Taficotz

Taficotz Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Taficotz, Government Organization, P. O. Box 2336, Dar es Salaam.

Ukurasa Rasmi wa Shirika la Uvuvi Tanzania
Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) ni Shirika lenye dhamana ya kukuza sekta ya uvuvi nchini kupitia Uvuvi wa Bahari Kuu

29/08/2026
24/08/2026
DKT. KIULA AWASILI RASMI TAFICO, AHIMIZA UWAJIBIKAJI NA UBUNIFUAfisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO)...
14/08/2026

DKT. KIULA AWASILI RASMI TAFICO, AHIMIZA UWAJIBIKAJI NA UBUNIFU
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), Dkt. Suleiman Peter Kiula, ndc, leo Agosti 14, 2026, amewasili rasmi ofisi za Makao Makuu ya Shirika zilizopo Kigamboni Dar es Salaam, na kuzungumza na watumishi wa Shirika, akisisitiza umuhimu wa mshik**ano, nidhamu na uwajibikaji katika kutekeleza majukumu ya TAFICO.

Dkt. Kiula amesema TAFICO ina majukumu makubwa katika mnyororo wa thamani wa sekta ya uvuvi, ikiwemo uendeshaji wa meli, bandari, viwanda vya uchakataji wa mazao ya uvuvi pamoja na kuingia katika ufugaji wa samaki.

Katika kuyafanikisha malengo ya Shirika, Dkt. Kiula ametoa rai kwa watumishi kuwa sehemu ya Shirika na kila mmoja kuwa kiongozi katika eneo lake la utendaji, huku akisisitiza nidhamu na ushirikiano.

“Tutasimama pamoja, tutashirikiana ili tutengeneze historia ya sekta ya uvuvi nchini. TAFICO inaanza safari ya kwenda kuingia bahari kuu.” alisisitiza.

TAFICO INAKWENDA KUWA INJINI YA UCHUMI WA BULUU - DKT. KIULAShirika la uvuvi Tanzania (TAFICO) limeelezea dhamira ya kuw...
12/08/2026

TAFICO INAKWENDA KUWA INJINI YA UCHUMI WA BULUU - DKT. KIULA
Shirika la uvuvi Tanzania (TAFICO) limeelezea dhamira ya kuwa injini na nyenzo ya kimkakati katika utekelezaji wa Dira 2050, hususani kujenga uchumi wa buluu, kujenga ajira, kuleta mapato ya fedha za kigeni, kukuza viwanda vinavyotegemea rasilimali za maji na kuchochea kasi ya miundombinu ya uvuvi.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa TAFICO, Dkt. Suleiman Kiula, ndc, leo Agosti 12, 2026, wakati akichangia mada kuhusu “Mapinduzi katika Uvuvi na Ukuzaji Endelevu wa Viumbe Maji katika Kuchochea Utekelezaji wa Dira 2050”, kwenye Kongamano la Uchumi wa Buluu linalofanyika Kizimkazi, Zanzibar.

Dkt. Kiula alikuwa akijibu swali la Muongoza Mada, Prof. Mohammed Sheikh, ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), aliyetaka kufahamu namna TAFICO ilivyojipanga katika kutekeleza jukumu lake la kuinua sekta ya uvuvi nchini.

Akijibu, Dkt. Kiula alisema TAFICO ni Shirika lenye uwezo wa kuchochea mnyororo mzima wa thamani wa sekta ya uvuvi, kuanzia uzalishaji hadi uchakataji na uongezaji thamani.

“TAFICO inakwenda kuwa injini ya Uchumi wa Buluu nchini. Inakwenda kuwa nyenzo muhimu katika maendeleo ya sekta ya uvuvi nchini,” alisema Dkt. Kiula.

