Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Kusimamia na Kuratibu Uendeshaji wa chaguzi kwa mujibu wa Sheria.......

07/07/2026
Menejimenti ya INEC yajengewa uwezo wa utekelezaji wa mikataba kupitia Nest.INEC-Dar es SalaamMkurugenzi Mkuu wa Mamlaka...
27/06/2026

Menejimenti ya INEC yajengewa uwezo wa utekelezaji wa mikataba kupitia Nest.

INEC-Dar es Salaam

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA)Bw.Dennis Kwame Simba leo tarehe 27 Juni, 2026 amefungua mafunzo ya siku tano kwa Menejimenti ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kuhusu sheria ya ununuzi wa Umma na matumizi ya mfumo wa NeST yanayofanyiKa katika Ukumbi wa Bohari Jijini Dar es Salaam.

Bw.Simba katika hotuba yake ya ufunguzi amesema kuwa mfumo wa kidijitali wa ununuzi wa umma (NeST) umekuwa mkombozi mkubwa kwa kuongeza uwazi, uwajibikaji, na kudhibiti udanganyifu ikiwemo matumizi ya nyaraka za kughushi kwenye michakato ya zabuni nchini.

​Ameongeza kuwa mfumo huo umekuja kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya ununuzi kwa kuhakikisha Taasisi nunuzi na wazabuni wote wanawajibika kikamilifu kulingana na sheria na miongozo iliyopo.

​"Mfumo wa NeST umesaidia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa taarifa sahihi na za kuaminika kwa wakati, jambo ambalo limeondoa kabisa mianya ya matumizi ya nyaraka za kughushi zilizokuwa zikijitokeza huko nyuma," amesisitiza Bw.Simba.

​Mbali na kudhibiti udanganyifu na kuimarisha uwazi, Mkurugenzi Mkuu wa PPRA, Bw.Simba amebainisha faida nyingine za kiikolojia na kiuchumi za mfumo huo, akisema umepunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya karatasi katika ofisi za serikali, hatua inayoongeza utunzaji wa kumbukumbu.

​Bw.Simba amewahimiza washiriki kufuatilia mafunzo hayo kwa umakini mkubwa ili kupata uelewa wa kina utakaosaidia kurahisisha utekelezaji wa mikataba ya zabuni na kuleta tija katika taasisi hiyo muhimu.

Awali wakati akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa PPRA, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Kailima R.K alisema ​Mafunzo haya yanafanyika kwa lengo la kuwajengea uwezo Menejimenti na watumishi wa INEC kuendesha michakato ya ununuzi kwa ufanisi wa hali ya juu na kwa kuzingatia viwango vya kisasa vya kidijitali.

RISALA UCHAGUZI MDOGO ISMANI NA KATA 12!
31/05/2026

RISALA UCHAGUZI MDOGO ISMANI NA KATA 12!

Wapiga Kura 222,218 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura watashiriki kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge ...
31/05/2026

Wapiga Kura 222,218 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura watashiriki kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Isimani lililopo Halamashauri ya Wilaya ya Iringa Mkoani Iringa na Kata 12 za Tanzania Bara.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele ameyasema hayo leo Mei 31, 2026 Mkoani Iringa wakati akisoma risala maalum kuhusu uchaguzi katika jimbo na kata husika utakao fanyika kesho Juni 01, 2026 na kusema kuwa jumla ya vituo 628 vya Kupigia Kura vitatumika.

“wapiga kura 89,753 wapo kwenye Jimbo la Ismani na wapiga kura 132,465 wapo kwenye kata 12 zitakazofanya uchaguzi mdogo na vituo 277 vipo kwenye Jimbo la Ismani na vituo 351 vipo kwenye kata 12 zitakazofanya uchaguzi mdogo.,”amesema Jaji Mwambegele.

Aidha, amesema Katika Uchaguzi huo, jumla ya wagombea 108 kutoka katika vyama vya siasa 17 wanawania nafasi wazi ya ubunge na udiwani katika maeneo aliyoyataja.

