Ucsaf-Tanzania

Ucsaf-Tanzania UCSAF ilianzishwa na Serikali kwa lengo la kufanikisha huduma ya mawasiliano katika maeneo yasio na mvuto kwa watoa huduma ya mawasiliano nchini.

13/07/2026

Wananchi wa maeneo ya vijijini wameeleza namna maboresho ya huduma za mawasiliano yalivyosaidia kurahisisha maisha yao, hususan katika kupata huduma za afya na kuwasiliana na ndugu pamoja na jamaa zao.

Mmoja wa wananchi hao, Lucy Kusimula, mkazi wa Kijiji cha Ikowa wilayani Chamwino mkoani Dodoma, amesema hapo awali walikabiliwa na changamoto kubwa za mawasiliano, hali iliyowalazimu kutegemea simu za majirani walipokuwa wakikumbwa na dharura.

Amesema wanawake wajawazito walilazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya, lakini kwa sasa upatikanaji wa huduma za mawasiliano umewezesha mawasiliano ya haraka na kurahisisha hata kupokea fedha kutoka kwa ndugu wakati wa mahitaji ya dharura.

Kwa upande wake, Rose Charles ameishukuru Serikali pamoja na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kuendelea kusogeza huduma za mawasiliano karibu na wananchi kupitia ujenzi wa minara ya mawasiliano.

Amesema hatua hiyo imeimarisha upatikanaji wa huduma muhimu, ikiwemo kuwasiliana na vituo vya afya na kuitisha huduma za dharura kwa akina mama wajawazito, jambo ambalo limeongeza usalama na ustawi wa jamii.
Reposted from TBC DIGITAL

Wananchi wameendelea kutembelea banda la Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Bia...
10/07/2026

Wananchi wameendelea kutembelea banda la Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), wakipata elimu kuhusu miradi ya mawasiliano inayotekelezwa na Serikali kupitia UCSAF na mchango wake katika kusogeza huduma za mawasiliano karibu na wananchi.

Karibu banda la UCSAF ujifunze, upate taarifa sahihi kutoka kwa wataalamu wetu, uulize maswali na ufahamu zaidi kuhusu jinsi Serikali inavyoendelea kuimarisha mawasiliano kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.




MRADI WA MINARA 758 WAIPA TANZANIA TUZO YA KIMATAIFA YA WSIS PRIZES 2026Geneva, Uswisi – Julai 10, 2026Tanzania imeandik...
10/07/2026

MRADI WA MINARA 758 WAIPA TANZANIA TUZO YA KIMATAIFA YA WSIS PRIZES 2026

Geneva, Uswisi – Julai 10, 2026

Tanzania imeandika historia baada ya kutunukiwa Tuzo ya Kimataifa ya WSIS Prizes 2026 kupitia mradi wa ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano, uliopanua upatikanaji wa huduma za mawasiliano katika maeneo ya vijijini yaliyokuwa hayana huduma nchini.

Tuzo hiyo imepokelewa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki (Mb.), katika hafla iliyofanyika Geneva, Uswisi, tarehe 10 Julai 2026. Utambuzi huo unaonesha mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha miundombinu ya mawasiliano na kuharakisha ujumuishaji wa kidijitali nchini.

Mradi wa Minara 758 ulitekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwa kushirikiana na kampuni za mawasiliano za YAS, Vodacom, Airtel, TTCL na Halotel. Mradi huo umefikisha huduma za mawasiliano katika vijiji 1,400 na kuwawezesha wananchi zaidi ya milioni 8.5 kupata huduma za mawasiliano. Hatua hiyo imeongeza fursa za biashara, elimu, afya, huduma za kifedha na huduma nyingine za kijamii kupitia teknolojia za kidijitali.

Mbali na ushindi huo, Tanzania iliteuliwa katika vipengele saba (7) vya Tuzo za WSIS Prizes 2026, na kufanikiwa kutwaa tuzo mbili, sambamba na kupokea vyeti vya utambuzi kwa miradi mingine iliyofanya vizuri katika sekta ya TEHAMA.

Mradi wa Minara 758 ulizinduliwa rasmi na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 10 Aprili 2026 jijini Dodoma. Leo, mradi huo unatambuliwa kimataifa k**a mfano wa mafanikio katika kupunguza pengo la kidijitali, kuimarisha ushirikishwaji wa wananchi katika uchumi wa kidijitali na kuharakisha utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu kupitia teknolojia ya mawasiliano.




Mbunge wa Afrika Mashariki, Mhe. Fatma Kange, ametembelea banda la Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) katika Maonesho...
07/07/2026

Mbunge wa Afrika Mashariki, Mhe. Fatma Kange, ametembelea banda la Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), ambapo alipokea maelezo kuhusu utekelezaji wa miradi ya mawasiliano inayosimamiwa na UCSAF nchini.

Akiwa katika banda hilo, Mhe. Kange alipata fursa ya kujionea mafanikio ya miradi ya mawasiliano inayolenga kuboresha upatikanaji wa huduma za simu na intaneti, hususan katika maeneo ya vijijini na yasiyo na mvuto wa kibiashara. Pia alifahamishwa kuhusu mchango wa UCSAF katika kuimarisha ujumuishaji wa kidijitali na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi kupitia huduma za mawasiliano.

