Wizara ya Madini

Wizara ya Madini Sekta ya Madini kwa Uchumi Imara na Maendeleo Endelevu

repost from HABARILEO DAR ES SALAAM; MTOTO Mtanzania Xyleen Mapunda (15) amesema amefurahi kujifunza namna madini ya ura...
16/08/2026

repost from HABARILEO DAR ES SALAAM; MTOTO Mtanzania Xyleen Mapunda (15) amesema amefurahi kujifunza namna madini ya urani yanavyotumika kutengeneza nishati ya nyuklia na faida zake.
-
Xyleen alisema hayo alipowasili kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam leo Agosti 16, 2026 akitoka nchini Urusi.
-
Alikwenda huko kwa safari ya kielimu na kisayansi baada ya kushinda shindano la kimataifa la Icebreaker of Knowledge 2026 kupitia programu ya kampuni ya Nishati ya Nyuklia ya Urusi, Rosatom.
-
Xyleen ameweka historia kwa kuwa Mtanzania wa kwanza kufika Ncha ya Kaskazini (North Pole) katika safari ya siku 10 akiwa na wanafunzi wenzake wenye vipaji kutoka nchi 22 duniani.
-
Katika safari hiyo kutoka mji wa Murmansk kwenda Ncha ya Kaskazini, Franz Josef Land na kurejea Murmansk, wanafunzi hao walitumia meli kubwa zaidi duniani inayotumia nishati ya nyuklia 50 Let Pobedy.
-
“Meli yenyewe inatumia nyuklia, tumejifunza namna madini ya urani yanavyotumika kutengeneza nishati ya nyuklia na namna inavyotumika kwenye masuala mbalimbali… nimejifunza jambo zuri sana ambalo sikuwahi kufikiria,” alisema Xyleen.
-
Isome zaidi kupitia kiunganishi cha http://epaper.tsn.go.tz
Imeandaliwa na Zena Chande

16/08/2026

MWONEKANO WA MRADI WA UCHIMBAJI WA MADINI YA KINYWE MBWADE–DUTHUMI MOROGORO

Huu ndiyo mwonekano wa Mradi wa Uchimbaji Madini ya Kinywe ( Graphite) unaotekelezwa Mbwade–Duthumi, Kata ya Bwakwila Chini, Wilaya ya Morogoro, baada ya Serikali na Kampuni ya
Henan Yudi Mining kusaini Mikataba ya Ubia ya Uchimbaji na Uchakataji wa Madini hayo.

Mradi una mashapo yaliyothibitishwa ya tani milioni 104.28 za madini, yenye takribani tani milioni 61.2 za Kaboni (Total Graphitic Carbon).

Uwekezaji wa mradi unakadiriwa kufikia Dola za Marekani milioni 100, ( Bilioni 265) huku takribani Dola milioni 111.3 tayari zikiwa zimewekezwa katika awamu ya kwanza.

Mradi unatarajiwa kuzalisha tani 50,000 za madini ya kinywe kwa mwaka na kutoa ajira kwa Watanzania wapatao 600 kupitia ajira za moja kwa moja na nyingine zisizo za moja kwa Moja.

Huu ni miongozi mwa mikataba 14 wa Msingi ambayo tayari imesainiwa na Serikali na Kampuni mbalimbali za uchimbaji madini katika miradi ya uchimbaji na uchakataji madini ya kinywe, niobium na helium tangu mwezi Mei hadi Agosti 2026, huku mikataba mingine ikiwa mbioni kusainiwa.





 Be Seen,Connect and Shape the Future.TMIC 2026 will feature a major Mining Exhibition, offering an opportunity to showc...
16/08/2026



Be Seen,Connect and Shape the Future.

TMIC 2026 will feature a major Mining Exhibition, offering an opportunity to showcase your company, products, value-added solutions and technologies across the mining value chain from small-scale mining to global mining innovation.

Be part of shaping the future of mining, sustainable development and industrial growth.

For registration and more information: conference.madini.go.tz
+255 714 278 620

IndustrialGrowth MiningInnovation

15/08/2026

Hafla ya Utiaji Saini Mikataba ya Uchimbaji Madini ya Kinywe Wilayani Morogoro.

