Bodi ya Chai Tanzania

Bodi ya Chai Tanzania Ukurasa wa Bodi ya Chai Tanzania

Wageni mbalimbali wameolendelea kutembelea banda la Bodi ya Chai Tanzania katika Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima ya Na...
04/08/2026

Wageni mbalimbali wameolendelea kutembelea banda la Bodi ya Chai Tanzania katika Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima ya Nane Nane yanayoendelea katika viwanja vya John Mallecela jijini Dodoma wanapatiwa elimu kuhusu mnyororo wa thamani wa sekta ya chai, pamoja na kujionea aina mbalimbali za chai bora zinazozalishwa nchini.

Karibu kwenye banda letu ujifunze zaidi kuhusu safari ya chai kutoka shambani hadi kikombeni, faida zake kiafya, na fursa zinazopatikana katika sekta ya chai kwa maendeleo ya uchumi wa taifa.

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Chai Tanzania, Bi. Beatrice Banzi, ametoa mafunzo kwa wananchi na wageni waliotembelea banda ...
04/08/2026

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Chai Tanzania, Bi. Beatrice Banzi, ametoa mafunzo kwa wananchi na wageni waliotembelea banda la Bodi ya Chai katika Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima ya Nane Nane akionesha hatua sahihi za kupika chai ili kupata ladha harufu na ubora halisi wa chai ya Tanzania.

Kupitia mafunzo hayo, Bi. Banzi aliwahimiza Watanzania kuzingatia njia bora za uandaaji wa chai ili kufurahia ubora wake huku akiwakaribisha wananchi kuendelea kutembelea banda la Bodi ya Chai kujifunza zaidi kuhusu mnyororo wa thamani wa sekta ya chai na bidhaa mbalimbali zinazozalishwa nchini.

MAKAMU WA RAIS APONGEZA MAONESHO YA NANE NANE 2026 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Dkt. E...
03/08/2026

MAKAMU WA RAIS APONGEZA MAONESHO YA NANE NANE 2026

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, ametembelea Maonesho ya Kitaifa na Kimataifa ya Nane Nane tarehe3 Agosti 2026 na kupongeza kazi nzuri za waoneshaji za teknolojia mbalimbali zinazoakisi kwa vitendo kaulimbiu yake katika safari ya utekelezaji wa DIRA 2050.

Maonesho ya Nanenane 2026 yanafanyika katika Viwanja vya Dkt. John Samuel Malecela, jijini Dodoma chini ya kaulimbiu "Tambua Soko; Ongeza Tija Kutekeleza DIRA 2050".

Mheshimiwa Makamu wa Rais ametembelea na kupokea maelekezo kutoka kwa wataalamu kuhusu shughuli mbalimbali za uzalishaji na ubunifu wa sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi pamoja na mikakati inayotekelezwa katika kufikia malengo ya DIRA 2050.

Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Makamu wa Rais ametembelea banda la mdhamini mkuu wa maonesho hayo, Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), pamoja na mabanda mbalimbali ya maonesho yaliyohusisha vipando vya zao la ulezi kutoka Halmashauri ya Mpwapwa, mbegu bora za mifugo ya mbuzi, kondoo na ng'ombe, vifaranga vya samaki, pamoja na shamba darasa la mbegu za malisho ya mifugo.

Aidha, ametembelea eneo la maadhimisho ya miaka 10 ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), pamoja na kushiriki shughuli za Siku ya Ushirika, ambazo zimekuwa sehemu ya matukio muhimu yanayoambatana na Maonesho ya Nane Nane mwaka huu.

Ziara hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, akiwemo Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo (Mb); Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule; Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego; Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Ng'wasi Damas Kamani; Mkurugenzi Mkuu wa TARI, Dkt. Thomas Bwana; Mrajisi wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dkt. Benson Ndiege, pamoja na wadau mbalimbali muhimu katika mnyororo wa thamani wa Sekta za Kilimo, mifugo na uvuvi.

Wizara Ya Manugu kilimo

DKT. SOPHIA KIZIGO AFURAHISHWA NA ELIMU YA SEKTA YA CHAI KATIKA BANDA LA BODI YA CHAI Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Dkt. Sop...
03/08/2026

DKT. SOPHIA KIZIGO AFURAHISHWA NA ELIMU YA SEKTA YA CHAI KATIKA BANDA LA BODI YA CHAI

Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Dkt. Sophia Mfaume Kizigo ametembelea banda la Bodi ya Chai Tanzania katika Maonesho ya Kimataifa ya Wakulima ya Nanenane yanayoendelea jijini Dodoma ambapo ameeleza kufurahishwa na elimu aliyopata kuhusu zao la chai kuanzia uzalishaji, uchakataji, uongezaji thamani hadi fursa mbalimbali zilizopo katika sekta hiyo. Aidha alipata fursa ya kuonja aina mbalimbali za chai zinazozalishwa nchini na kusifu ubora wake.

