Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu

Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Karibu Katika ukurasa rasmi ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu.

*KIONGOZI WA BUDDHA ASIFU UHURU WA KUABUDU TANZANIA*Na: Mwandishi wetu - Dar es Salaam, Juni 7, 2026Kiongozi Mkuu wa din...
07/06/2026

*KIONGOZI WA BUDDHA ASIFU UHURU WA KUABUDU TANZANIA*

Na: Mwandishi wetu - Dar es Salaam, Juni 7, 2026

Kiongozi Mkuu wa dini ya Buddha nchini, Mchungaji Dkt. Ilukuptiye Pannasekara, amesifu ushirikiano ambao wanaupata sio tu kutoka katika dini zingine bali pia serikalini kwa ujumla.

Ametoa kauli hiyo wakati wa kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa kiongozi wa dhehebu la Buddha duniani na uzinduzi wa sanamu ya dhahabu ya Buddha (Golden Buddha Statue) eneo la Upanga jijini Dar es Salaam Juni 7, 2026, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu, akimwakilisha Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.

Alisema, amekuwa akipata ushirikiano mkubwa kutoka dini nyingine hapa nchini na hivyo kuwafanya waumuni wa Buddha kujisikia furaha.

“Kutokana na mazingira hayo mazuri, tuna jumla ya miradi mitano kwenye sekta za elimu, utalii na afya, miradin hii tayari mingine imeanza na mingine iko katika hatua mbalimbali.” Alisema.

“Hatuhitaji usaidizi wa fedha kutoka serikalini, tunahitaji ushirikiano, miradi hii mitano ni ya uhakika, italeta zaidi ya dola za kimarekani milioni 100 kwenye uchumi wa Tanzania, alisema Mchungaji Dkt. Pannasekara.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu, amewahakikishia kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wake, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, itaendelea kutoa ushirikiano kwa dini zote bila kuwepo kwa ubaguzi.

Amesema Muelekeo wa serikali inapoanza utekelezaji wa dira ya Maendeleo ya 2050 imefungua milango ya kidiplomasia ili kuwaalika wawekezaji kuwekeza hapa nchini.

“Kama serikali tumewahakikishia kuwa kupitia Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji tumewahakikishia kwamba watakapokuwa tayari tutawepeleka kwenye maeneo ya kimkakati ili kutekeleza miradi yao katika sekta za Utalii, Afya na Elimu.” Alisema.

Mwisho.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu (mwenye suti), akimiminia maji sanamu ya B...
07/06/2026

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu (mwenye suti), akimiminia maji sanamu ya Buddha k**a ishara ya utakaso katika roho, fikra, maneno na matendo na kuombea neema wakati wa kuachimisha siku ya kuzaliwa ya dini hiyo, na uzinduzi wa Sanamu ya Golden Buddha Upanga jijini nDar es Salaam Juni 7, 2026.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu (kushoto), akipokea sanamu ya Buddha, kuto...
07/06/2026

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu (kushoto), akipokea sanamu ya Buddha, kutoka kwa Kiongozi Mkuu wa Buddha hapa nchini, Mchungaji Dkt. Pannasekara wakati wa sherehe za kuachimisha siku ya kuzaliwa ya dini hiyo, na uzinduzi wa Sanamu ya Golden Buddha Upanga jijini Dar es Salaam Juni 7, 2026.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu (mwenye suti), akiwa na Kiongozi Mkuu wa ...
07/06/2026

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu (mwenye suti), akiwa na Kiongozi Mkuu wa Buddha hapa nchini, Mchungaji Dkt. Ilukuptiye (kushoto) na Mchungani Xianhong, wakielekea eneo la sherehe za kuachimisha siku ya kuzaliwa ya dini hiyo, na uzinduzi wa Sanamu ya Golden Buddha Upanga jijini Dar es Salaam Juni 7, 2026.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu (mwenye suti), akiwa na Kiongozi Mkuu wa B...
07/06/2026

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu (mwenye suti), akiwa na Kiongozi Mkuu wa Buddha hapa nchini, Mchungaji Dkt. Ilukuptiye Pannasekara na viongozi wengine, wakati akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Sanamu ya Buddha kwenye temple la dini hiyo Upanga jijini Dar es Salaam, Juni 7, 2026.