"Kipekee kabisa nimshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuendelea kuvutia uwekezaji mkubwa Sekta ya Madini. Leo Morogoro inaandika historia nyingine ya Kusaini Mkataba wa Msingi kati ya Serikali na Mwekezaji ambapo Serikali itakuwa na Hisa za asilimia 17 katika mradi huu nje ya kodi, tozo na ushuru mbalimbali ambao kampuni hii itatozwa," Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde.




SEKTA YA MADINI YAVUTIA UWEKEZAJI WA TRILIONI 9 NDANI YA MIAKA MINNE▪️Mikataba ya Msingi 14 ya Madini Yasainiwa▪️Serikal...
15/08/2026

SEKTA YA MADINI YAVUTIA UWEKEZAJI WA TRILIONI 9 NDANI YA MIAKA MINNE

▪️Mikataba ya Msingi 14 ya Madini Yasainiwa

▪️Serikali yasaini Mkataba wa Bilioni 265 na Kampuni ya Henan Yudi Mining ya Mradi wa Graphite Morogoro

▪️Tanzania yawa kivutio kikubwa cha uwekezaji sekta ya Madini Afrika

▪️Rais Samia apongezwa kwa mazingira wezeshi ya uwekezaji

📍MOROGORO:

Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, amesema ndani ya kipindi cha Miaka Minne, (4) Sekta ya Madini imevutia uwekezaji wa Shilingi trilioni 9, hatua inayoiweka Tanzania kuwa kivutio cha uwekezaji wa Madini Barani Afrika.

Amesema hayo leoAgosti 15, 2026, Mkoani Morogoro wakati wa hafla ya utiaji saini wa Mikataba ya Ubia wa Uchimbaji wa Madini ya Kinywe baina ya Serikali na Kampuni ya Henan Yudi Mining na kuongeza kuwa, hadi sasa tayari jumla ya mikataba ya Msingi 14 imekwisha sainiwa.

Amesema kuwa mradi huo una mashapo yaliyothibitishwa ya takribani tani milioni 104.28 za kinywe, na unatarajiwa kuwekeza takribani Dola milioni 100 (Shilingi bilioni 265) huku uzalishaji wa kiwango kamili ukilenga kufikia tani 50,000 za kinywe kwa mwaka na kwamba mradi unatakuwa na uwezo wa kuchakata tani milioni moja kwa mwaka wakati huohuo zaidi ya Watanzania 600 wakitarajiwa kupata ajira za moja kwa moja.

Mavunde amesema Serikali inaendelea kuimarisha nafasi yake katika sekta ya madini kutoka kuwa mwenyeji wa uchimbaji hadi kuwa mshiriki wa thamani inayozalishwa, ambapo katika mradi huo Serikali inamiliki asilimia 17 ya hisa.

Amesema kinywe ni madini muhimu katika teknolojia za kisasa, ikiwemo utengenezaji wa anode za betri, hivyo mradi huo una nafasi ya kuchangia katika azma ya Tanzania kushiriki zaidi kwenye mnyororo wa thamani wa kinywe duniani.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, M***a Kilakala, amesema Serikali ya Wilaya inashukuru juhudi zilizofanyika kufanikisha makubaliano hayo, akieleza kuwa mradi unatarajiwa kufungua fursa za kiuchumi na ajira, kuongeza uzalishaji wa madini na kuchochea maendeleo ya sekta ya madini na uchumi wa Taifa.

Aidha, Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian, amezipongeza pande zote zilizoshiriki katika majadiliano hayo inaendelea....

“Sisi k**a Chama matumaini yetu ni kuona makubaliano haya yanenda kusimamiwa na pande zote mbili kwa ukamilifu kwa manuf...
15/08/2026

“Sisi k**a Chama matumaini yetu ni kuona makubaliano haya yanenda kusimamiwa na pande zote mbili kwa ukamilifu kwa manufaa ya taifa na hatutegemei k**a kutakuwa na ukiukwaji wa makubaliano, tutasimamia kila hatua kuhakikisha kila lengo linafikiwa katika mradi huu”

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro, Michael Bundala, akizungumza katika Hafla ya Utiaji Saini wa Mikataba ya Ubia wa Uchimbaji wa Madini ya Kinywe baina ya Serikali na Kampuni ya Henan Yudi Mining.