Kauli hiyo inatokana na hatua ambazo TAFICO tayari imeanza kuchukua katika kujenga uwezo wa Taifa katika sekta hiyo, akitaja utekelezaji wa Mradi wa Bandari ya Uvuvi ya Kilwa Masoko ambao umekamilika, meli moja ya uvuvi wa bahari kuu, huku mchakato wa ununuzi wa meli nyingine nne ukiendelea, mchakato wa ujenzi wa viwanda vya uchakataji wa mazao ya uvuvi, hatua inayolenga kuongeza thamani ya mazao ya uvuvi, kukuza fursa za ajira na biashara pamoja na kuongeza mchango wa sekta hiyo katika uchumi wa Taifa.

Kongamano hilo lenye kauli mbiu “Hifadhi Bahari, Changamkia Fursa za Uchumi wa Buluu” ni sehemu ya shughuli zinazoambatana na Tamasha la Kizimkazi 2026, linalolenga kujadili fursa mbalimbali zinazotokana na Uchumi wa Buluu pamoja na namna ya kuzitumia kwa maendeleo endelevu.

TAFICO inalenga kutumia uwekezaji katika miundombinu, meli za uvuvi na viwanda vya uchakataji k**a msingi wa kuimarisha mnyororo wa thamani wa sekta ya uvuvi.

08/08/2026

"TAFICO NI MTOTO WETU"—KAMATI YA KUDUMU YA BUNGEKamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imesema...
07/08/2026

"TAFICO NI MTOTO WETU"—KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imesema ina wajibu wa kuhakikisha Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) linaendelea kuimarika na kufikia malengo yaliyokusudiwa na Serikali.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Deodatus Mwanyika (Mb), leo Agosti 07,2026, wakati wa ziara ya Kamati kwenye banda la TAFICO, katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Dkt. John Samuel Malecela, Nzuguni jijini Dodoma.

Kamati imetembelea TAFICO kwa lengo la kujionea maendeleo ya miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Shirika katika kuimarisha sekta ya uvuvi nchini. Akiwa katika banda la TAFICO, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, pamoja na wajumbe wa Kamati, walipokea maelezo kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati na hatua zilizofikiwa, yaliyowasilishwa na Afisa Uvuvi Mwandamizi wa TAFICO, Bw. Mgalula Lyobah.

Baada ya kupokea maelezo hayo, Mhe. Mwanyika alieleza kuridhishwa na hatua zinazopigwa na Shirika katika kutekeleza dhamira ya Serikali ya kuendeleza sekta ya uvuvi wa kisasa na kuongeza mchango wake katika uchumi wa Taifa.

"TAFICO ni mtoto wetu. Ni wajibu wetu kuhakikisha linaendelea kuimarika na kufikia malengo yaliyokusudiwa na Serikali. Tunafurahishwa na hatua zinazoendelea kuchukuliwa katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati, ambayo itaongeza tija, ajira na mchango wa sekta ya uvuvi katika maendeleo ya nchi," alisema Mhe. Mwanyika.

Kwa upande wake, Bw. Lyobah alieleza kuwa TAFICO inaendelea kutekeleza kwa ufanisi miradi ya kimkakati inayolenga kukuza uvuvi wa bahari kuu, ikiwemo ununuzi wa meli 4 ambazo ziko katika hatua ya ununuzi na kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu wezeshi .
Kukamilika kwa miundumbinu hii kuna kwenda sambamba na kukamilika kwa ujenzi wa bandari ya uvuvi iliyojengwa na Serikali Kilwa Masoko hizi ni jitahada za Serikali katika kuleta mapinduzi katika sekta ya uvuvi nchini.

Hatua hizi zinakwenda sambamba na malengo ya Serikali ya kuendeleza uchumi wa buluu na kuhakikisha rasilimali za uvuvi zinatumika kwa manufaa ya watanzania. Alisema Bw.Mgalula

TAFICO inaendelea kutumia jukwaa la Maonesho ya Nanenane kutoa elimu kwa wananchi.

Address

P. O. Box 2336
Dar Es Salaam

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 09:30 - 15:30
Friday 09:30 - 15:30

Telephone

+255733506430

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Taficotz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share