20/12/2025
ROHO YA AIBU ITAKUACHIA LEO KWA JINA LA YESU.π ISAYA 54: 4π₯
AIBU NI NINI?π€
Aibu na fedheha ni roho ambayo shetani huitumia kumshambulia mtu, kwalengo la kumuvua mtu Utukufu na Heshima ya Mungu kwenye maisha yake.
Pia Aibu ni roho inayo tafuna matokeo ya kazi na juhudi za mtu ili kumwaibisha baadae mfano inaweza kuharibu kazi, ndoa, uchumi, afya, mahusiano, au kibali yani ntotaβοΈ YEREMIA 3: 24π₯
Roho ya aibu inapokuvamia
Inakuja na (Dhihaka, Fedhehaπͺ na Hofu)
Dhihaka hutumika k**a shambulio kutoka kwa watu wainje, ili kuku dhoofisha na kuongeza ukubwa wa kosa lako au aibu yako,
Fedheha hutumika k**a mlango wa kujihukumu nakujiona kuwa wewe siyo kitu na hufai tena kwa lolote, ujasiri wakufanya lolote unapotea
Hofu, huchukua nafasi kwenye maisha ya mtu nauwezo wake wa ndani unakufa kila anacho jaribu kufanya anaogopa nakuona hawezi, hapo ndipo wengi hujitenga na upweke kutawala kwenye maisha ya mtu mpaka kufikia kujiua.πͺ
ROHO YA AIBU ILITOKA WAPI? MWANZO 3: 7- 10π₯
Ukisoma hapo utagundua roho ya aibu niwakala wakwanza washetani, kabla ya kifo, kabla ya magonjwa, kabla ya umasikini, hata kabla ya laana ya aridhi.
Roho ya aibu nisilaha yakwanza ambayo shetani hutumia baada ya kufanikisha kuingiza dhambi au kosa kwa mwanadamu.
Ukisoma hiyo Mwanzo 3: 7π₯ utaona baada ya Adamu kula tunda tu walifumbuliwa macho wakajiona wako uchi wakaona (Aibu)wakaenda kujificha, tayari unaona aibu imejitokeza na kuwatia hofu
Aibu ni roho yapili baada ya dhambi.
Mpendwa, unaweza kuwa unapita kwenye hali k**a hii roho ya aibu imekuvamia inataka kukufedhehesha kwa njia ya kosa ulilo tenda au kwa njia ya madhaifu yako mbali mbai au madeni na unajiuliza natokaje kwenye hali hii?
Usiogpe Yesu alidhihilishwa ili azivunje kazi za shetani kwenye maisha yako
1YOHANA 3: 8π₯
NASHINDAJE ROHO YA AIBU?
Hatua ya kwanza tubu mwambie Mungu nisamehe makosa yangu yote niliyotenda kwa kujua na kutokujua.π unioshe kwa damu ya Yesu ZABURI 51: 1- 4π₯
Hatua ya pili mwombe Mungu akurejeshee nafasi uliyoipoteza kiroho, kiuchumi, kiheshima, kikazi au kibiashara, na akufunike kwa utukufu wake.π
Baada ya hapo uutapata amani na tumaini jipya ndani yako, utaanza kuona ukirejea kwenye uwezo wako taratibu na aibu itaondoka kwakoπ
Baada ya hayo Mungu anakuahidi kuwa ataiondoa aibu yako na haitakumbukwa tena ISAYA 54: 4π₯
MUNGU AKUBARIKI NA KU FUTA AIBU JUU YAKO NA WATOTO WAKOπ
Kwa maombi na maombezi piga π²+255716822126βοΈ
βοΈby Fahim Rasham π₯