FURSA 200 ZA AJIRA KWA MADEREVA TEKSI KATIKA NCHINI YA UMOJA WA FALME ZA KIARABU
06/06/2026

FURSA 200 ZA AJIRA KWA MADEREVA TEKSI KATIKA NCHINI YA UMOJA WA FALME ZA KIARABU

DKT. MUNISI AKUTANA NA KUFANYA KIKAO KAZI CHA KIMKAKATI NA WAKURUGENZI WA IDARA YA AJIRA NA UKUZAJI UJUZINa. OWM (KAM) D...
04/06/2026

DKT. MUNISI AKUTANA NA KUFANYA KIKAO KAZI CHA KIMKAKATI NA WAKURUGENZI WA IDARA YA AJIRA NA UKUZAJI UJUZI

Na. OWM (KAM) Dodoma

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Dkt. Evaline Munisi amekutana na kufanya kikao kazi na Wakurugenzi pamoja na wataalamu wa Idara ya Ajira na Ukuzaji Ujuzi kutoka Ofisi hiyo kwa lengo la kuimarisha utekelezaji wa majukumu, kuongeza ufanisi wa kazi na kuimarisha ushirikiano katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Katika kikao hicho kilichofanyika ofisini kwake Dodoma Juni 04,2026 , Dkt. Munisi ameitaka idara hiyo kuongeza juhudi katika kutangaza fursa mbalimbali za ajira na programu za ukuzaji ujuzi zinazotolewa na Serikali ili kuwafikia Watanzania wengi zaidi na kuwawezesha kunufaika na fursa hizo kwa wakati.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa ubunifu, uwajibikaji na ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu ya idara hiyo ili kuhakikisha huduma zinazotolewa zinakuwa na tija, zinawafikia walengwa ipasavyo na kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.

Dkt. Munisi ameelekeza idara hiyo kuweka mkazo katika uboreshaji wa takwimu za soko la ajira na kufanya tathmini ya mara kwa mara ya mahitaji ya ujuzi katika sekta mbalimbali. Alisema hatua hiyo itawezesha Serikali kuandaa programu zinazoendana na mahitaji halisi ya waajiri na soko la ajira kwa ujumla.

Kwa upande wao, Wakurugenzi wa Idara hizo Bi.Alana Nchimbi na Bi.Jane Sorogo wamemshukuru Naibu Waziri kwa maelekezo na mwongozo alioutoa ambapo wameahidi kuongeza kasi ya utekelezaji wa mipango ya idara, ikiwemo kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi, vyuo vya ufundi na taasisi za elimu ya juu ili kuhakikisha vijana wanapata ujuzi unaohitajika sokoni.

Kikao hicho ni sehemu ya jitihada endelevu za Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Ajira na Mahusiano kuhakikisha kuwa Sera ya Taifa ya Ajira ya mwaka 2008 inatekelezwa kwa vitendo, changamoto za ajira zinapungua na fursa za kiuchumi zinapanuliwa kwa vijana na makundi mengine katika jamii.

Mwisho.

04/06/2026
WAZIRI SANGU AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA MKUTANO WA 114 ILONa: OWM (KAM) – Geneva, UswisiWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri ...
04/06/2026

WAZIRI SANGU AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA MKUTANO WA 114 ILO

Na: OWM (KAM) – Geneva, Uswisi

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Sangu ameongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki katika Mkutano Mkuu wa 114 wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) unaofanyika Jijini Geneva, nchini Uswisi.

Akizungumza leo Juni 4, 2026 Mhe. Sangu amesema mkutano huo umekuwa na manufaa makubwa kwa Taifa katika kujadili masuala ya haki za wafanyakazi, kusimamia viwango vya kazi ili kuwa na stahiki kulingana na makubaliano ya pamoja chini ya Shirika la Kazi Duniani.

Waziri Sangu amebainisha maeneo makuu ya mjadala katika mkutano huo wa mwaka 2026 ni pamoja na: Masuala mbalimbali yanayohusu Sekta ya Kazi Duniani; Utekelezaji wa mikataba mbalimbali ambayo Tanzania imeridhia chini ya ILO; na Matumizi ya Akili Unde (AI) inavyoweza kutumika katika kuhakikisha kazi za staha zinazingatiwa kwa wafanyakazi.

Vile vile, amesema kuwa katika mkutano huo wameweza kujadili na Wadau wa Utatu (Serikali, Waajiri na Wafanyakazi) kutoka Tanzania Bara na Visiwani ili kuona namna bora ya kushirikiana na kuwa na majadiliano ya kijamii ambayo yanaleta tija hususan katika nyakati hizi za matumizi ya teknolojia na ukuaji wa uchumi wa kidijitali.

Kwa upande mwengine, Waziri Sangu amemshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu wadau wa utatu kushiriki katika mkutano huo ambao unawawezesha kubadilishana uzoefu na kujadili masuala yanayohusu ustawi wa sekta ya kazi.

Mkutano Mkuu wa 114 wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) unaofanyika Jijini Geneva, nchini Uswisi unashirikisha wawakilishi wa Serikali, Waajiri na Wafanyakazi kutoka nchi wanachama 187. Mkutano huo ulianza rasmi tarehe 1 Juni, 2026 na utahitimishwa Juni 12, 2026.

Address

Mji Wa Serikali, Mtumba
Dodoma

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu:

Share