Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika - coasco

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika - coasco Karibu kwenye ukurasa rasmi wa Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO)

WIZARA YA KILIMO, COASCO ZAJADILI MIKAKATI YA KUIMARISHA HUDUMA ZA UKAGUZI NA USIMAMIZI WA VYAMA VYA USHIRIKA Kurugenzi ...
13/08/2026

WIZARA YA KILIMO, COASCO ZAJADILI MIKAKATI YA KUIMARISHA HUDUMA ZA UKAGUZI NA USIMAMIZI WA VYAMA VYA USHIRIKA

Kurugenzi ya Masoko na Usalama wa Chakula ya Wizara ya Kilimo imefanya kikao kazi na Menejimenti ya Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) kwa lengo la kupitia utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Daniel G. Chongolo Waziri wa Kilimo na kujadili mipango, changamoto zilizopo, pamoja na kuweka mikakati ya kuimarisha utoaji wa huduma za Shirika.

Kikao hicho kimefanyika Agosti 8, 2026 katika ukumbi wa mikutano wa Makao makuu ya Shirika jijini Dodoma, kikiongozwa na Mkurugenzi wa Masoko na Usalama, Happy Kitingati, akiwa pamoja na viongozi wengine kutoka Wizara ya Kilimo.

Kikao hicho ni sehemu ya ushirikiano kati ya Wizara ya Kilimo kupitia Kurugenzi ya Masoko na Usalama wa Chakula na COASCO katika kuimarisha ukaguzi, usimamizi, uwajibikaji na ufanisi wa sekta ya ushirika nchini.

13/08/2026

COASCO inaimarisha uwajibikaji na utawala bora katika Vyama vya ushirika

“Ukaguzi wa Uhakika, Ushirika Imara”

Tunawatakia Heri ya Siku ya Nanenane 2026Kauli Mbiu: “Tambua Soko: Ongeza Tija Kutekeleza Dira 2050”
08/08/2026

Tunawatakia Heri ya Siku ya Nanenane 2026

Kauli Mbiu: “Tambua Soko: Ongeza Tija Kutekeleza Dira 2050”

08/08/2026

COASCO tupo Nanenane, karibu tukuhudumie

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) linaendelea kutoa elimu na huduma za ushauri kwa wadau mb...
07/08/2026

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) linaendelea kutoa elimu na huduma za ushauri kwa wadau mbalimbali wanaotembelea banda lake katika maonesho ya Kilimo ya Kimataifa Nanenane 2026 yanayoendelea kwenye Viwanja vya John Malecela (Nzuguni), jijini Dodoma.

Kupitia maonesho hayo, COASCO inatoa elimu kuhusu majukumu yake na nafasi ya Shirika katika kuimarisha uwajibikaji na utawala bora katika vyama vya ushirika.

COASCO inakukaribisha kutembelea banda lake lililopo ndani ya banda la Wizara ya Kilimo na Kijiji cha Ushirika ili upate elimu na ushauri wa huduma mbalimbali zinazotolewa na Shirika.

Makamishna wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), leo Agosti 5, 2026, wametembelea banda la Shirika la Ukaguz...
05/08/2026

Makamishna wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), leo Agosti 5, 2026, wametembelea banda la Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) lililopo katika kijiji cha ushirika kwenye maonesho ya Nanenane yanayoendelea kwenye viwanja vya John Malecela (Nzuguni), jijini Dodoma na kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo.

Wadau mbalimbali wakipata huduma kwenye banda la Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) katika m...
05/08/2026

Wadau mbalimbali wakipata huduma kwenye banda la Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) katika maonesho ya Nanenane 2026 yanayoendelea katika Viwanja vya John Malecela (Nzuguni), jijini Dodoma.

Karibu utembelee banda la Shirika lililopo ndani ya banda la Wizara ya Kilimo na Kijiji cha Ushirika ili upate elimu kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Shirika.

Karibu tukuhudumie

Viongozi na watumishi wa Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) wakiwa katika picha ya pamoja nd...
04/08/2026

Viongozi na watumishi wa Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya banda la shirika kwenye Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa Nanenane 2026 yanayoendelea Viwanja vya Nzuguni, Dodoma.

