15/05/2026
WANAUSHIRIKA KILIMANJARO WAPATIWA ELIMU YA USHIRIKA KUHUSU USIMAMIZI NA UENDESHAJI WA VYAMA
Wanaushirika wakiwemo Wanachama wa SACCOS na AMCOS Mkoani Kilimanjaro wamepatiwa Elimu kuhusu masuala mbalimbali yanahohusu Ushirika.
Hayo yamefanyika leo Mei 15, 2026 katika siku ya pili ya kuhitimisha Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika mkoani humo.
Wawezeshaji waliotoa Elimu ni pamoja na Mkuregenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Miriam Mmbaga ameelezea kuhusu Mwongozo wa Ajira na utendaji, haki, wajibu na majukumu ya mwajiri na mwajiriwa.
Liliani Lyimo, Afisa Sheria kutoka TCDC ametoa Elimu kuhusu mabadiliko ya Sheria ya vyama vya Ushirika na toleo Rekebu la Mwaka 2025, haki na majukumu ya mwanachama na mamlaka ya Mrajis wa vyama vya Ushirika.
Naye Daudi Ramadhani, Afisa Tehama kutoka TCDC ameelezea kuhusu Mfumo wa Vyama vya Ushirika (MUVU). Namna ya kujiunga, vipengele vinavyofanyiwa marekebisho na namna unavyofanya kazi.
Pia walikuwepo wawezeshaji wengine ambao kutoka Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB), Bima ya Afya (NHIF), Chama Kikuu cha Ushirika cha Akiba na mikopo Tanzani (SCCULT), Shirikisho la vyama vya Ushirika Tanzania (TFC), Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Waadhiri kutoka chuo cha Ushirika moshi (MoCU), Kampuni ya Bima (BUMACO), na Benki ya Ushirika Tanzania (COOP BANK).