17/04/2026
ZINGATIA MAMBO MUHIMU UNUNUAPO KIWANJA
Kwenye sekta ya ardhi kuna mambo mengi sana.
Migogoro mingi ya ardhi unayoiona inatokana na tamaa za wauzaji na pia kutokuwa na elimu sahihi kwa mtu anayenunua kiwanja.
Wakati mwingine Hati pekee haitoshi kuwa kigezo cha kununua kiwanja na kuamini kuwa kiwanja hiko ni salama.
Wapo watu wengi Tanzania wamepoteza fedha kwa sababu waliamini tu kiwanja kina hati tu bila kufanya uhakiki wa mambo mengine muhimu.
K**a unataka kununua kiwanja mkononi kwa mtu namaanisha sio kwenye kampuni basi zingatia mambo haya pia:
1. Uhalali wa hati
Hakikisha hati imehakikiwa kwenye ofisi za ardhi husika. Zipo hati zimewahi kughushiwa au kuuzwa kwa watu zaidi ya mmoja hivyo kufanya uhakiki ni muhimu hasa k**a wewe ni mgeni na unanunua mkononi kwa mtu na sio kwenye kampuni.
2. Ifahamu Historia ya kiwanja
Uliza kiwanja kilikuwa cha nani kabla.
Kwanini kinauzwa.
Wakati mwingine migogoro hutokea kwa sababu ya urithi au familia kudai haki.
3. Uliza Mipaka ya kiwanja
Naam tembelea eneo na uhakikishe mipaka inaonekana wazi na majirani wanaijua ili kuepusha kero za kugombania mipaka.
4. Omba Ramani ya eneo (Survey Plan)
Hakikisha kiwanja kipo kwenye ramani rasmi na sio kuonyeshwa tu kwa maneno.
5. Fika Serikali ya Mtaa/Kijiji
Pata uthibitisho kutoka kwa serikali ya mtaa au kijiji ili kujua k**a kuna mgogoro wowote.
6. Hakiki Matumizi ya ardhi
Angalia k**a eneo limetengwa kwa makazi, biashara, au matumizi mengine. Watu wengine hununua viwanja kwenye maeneo yaliyopangwa kwa matumizi tofauti.
7. Tembelea eneo mara kadhaa
Usinunue kiwanja kwa kuonyeshwa picha au kuambiwa tu. Nenda mwenyewe ukaone mazingira.
Upate kuhakiki kwenye picha na video ulizoziona je ni sawa?
Zingatia;
Kuna faida nyingi na hasara chache kununua viwanja/mashamba kwenye kampuni kuliko kununua mkononi kwa mtu.
Miongoni mwa faida kubwa ni kuwa msululu wa uhakiki unakua umeshafanywa na kampuni na ndio maana wanauza lakini pia ikitokea changamoto kampuni iliyokuuzia inawajibika kukutatulia changamoto hizo labda nao wawe matapeli ndio hawataweza kukutatulia changamoto ya eneo umenunua kutoka kwao.
KARIBU SANA LAND FOCUS
WASILIANA NASI Whatsapp 0740 188 210
Ofisi zetu zipo Goba njia nne