Weights and Measures Agency Tanzania - WMA

Weights and Measures Agency  Tanzania - WMA Dhima ya Wakala wa Vipimo ni kuthibiti vipimo vyote vinavyotumika na vinavyokusudiwa kutumika katika Sekta ya Biashara, Mazingira, Afya na Usalama.

Wakala wa Vipimo ni Taasisi ya Serikali iliyoko chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara inayosimamia matumizi sahihi ya vipimo katika biashara, Afya, Usalama na Mazingira. Iliundwa Mwaka 2002 na Majukumu yake ni Kumlinda mlaji katika Sekta za Biashara, Afya, Usalama na Mazingira kupitia matumizi ya Vipimo sahihi. Kuilinda jamii kuepukana na madhara yatokanayo na matumizi mabaya ya vipimo katika Sek

ta za Biashara, Afya, Usalama na Mazingira. Kuthibiti ufungashaji wa Bidhaa (Net quantity & lebelling)

Kuwa kiungo kati ya Taifa letu na taasisi za kikanda na Kimataifa katika masuala ya Vipimo (Legal Metrology)

Kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu Masuala ya Vipimo kwa wadau. Kuhakikisha vifaa vyote vitumikavyo nchini k**a standards za vipimo vinaulinganisho sahihi na ule wa Kimataifa.

TANGAZO LA MUHIMU
16/07/2026

TANGAZO LA MUHIMU

16/07/2026

Tunapozungumzia majukumu ya Wakala wa Vipimo (WMA) katika kumlinda mlaji, hususan katika kipimo cha Mizani, je unayajua majukumu hayo kwa kina? Je, ni uhakiki wa mizani zilizoko sokoni na madukani pekee? Vipi kuhusu wafanyabiashara wanaoagiza mizani hizo kwa lengo la kuuza hapa nchini? Wao wanapaswa kufanya nini? Afisa Vipimo Mkuu, Bw. Mulokozi Zimbeiya anadadavua....

15/07/2026

Je, unajua namna Wakala wa Vipimo (WMA) inavyohakiki vipimo katika bidhaa zilizofungashwa? Msikilize hapa BI GRACE KULENGWA, Afisa Vipimo Mwandamizi akielezea....

15/07/2026

Maji ni UHAI ...Maji yanagusa maisha ya kila mmoja wetu moja kwa moja. Kwa kulitambua hilo, Wakala wa Vipimo (WMA) inaendelea kuwaelimisha wananchi namna inavyowajibika kumlinda mlaji katika sekta hiyo ikiwa ni moja ya majukumu yake ya msingi. Zoezi la utoaji elimu ni endelevu. Hapa, Meneja wa WMA Mkoa wa ki-vipimo Temeke, Bw. Hilolimus Mahundi anadadavua akiwa katika Maonesho ya SabaSaba 2026 ambako WMA ilitoa elimu na huduma kwa maelfu ya wananchi. Karibu nawe upate elimu hii.

Elimu ya Vipimo ikiendelea kutolewa kwa wadau katika Banda la Wakala wa Vipimo na kwa waagizaji wa Vipimo kwenye Banda l...
09/07/2026

Elimu ya Vipimo ikiendelea kutolewa kwa wadau katika Banda la Wakala wa Vipimo na kwa waagizaji wa Vipimo kwenye Banda la China

06/07/2026

MBIU YA VIPIMO leo inaangazia maoni ya baadhi ya wadau waliotembelewa na maafisa vipimo katika mabanda yao ya maonesho sabasaba na kupewa elimu ya matumizi sahihi ya vipimo.

Wakala wa Vipimo (WMA) inaendelea kutembelea wajasiriamali mbalimbali katika maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba...
04/07/2026

Wakala wa Vipimo (WMA) inaendelea kutembelea wajasiriamali mbalimbali katika maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) kwa lengo la kuwapa elimu ya matumizi sahihi ya vipimo na ufungashaji sahihi wa bidhaa zao ili ziweze kuongeza thamani na kushindana katika soko la Kimataifa.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Ndugu Aristides Robert Mbwasi akisikiliza maelezo kuhusu teknolojia ya k...
04/07/2026

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Ndugu Aristides Robert Mbwasi akisikiliza maelezo kuhusu teknolojia ya kisasa iliyofungwa kwenye mizani kwa lengo la kuzuia uchakachuaji wa Vipimo kwa kuchezea mizani alipotembelea Banda la WMA katika maonesho ya Kimataifa ya Biashara (sabasaba).

Karibu sabasaba tukuhudumie
02/07/2026

Karibu sabasaba tukuhudumie

Mhe. Judith Salvio Kapinga (Mb) Waziri wa Viwanda na  Biashara akikabidhiwa zawadi mara baada ya kutembelea Banda la Wak...
02/07/2026

Mhe. Judith Salvio Kapinga (Mb) Waziri wa Viwanda na Biashara akikabidhiwa zawadi mara baada ya kutembelea Banda la Wakala wa Vipimo katika maonesho ya sabasaba Jijini Dar es Salaam.

Address

Dar Es Salaam
313

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Weights and Measures Agency Tanzania - WMA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share