23/10/2020
DUNIA INAHITAJI AMANI
Hakika dunia inahitaji amani, Afrika Ulaya Asia marekani na kwengineko wimbo ni amani lazima tuilinde amani.
Bila shaka amani ni jambo kubwa na hii inaleta tanbihi kwetu juu ya kujua umuhimu wa kujifunza jinsi ya kuijenga kuitunza na kuidumisha amani katika mataifa yetu.
Kujifunza kujua hali halisi wakati wa amani lakini pia kujua hali wakati inapokosekana amani katika jamii zetu na hata katika ngazi ya familia mpaka taifa na kimataifa.
Ziangalie familia, jamii na hata nchi na mataifa yaliyokuwa katika amani na utulivu, lakini baadae yakajisahau na kujiingiza katika machafuko hivi sasa hali za familia jamii au nchi na mataifa hayo zikoje !?
Tujifunze pia historia ya machafuko chanzo chake mara nyingi ni nini hasa, hapo utagundua kuwa ni matumizi mabaya ya uhuru wa mitandao ya kijamii.
Lakini sababu nyingine ni pamoja na tamaa ya madaraka siasa za kichochezi pengine kwa kupitia mgongo wa dini ukabila au kisingizio cha kudai haki kwa malengo tofauti.
Tunza amani kwa faida yako jiepushe na jiweke mbali kabisa na sababu zote za uvunjifu wa amani na utulivu katika ngazi zote za kijamii kitaifa na kimataifa.
Dumisha amani kwa faida yako kizazi cha sasa na cha baadae, maendeleo yoyote bila amani hayawezi kufikiwa.
Hata mataifa yanayouza silaha yenyewe hayataki machafuko katika nchi zao ili yafaidi matunda ya kazi yao kwa amani na utulivu hawataki vita katika nchi zao.
Mo Hasanaly
[email protected]