Dkt. Kizigo ameipongeza Bodi ya Chai Tanzania kwa kutumia Maonesho ya Nanenane kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mnyororo wa thamani wa sekta ya chai akieleza kuwa elimu hiyo inaongeza uelewa wa jamii na kuwahamasisha Watanzania kuthamini na kutumia chai inayozalishwa nchini.

Anytime is Tea Time... especially at Nane Nane!
03/08/2026

Anytime is Tea Time... especially at Nane Nane!

GODWIN GONDWE AIPONGEZA CHAI YA TANZANIA MAONESHO YA NANENANEMkuu wa Wilaya ya Singida Godwin Gondwe ametembelea banda l...
03/08/2026

GODWIN GONDWE AIPONGEZA CHAI YA TANZANIA MAONESHO YA NANENANE

Mkuu wa Wilaya ya Singida Godwin Gondwe ametembelea banda la Bodi ya Chai Tanzania katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Nanenane yanayoendelea jijini Dodoma ambapo ameonesha kuvutiwa na ubora wa chai ya Tanzania, hususan ladha harufu na ubora wake.

Akiwa katika bandani humo Gondwe alipata fursa ya kuonja aina mbalimbali za chai zinazozalishwa nchini na kueleza kuwa chai ya Tanzania ina viwango vinavyoweza kushindana katika soko la kimataifa. Pia aliwahamasisha wananchi kutambua thamani ya chai ya Tanzania kwa kuitumia na kuendelea kuiunga mkono.

Hata hivyo Bodi ya Chai Tanzania imeeleza kuwa ushiriki wake katika Maonesho ya Nanenane unalenga kuhamasisha matumizi ya chai ya Tanzania kutangaza ubora wake pamoja na kufungua fursa za masoko na uwekezaji katika sekta ya chai.

MAONESHO YA NANE NANE YAENDELEA KUFUNGUA FURSA ZA MASOKO KWA CHAI YA TANZANIAKaimu Mtendaji Mkuu wa Mtibwa Sugar Estates...
02/08/2026

MAONESHO YA NANE NANE YAENDELEA KUFUNGUA FURSA ZA MASOKO KWA CHAI YA TANZANIA

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mtibwa Sugar Estates Ltd, Bw. SS. Rao, ametembelea banda la Bodi ya Chai Tanzania katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea jijini Dodoma na kueleza kuvutiwa na ubora wa Specialty Tea inayozalishwa wilayani Kilolo, mkoani Iringa.

Baada ya kuonja chai hiyo, Bw. Rao amesema ina ladha na ubora wa kipekee unaoweza kuvutia soko la ndani na la kimataifa. Kutokana na kuvutiwa kwake ameomba mawasiliano ya Bodi ya Chai Tanzania ili kuendelea na majadiliano kuhusu fursa za ushirikiano na biashara ya chai.

Ushiriki wa Bodi ya Chai Tanzania katika Maonesho ya Nane Nane unaendelea kuzaa matokeo chanya kwa kuunganisha wazalishaji, wanunuzi na wawekezaji, huku ukitangaza ubora wa chai ya Tanzania na kufungua fursa mpya za masoko, biashara na uwekezaji.

Anytime is tea time…☕pause, sip, and enjoy the little moments.Karibu nane nane banda la Bodi ya chai Tanzania
02/08/2026

Anytime is tea time…☕pause, sip, and enjoy the little moments.

Karibu nane nane banda la Bodi ya chai Tanzania

02/08/2026
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Schelkovo Agrohim Bw. Zakaria Eissa, yenye makao makuu nchini Misri na tawi nchini Tanzani...
01/08/2026

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Schelkovo Agrohim Bw. Zakaria Eissa, yenye makao makuu nchini Misri na tawi nchini Tanzania ametembelea Banda la Bodi ya Chai Tanzania katika Maonesho ya Nanenane na kueleza kuvutiwa na ubora wa chai ya Tanzania.

Baada ya kupata fursa ya kuonja na kujifunza kuhusu aina mbalimbali za chai zinazozalishwa nchini Bw. Eissa ameomba mawasiliano ya Bodi ya Chai Tanzania ili kuwezesha ushirikiano kati ya Bodi na makampuni ya biashara ya chai yaliyopo nchini Urusi na Misri kwa lengo la kupanua masoko ya chai ya Tanzania katika nchi hizo.

Ziara hiyo imekuja kufuatia juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kuimarisha diplomasia ya uchumi ikiwemo ziara ya Rais nchini Urusi iliyolenga kuitangaza Tanzania na kufungua fursa za biashara na uwekezaji.

Urusi ni miongoni mwa nchi zenye utamaduni mkubwa wa unywaji wa chai, jambo linaloifanya kuwa soko lenye fursa kubwa kwa chai ya Tanzania, hususan chai maalum (Specialty Tea) inayozalishwa nchini.

Address

P. O. Box 2663, Tetex Building Pamba Road
Dar Es Salaam
00000

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Bodi ya Chai Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Bodi ya Chai Tanzania:

Shortcuts

Share