Tume ya Utumishi wa Mahakama

Tume ya Utumishi wa Mahakama Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Tume ya Utumishi wa Mahakama, Government Organization, 12, Haki House' Mtaa wa Lithuli, Dar es Salaam.

Tume ya Utumishi wa Mahakama imeanzishwa kwa mujibu wa ibara ya 112 (1) ya katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ikisomwa pamoja na sheria ya uendeshaji wa mahakama Na.4 ya mwaka 2011

Watumishi wa Tume ya Utumishi wa Mahakama wakiendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu majukumu, huduma na shughuli mbali...
03/07/2026

Watumishi wa Tume ya Utumishi wa Mahakama wakiendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu majukumu, huduma na shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na Tume katika banda lake kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026), yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Dkt. Juma Homera akizungumza na Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi wa Tume ya Utumishi wa Ma...
03/07/2026

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Dkt. Juma Homera akizungumza na Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi wa Tume ya Utumishi wa Mahakama alipotembelea banda la Tume kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa leo tarehe 03 Julai, 2026 jijini Dar es salaam.

Picha mbalimbali zikionesha wananchi na wadau mbalimbali wakitembelea banda la Tume ya Utumishi wa Mahakama katika Maone...
03/07/2026

Picha mbalimbali zikionesha wananchi na wadau mbalimbali wakitembelea banda la Tume ya Utumishi wa Mahakama katika Maonesho ya Kimataifa ya Kibiashara ya Dar es salaam ( Sabasaba) 2026 yanayofanyika katika Viwanja vya Viwanja vya Mwl. J. K Nyerere Jijini Dar es salaam. Kupitia maonesho hayo, Tume inaendelea kutoa elimu kuhusu majukumu yake, huduma zinazotolewa na mchango wake katika kuimarisha usimamizi wa rasilimali watu katika Mahakama ya Tanzania.

03/07/2026
Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. George Masaju amemuapisha Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Dkt. J...
03/07/2026

Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. George Masaju amemuapisha Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Dkt. John Antony Jingu kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama katika Hafla iliyofanyika tarehe 26 Juni, 2026 jijini Dodoma.

Mtendaji Mkuu wa Mahakama na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Prof. Elisante Ole Gabriel, amefunga mafunzo ya Kama...
08/06/2026

Mtendaji Mkuu wa Mahakama na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Prof. Elisante Ole Gabriel, amefunga mafunzo ya Kamati za Nidhamu za Watumishi wasio Maafisa Mahakama yaliyofanyika tarehe 05 Juni 2026 katika Ukumbi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Jijini Mwanza. Mafunzo hayo yanalenga kuimarisha uwezo wa Kamati za Nidhamu katika kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma, pamoja na kuendelea kuimarisha nidhamu, uwajibikaji na weledi ndani ya Mahakama ya Tanzania.

Naibu Katibu (Nidhamu na Maadili), Bi. Alesia Mbuya, akitoa mafunzo kwa Wajumbe wa Kamati za Nidhamu za Watumishi wasio ...
08/06/2026

Naibu Katibu (Nidhamu na Maadili), Bi. Alesia Mbuya, akitoa mafunzo kwa Wajumbe wa Kamati za Nidhamu za Watumishi wasio Maafisa Mahakama yaliyofanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Jijini Mwanza.

Mafunzo hayo yalilenga kuimarisha uwezo wa Kamati za Nidhamu katika kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.
Aidha, mafunzo hayo yalikusudia kuendelea kuimarisha nidhamu, uwajibikaji na weledi miongoni mwa watumishi wa Mahakama ya Tanzania ili kuhakikisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi na usimamizi madhubuti wa masuala ya nidhamu katika utumishi wa Mahakama.

Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Mahakama wakiwa kwenye picha ya pamoja katika Hafla ya kumuaga aliyekuwa Mjumbe wa Tume J...
15/05/2026

Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Mahakama wakiwa kwenye picha ya pamoja katika Hafla ya kumuaga aliyekuwa Mjumbe wa Tume Jaji wa Mahakama ya Rufani Mhe. Dkt Gerald Ndika wa tatu (kushoto) baada ya kumaliza kipindi cha pili cha kuwa Mjumbe wa Tume.
katikati ni Jaji Mkuu wa Tanzania na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Mhe. George Masaju, Wapili (kushoto) ni Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mjumbe wa Tume Mhe. Gerson Mdemu, wa tatu (kulia) ni Jaji Kiongozi na Mjumbe wa Tume Mhe. Dkt. Mustapher Siyani, wapili (kulia) ni Mjumbe wa Tume Wakili Bahame Tom Nyanduga, wa kwanza (kushoto) ni Mjumbe wa Tume Wakili Dosca Mutabuzi na (Kulia) ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama na Katibu wa Tume Prof. Elisante Ole Gabriel.

MTENDAJI MKUU WA MAHAKAMA  NA KATIBU WA TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA PROF. ElISANTE OLE GABRIEL ALIPOFUNGUA KIKAO CHA BA...
11/04/2026

MTENDAJI MKUU WA MAHAKAMA NA KATIBU WA TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA PROF. ElISANTE OLE GABRIEL ALIPOFUNGUA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYA KAZI KILICHOFANYIKA TAREHE 10 APRILI, 2026 KATIKA UKUMBI WA TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA JIJINI DODOMA.

JAJI MKUU AWAAPISHA WAJUMBE WA TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMANa Lydia Churi- Tume ya Utumishi wa MahakamaJaji Mkuu wa Maha...
13/03/2026

JAJI MKUU AWAAPISHA WAJUMBE WA TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMANa

Lydia Churi- Tume ya Utumishi wa Mahakama

Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania na Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Mhe. George Masaju leo tarehe 13 Machi, 2026 amewaapisha wajumbe wanne wa Tume ya Utumishi wa Mahakama.

Katika hafla iliyofanyika leo kwenye ofisi za Tume ya Utumishi wa Mahakama jijini Dodoma, Jaji Mkuu amemuapisha Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania Mhe. Gerson Mdemu kuwa Mjumbe wa Tume kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.

Aidha, Jaji Mkuu pia amemuapisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza Johari kuwa Mjumbe wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kufuatia kuteuliwa kwa mara ya pili na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali baada ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika Oktoba 29, 2025.

Jaji Mkuu pia amewaapisha kwa mara ya pili Mawakili Bahame Tom Nyanduga na Dosca Kemilembe Mutabuzi kuwa Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Mahakama baada ya kumaliza kipindi chao cha miaka mitatu cha kuwa Wajumbe wa Tume na kuteuliwa tena na Rais kushika nafasi hiyo kwa mujibu wa Ibara ya 112 (1) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tume ya Utumishi wa Mahakama inaundwa na wajumbe wafuatao; Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania ambaye ni Mwenyekiti, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani anayeteuliwa na Rais, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Wajumbe wawili wanaoteuliwa na Rais.

Tume ya Utumishi wa Mahakama ni chombo kilichoundwa kwa mujibu wa Ibara ya 112 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ikisomwa pamoja na Sheria ya Usimamizi wa Mahakama Sura ya 237. Chombo hiki kimeundwa kwa lengo la kusimamia utendaji kazi wa Mahakama ya Tanzania ikiwa ni pamoja na kusimamia Ajira na Nidhamu za Watumishi wa Mahakama.

Address

12, Haki House' Mtaa Wa Lithuli
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tume ya Utumishi wa Mahakama posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share