Ushiriki wa COASCO katika maonesho hayo unalenga kuendelea kuwafikia wadau kwa kutoa elimu kuhusu huduma za ukaguzi, usimamizi, mafunzo na ushauri ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha uwajibikaji, uwazi na utawala bora katika vyama vya ushirika na taasisi nyingine nchini.

𝗖𝗢𝗔𝗦𝗖𝗢 𝘆𝗮𝗼𝗻𝗴𝗲𝘇𝗮 𝘂𝘄𝗮𝗷𝗶𝗯𝗶𝗸𝗮𝗷𝗶 𝘄𝗮 𝗩𝘆𝗮𝗺𝗮 𝘃𝘆𝗮 𝘂𝘀𝗵𝗶𝗿𝗶𝗸𝗮 𝗞𝘂𝗽𝗶𝘁𝗶𝗮 𝘂𝗸𝗮𝗴𝘂𝘇𝗶 𝗻𝗮 𝗺𝗮𝗳𝘂𝗻𝘇𝗼Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya...
04/08/2026

𝗖𝗢𝗔𝗦𝗖𝗢 𝘆𝗮𝗼𝗻𝗴𝗲𝘇𝗮 𝘂𝘄𝗮𝗷𝗶𝗯𝗶𝗸𝗮𝗷𝗶 𝘄𝗮 𝗩𝘆𝗮𝗺𝗮 𝘃𝘆𝗮 𝘂𝘀𝗵𝗶𝗿𝗶𝗸𝗮 𝗞𝘂𝗽𝗶𝘁𝗶𝗮 𝘂𝗸𝗮𝗴𝘂𝘇𝗶 𝗻𝗮 𝗺𝗮𝗳𝘂𝗻𝘇𝗼

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika Tanzania (COASCO) limesema linaendelea kuimarisha uwajibikaji na utawala bora katika vyama vya ushirika kupitia ukaguzi wa hesabu, mafunzo na huduma za ushauri zinazolenga kulinda rasilimali za wanachama na kuongeza ufanisi wa vyama hivyo

Akizungumza katika Maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika Viwanja vya John Malecela jijini Dodoma, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COASCO, CPA Jeremiah Mugeta, amesema shirika hilo lina jukumu la kukagua vyama vya ushirika na Taasisi nyingine, kutoa ushauri na huduma za usimamizi

Pia amewaalika wananchi kutembelea banda la COASCO ndani ya banda la Wizara ya Kilimo na Kijiji cha ushirika kujifunza kuhusu huduma zinazotolewa.

Naye, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa COASCO, Prisilla Mushi, amesema mafunzo kwa viongozi na watendaji wa vyama vya ushirika yamechangia kuboresha matokeo ya ukaguzi. Amesema katika mwaka wa fedha 2025/2026, vyama vilivyopata hati safi za ukaguzi vimeongezeka kutoka asilimia 16 hadi 20, huku hati zenye dosari kubwa zikishuka kutoka asilimia 17 hadi 13.

COASCO TUPO NANENANE 2026, KARIBU TUKUHUDUMIEWadau mbalimbali wameendelea kutembelea banda la Shirika la Ukaguzi na Usim...
02/08/2026

COASCO TUPO NANENANE 2026, KARIBU TUKUHUDUMIE

Wadau mbalimbali wameendelea kutembelea banda la Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) katika Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa Nanenane yanayofanyika Viwanja vya Nzuguni, Dodoma, na kupata elimu kuhusu majukumu na huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika.

COASCO inapatikana katika Banda la Wizara ya Kilimo na Kijiji cha Ushirika, ambapo inatoa elimu na ushauri wa kitaalamu kuhusu ukaguzi, uhasibu, fedha, kodi, uwekezaji, utawala, usimamizi wa vihatarishi, pamoja na uandaaji wa sera, kanuni, miongozo na taratibu za kiutendaji.

Maonesho hayo yanafanyika kuanzia tarehe 1 hadi 8 Agosti 2026 kwa kaulimbiu isemayo, “Tambua Soko; Ongeza Tija Kutekeleza Dira 2050.” Karibu COASCO, tukuhudumie

Address

2 Barabara Ya Hatibu,3 Madukani, S. L. P 761, Dodoma4110
Dodoma
4110

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika - coasco posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share