Ziara hiyo ni sehemu ya matembezi ya viongozi, wadau na wananchi mbalimbali wanaotembelea banda la UCSAF katika Maonesho ya Sabasaba, kujionea utekelezaji wa miradi na mafanikio ya Mfuko katika kuhakikisha huduma za mawasiliano zinawafikia Watanzania wengi zaidi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi ( SACP) Jumanne Muliro, ametembe...
06/07/2026

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi ( SACP) Jumanne Muliro, ametembelea banda la Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), ambapo alipokea maelezo kuhusu utekelezaji wa miradi ya mawasiliano inayosimamiwa na UCSAF nchini.

Akiwa katika banda hilo, Kamanda Muliro alifahamishwa kuhusu juhudi za UCSAF katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano, hususan katika maeneo ya vijijini na yasiyo na mvuto wa kibiashara. Pia alijionea mafanikio ya miradi inayotekelezwa na UCSAF katika kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanapata huduma za simu na intaneti, hatua inayochangia kuimarika kwa ulinzi na usalama pamoja na maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Ziara hiyo imekuwa sehemu ya shughuli zinazoendelea katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), ambapo UCSAF inaendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu miradi yake na mchango wake katika kuhakikisha huduma za mawasiliano zinawafikia Watanzania wengi zaidi.

Tunawakaribisha wananchi wote kutembelea banda la UCSAF na kujionea utekelezaji wa miradi ya mawasiliano pamoja na mafan...
03/07/2026

Tunawakaribisha wananchi wote kutembelea banda la UCSAF na kujionea utekelezaji wa miradi ya mawasiliano pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano nchini.

Pia, mtapata fursa ya kufahamu kwa undani kuhusu shughuli za UCSAF, kuzungumza na wataalamu wetu na kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu miradi ya mawasiliano.

Karibu banda la UCSAF, ndani ya Jengo la Karume.

📌Salamu za pongezi
03/07/2026

📌Salamu za pongezi

Karibu Banda la UCSAF katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba).Je, unafahamu jinsi Ser...
01/07/2026

Karibu Banda la UCSAF katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba).

Je, unafahamu jinsi Serikali inavyoendelea kupeleka huduma za mawasiliano katika maeneo ya vijijini na maeneo ambayo hayakuwa na mvuto wa kibiashara kwa watoa huduma?

Tembelea banda la UCSAF upate elimu kuhusu miradi ya mawasiliano inayotekelezwa nchini, ikiwemo mafanikio ya ujenzi wa minara ya mawasiliano, upanuzi wa huduma za simu na intaneti, pamoja na mipango inayoendelea kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wanapata huduma za mawasiliano zenye ubora.

Utapata fursa ya kuzungumza na wataalamu wetu, kupata majibu ya maswali yako na kujionea namna miradi ya UCSAF inavyochangia maendeleo ya wananchi na uchumi wa Taifa.

Karibu Sabasaba, tunapatilkana ndani ya jengo la Karume.

Msimu mwingine wa Sabasaba umefika! UCSAF inakukaribisha kutembelea banda lake katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kima...
29/06/2026

Msimu mwingine wa Sabasaba umefika!

UCSAF inakukaribisha kutembelea banda lake katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, ili upate elimu kuhusu utekelezaji wa miradi ya mawasiliano inayosimamiwa na Serikali kupitia UCSAF na namna tunavyoendelea kuboresha upatikanaji wa huduma za mawasiliano nchini.

Karibu ujifunze, uulize maswali na ujionee mafanikio ya miradi ya mawasiliano.

Karibu banda la UCSAF.

27/06/2026

Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), kwa kushirikiana na watoa huduma za mawasiliano, imekamilisha ujenzi wa minara 758 katika maeneo ya vijijini na pembezoni, mradi ambao umenufaisha wananchi takribani milioni 8.5 kwa kuwawezesha kupata huduma bora za mawasiliano na kushiriki kikamilifu katika shughuli za kijamii na kiuchumi.

Wananchi katika maeneo mbalimbali yaliyonufaika na ujenzi wa minara hiyo wanaendelea kuelezea manufaa wanayoyapata, wakisema huduma za mawasiliano zimeimarika kwa kiasi kikubwa na kurahisisha mawasiliano, biashara, elimu pamoja na upatikanaji wa huduma nyingine muhimu.

Baadhi yao wameeleza kuwa kabla ya ujenzi wa minara hiyo walilazimika kutembea umbali mrefu kutafuta maeneo yenye mtandao ili kupiga simu au kupata huduma za intaneti. Hata hivyo, kwa sasa huduma hizo zinapatikana karibu na makazi yao, jambo lililoboresha maisha yao na kuongeza ufanisi katika shughuli za kila siku.

Address

Jengo La UCSAF, S. L. P 1957, 10 Barabara Ya UCSAF, Makulu
Dodoma
41107

Opening Hours

Monday 08:00 - 16:00
Tuesday 08:00 - 16:00
Wednesday 08:00 - 16:00
Thursday 08:00 - 16:00
Friday 08:00 - 16:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ucsaf-Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Ucsaf-Tanzania:

Shortcuts

Share