24/07/2020
Watumishi wengi tunaamini kwamba kutembea sehemu nyingi Duniani, Kujulikana na watu wengi Duniani, Kuwa na Suti nyingi za gharama za kuvaa, Kuwa na Magari mengi ya Kifahari, Kuwa na Waumini wengi ndani ya Jengo la Kanisa NDIYO TIKETI YA KUKUBALIWA NA MUNGU!! Lahashaa!
Hivyo vyote si kigezo cha kukubaliwa na Mungu. Maana hata Shetani hivyo vitu huwa anavyo na pia ana uwezo mkubwa wa kukusanya watu wengi zaidi.
Bali tunapaswa kukaza mwendo katika utumishi wetu, kujinyenyekeza mbele za Mungu! Kuwa na huo Utakatifu ambao hakuna mtu atakayemwona Mungu asipokuwa nao. Kukiishi kiΔΊe tunachokihubiri na kuhakikisha tunakuwa na Mwisho mzuri wenye Ushuhuda, badala ya mwanzo mzuri.
Tuepuke kuwa na maneno ya kujikinai! Tuache kujimilikisha Kanisa na kulifanya MALI YETU. Kanisa siyo mali yetu. Kanisa siyo mali ya Wanadamu. Bali Kanisa ni mali ya Mungu mwenyewe na alilinunua kwa damu yake mwenyewe, tazamaππππ
"Matendo 20:28
28. Jitunzeni nafsi zenu, na lile kundi lote nalo, ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi ndani yake, mpate kulilisha kanisa lake Mungu, alilolinunua kwa damu yake mwenyewe."
ππHivi sisi tunayojimilikisha Kanisa na kulifanya Mali yetu, tunaposoma haya maandiko hayatupi hofu?? Je mimi na wewe tumeshamwaga damu kwa ajili ya Kanisa? Maana Mwenyewe alimwaga damu kwa ajili ya Kanisa lake. Halafu sisi tunajimilisha!!
Hivyo tuepuke sana na tuchunge sana midomo yetu watumishi. Hizi kauli tunazotamka kwambaπ "Hili ni Kanisa langu" "Hapa ni Kanisani kwangu" "Njoo Kanisani kwangu" "Mimi naponya kanisani kwangu". Haya ni maneno mabaya sana na hayampi Mungu utukufu, bali yeye anakuondolea ile nguvu yake ya kiutendaji na unabaki kuwa mfu kiroho na kiutendaji.
Mungu awabariki sana.
N imimi mtumwa katika Kristo Yesu
Mmissionary Shadrack Mwasonya.
Kwa mahitaji ya maombi Karibu sana
0786074455/ 0767074455
0713074455/ 0622074455