“Wananchi hawa wamesubiri sana kuanza kwa mradi huu wa madini ya kinywe, sasa baada ya makubaliano haya wananchi hawa wa...
15/08/2026

“Wananchi hawa wamesubiri sana kuanza kwa mradi huu wa madini ya kinywe, sasa baada ya makubaliano haya wananchi hawa wanategemea kuona manufaa ya uwepo wa madini haya hapa, wananchi wa hapa wanataka wapewe kipaumbele kwenye suala la ajira katika mradi huu”

Mbunge wa jimbo la Morogoro Mhe. Zuberi Mfaume, akizungumza katika Hafla ya Utiaji Saini wa Mikataba ya Ubia wa Uchimbaji wa Madini ya Kinywe baina ya Serikali na Kampuni ya Henan Yudi Mining.*

“Serikali ya Wilaya inashukuru kwa juhudi zilizofanyika kuhakikisha makubaliano haya yanafikiwa na hatimaye Mikataba hii...
15/08/2026

“Serikali ya Wilaya inashukuru kwa juhudi zilizofanyika kuhakikisha makubaliano haya yanafikiwa na hatimaye Mikataba hii inasainiwa leo hii, na kuashiria kuanza kwa utekelezaji wa mradi ukitarajiwa kufungua fursa za kiuchumi, ajira, kuongeza uzalishaji wa madini pamoja na kuchochea maendeleo ya Sekta ya Madini na uchumi wa Taifa.”

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, M***a Kilakala akizungumza katika Hafla ya Utiaji Saini wa Mikataba ya Ubia wa Uchimbaji wa Madini ya Kinywe baina ya Serikali na Kampuni ya Henan Yudi Mining.

“Leo tunazindua safari ya zaidi ya miaka 20 ya uchimbaji wa madini ya kinywe katika wilaya hii ya Morogoro, kwetu sisi k...
15/08/2026

“Leo tunazindua safari ya zaidi ya miaka 20 ya uchimbaji wa madini ya kinywe katika wilaya hii ya Morogoro, kwetu sisi kwa Ofisi ya Msajili wa Hazina, mradi huu ni kielelezo cha umiliki wa wananchi katika rasilimali zao zilizopo hapa nchini, mradi huu ni dhamana ya kizazi cha sasa na cha baadaye, Ofisi ya Msajili wa Hazina itaendelea kufanya kazi kwa niaba ya watanzania kwa manufuaa ya kichumi kwa taifa na wananchi kwa ujumla wake”

Mkurugenzi wa Mipango,Tafiti na Maendeleo, Ofisi ya Msajili wa Hazina, Dk. Emanuel Luvanda akizungumza katika Hafla ya Utiaji Saini wa Mikataba ya Ubia wa Uchimbaji wa Madini ya Kinywe baina ya Serikali na Kampuni ya Yudi Mining (T) Graphite Development Company Limited.

“Mradi huu unatarajiwa kutengeneza ajira 600 kwa Watanzania, kuwezesha uhamishaji wa teknolojia na ujuzi, tutafunga mfum...
15/08/2026

“Mradi huu unatarajiwa kutengeneza ajira 600 kwa Watanzania, kuwezesha uhamishaji wa teknolojia na ujuzi, tutafunga mfumo wa kisasa ambayo bado haijatumika ukanda huu, pamoja na kuiunganisha Tanzania na mnyororo wa thamani wa graphite duniani. Tunaamini uwekezaji huu utakuwa chachu ya kuongeza thamani ya rasilimali za Tanzania na kuchochea fursa zaidi za kiuchumi kwa Watanzania.”

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Yudi Mining Liu Zhenghao, akizungumza katika Hafla ya Utiaji Saini wa Mikataba ya Ubia wa Uchimbaji wa Madini ya Kinywe baina ya Serikali na Kampuni ya Yudi Mining (T) Graphite Development Company Limited.




Address

Dodoma
255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Wizara ya Madini posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share