Tax Ombudsman Services Tanzania

Tax Ombudsman Services Tanzania Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Tax Ombudsman Services Tanzania, Government Organization, P. O BOX 1441, Dodoma.

04/08/2026
ZanzibarJulai 28, 2026TOST imeendesha kampeni ya utoaji wa elimu kwa umma kwa makundi mbalimbali ya wafanyabiashara na w...
28/07/2026

Zanzibar
Julai 28, 2026

TOST imeendesha kampeni ya utoaji wa elimu kwa umma kwa makundi mbalimbali ya wafanyabiashara na washauri wa kodi kuhusu kazi, majukumu na mamlaka yake katika mnyororo mzima wa utekelezaji wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi.

Kampeni hiyo imewakutanisha zaidi ya wawakilishi 20 kutoka vyama, jumuiya na taasisi za wafanyabiashara pamoja na washauri wa kodi kutoka maeneo mbalimbali ya Zanzibar.

Lengo la kampeni hiyo ni kuongeza uelewa wa wadau kuhusu nafasi ya TOST katika Kodi zote zinazosimamiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania.

Singida | Julai 17, 2026Viongozi na Maafisa wa Ofisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (TOST) wakutana kusu...
17/07/2026

Singida | Julai 17, 2026

Viongozi na Maafisa wa Ofisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (TOST) wakutana kusuka mikakati ya kuboresha huduma zake kwa umma kwa kuandaa Mpango wa Ufuatiliaji na Tathmini wa mwaka wa fedha 2026/2027.

Kikao kazi hicho kimewaleta pamoja watumishi na viongozi kutoka vitengo na sehemu mbalimbali kupitia na kuboresha mipango ya utekelezaji wa bajeti kwa lengo la kuimarisha usuluhishi wa malalamiko na taarifa za kodi, kuongeza ufanisi wa utoaji wa elimu ya kodi kwa umma, na kuendelea kujenga imani ya walipakodi pamoja na kuhamasisha ulipaji wa kodi kwa hiari.

Matukio katika picha ni Wanafunzi waliotembelea banda la Ofisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (TOST) kat...
06/07/2026

Matukio katika picha ni Wanafunzi waliotembelea banda la Ofisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (TOST) katika Maonesho ya Sabasaba walipata elimu kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na taasisi hiyo.

Baada ya kupata elimu hiyo, wanafunzi walikabidhiwa zawadi maalum kutoka TOST k**a ishara ya kuthamini ziara yao.

Ofisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (TOST) imeendelea kutekeleza jukumu lake la kutoa elimu kwa umma ku...
04/07/2026

Ofisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (TOST) imeendelea kutekeleza jukumu lake la kutoa elimu kwa umma kuhusu kazi, majukumu na huduma zinazotolewa na ofisi hiyo kwa wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wanaotembelea banda la TOST lililopo ndani ya jengo la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba).

TOST inawakaribisha wananchi na wafanyabiashara wote kutembelea banda lake ili kupata elimu kuhusu masuala ya kodi, huduma za usuluhishi wa malalamiko ya kodi, pamoja na ushauri unaohusu haki na wajibu wao katika masuala ya kodi. Lengo ni kuongeza uelewa wa wananchi, kuimarisha ushirikiano kati ya walipakodi na mamlaka husika, na kuchangia katika ujenzi wa uchumi imara wa Taifa na ustawi wa wananchi.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde, ameipongeza Ofisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi ...
03/07/2026

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde, ameipongeza Ofisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (TOST) kwa kazi nzuri inayoifanya, na kuitaka iendelee kuhakikisha malalamiko na taarifa za kodi zinazowasilishwa na wananchi zinashughulikiwa kwa wakati ili kuongeza ufanisi katika usimamizi wa kodi na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Amesema usuluhishi wa haraka, wa haki na wenye uwazi utaongeza imani ya walipakodi, kuhamasisha ulipaji wa kodi kwa hiari, na kuchangia kufikiwa kwa lengo la Taifa la kuwa na uchumi wenye thamani ya dola trilioni moja ifikapo mwaka 2050.

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa Usajili wa Malalamiko Bi. Witness Mollel amesema TOST imeendelea kutumia Maonesho ya Sabasaba k**a jukwaa la kuwafikia wananchi na wafanyabiashara kwa kutoa elimu kuhusu haki na wajibu wa mlipakodi, kupokea malalamiko na taarifa za kodi, pamoja na kuzifanyia kazi kwa mujibu wa sheria.

Hatua hiyo inalenga kuongeza uelewa wa masuala ya kodi, kuimarisha ulipaji wa kodi kwa hiari, kujenga imani kati ya walipakodi na mamlaka husika, na kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia mazingira rafiki ya biashara.

02/07/2026

Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis M***a Omar (Mb) ametoa rai kwa Wananchi na Wafanyabiashara kutembelea Banda la Ofisi ya Usuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi (TOST) katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanayoendelea katika Viwanja vya Mwl. J.K. Nyerere, ili kupata elimu kuhusu huduma zinazotolewa na ofisi hiyo.

Rai hiyo imetolewa leo tarehe 2 Julai, alipotembelea Banda la TOST lililopo ndani ya Jengo la Wizara ya Fedha na kuhimiza Wananchi na Wafanyabiashara kutembelea banda hilo ili waweze kupata elimu kuhusu majukumu ya TOST, pamoja kupewa suluhisho ya malalamiko na taarifa zao za kodi.

Balozi Omar amesema kuwa huduma zinatolewa na TOST zinachangia kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato, kuboresha mazingira ya biashara na kuunga mkono utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Kwa upande wake, Msuluhishi wa Malalamiko na Taarifa za Kodi, Bw. Erastus Mtui, amesema TOST imeweka kambi katika maonesho hayo ili kutoa elimu kwa wananchi na wafanyabiashara sambamba na kupokea
malalamiko na taarifa za kodi kutoka kwa wananchi pamoja na kuzifanyia kazi kwa wakati kwa mujibu wa sheria ili kuongeza wigo wa ukusanywaji wa Kodi pamoja na ulipaji kodi wa hiari.

Waziri wa Fedha Mhe. Balozi Khamis M***a Omar (Mb) ametoa rai kwa Wananchi na Wafanyabiashara kutembelea Banda la Ofisi ...

Address

P. O BOX 1441
Dodoma

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tax Ombudsman Services Tanzania posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share