUSIANO, BUWASA.

21/05/2026

Address

BOX 81
Bukoba
BUKOBA

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Bukoba water supply and sanitation Authority posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share