“Jimbo la Ismani lina wagombea 17 wa nafasi ya Ubunge ambapo kati ya wagombea hao wagombea nane (08) sawa na asilimia 47.06 ni wanaume na wagombea tisa (09) sawa na asilimia 52.94 ni wanawake. Kata 12 zinazofanya uchaguzi mdogo wa udiwani zina jumla ya wagombea 91 ambapo kati ya hao wagombea 61 sawa na asilimia 67.03 ni wanaume na wagombea 30 sawa na asilimia 32.97 ni wanawake.” amesema Jaji Mwambegele.

Na kuongeza kwa kusema “Natumia fursa hii kuvikumbusha Vyama vya Siasa vinavyoshiriki uchaguzi kesho Juni 01, 2026 kuzingatia wajibu wao wa kuweka mawakala katika vituo vyote vya zoezi la kupiga, kuhesabu na kujumlishia kura. Wasimamizi wa uchaguzi katika Jimbo na Kata husika, wamekamilisha taratibu zinazoweka mazingira yanayowawezesha mawakala wa vyama vya siasa kufuatilia mchakato mzima wa uchaguzi".

Amesema, mawakala hao, wanawajibika katika kulinda maslahi ya vyama na wagombea wao. Hivyo, wanapaswa kuzingatia Sheria, Kanuni, taratibu za Uchaguzi na maelekezo ya Tume katika utekelezaji wa majukumu yao vituoni.

Jaji Mwambegele amesema vituo vitafunguliwa saa 01:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 jioni.

Msimamizi wa Uchaguzi, Jimbo la Kinondoni, Charles Lawisso akifungua Mafunzo ya Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Vi...
29/05/2026

Msimamizi wa Uchaguzi, Jimbo la Kinondoni, Charles Lawisso akifungua Mafunzo ya Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Vituo vya Kupigia Kura katika Uchaguzi Mdogo wa Udiwani Kata ya Mzimuni, Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, katika Ukumbi wa Mikutano wa Manispaa hiyo, jijini Dar es Salaam, leo Mei 29, 2026. Lawisso amewataka Washiriki hao kufanya kazi kwa weledi wakati wa uchaguzi.

Kata hiyo ni miongoni mwa kata 12 za Tanzania Bara zitakazofanya uchaguzi sambamba na uchaguzi mdogo wa ubunge kwenye Jimbo la Ismani Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Mkoa wa Iringa.

Kata nyingine ni Zongomera, Manispaa ya Kahama; Itilo, Halmashauri ya Mji wa Nzega; Ketare, Halmashauri ya Mji wa Tarime na Nyumbigwa, Halmashauri ya Mji wa Kasulu.

Nyingine ni kata ya Kala iliyoko Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi; Ziba, Halmashauri ya Wilaya Igunga; Kamsisi, Halmashauri ya Wilaya ya Mlele; Nyamugali, Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe; Namasakata Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, Kibiti; Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti na Kata ya Bwongera Halmashauri ya Wilaya ya Chato.

TAARIFA KWA UMMA!
18/05/2026

TAARIFA KWA UMMA!

Wagombea 17 wameteuliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kugombea ubunge kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Ismani lilil...
10/05/2026

Wagombea 17 wameteuliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kugombea ubunge kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Ismani lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Mkoani Iringa.

Uteuzi huo umefanywa kwa niaba ya Tume na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Ismani, Ndugu. Caroline Ang’wen Otieno leo tarehe 10 Mei, 2026.

Wagombea walioteuliwa na vyama vyao kwenye mabano ni Ndugu. Emmanuela Kaganda Mtatifikolo (CCM), Ndugu. Farida Issa Mwapungu (MAKINI), Ndugu. Asha Athumani Chuma (UPDP), Ndugu. Protas Shaibu Mgimbila (CCK), Ndugu. Fidelis Daud Mtikile (SAU), Ndugu. Hadija Husen Makawa (ADA-TADEA) Ndugu. Zavely Raurent Seleleka (UDP) na Ndugu. Subira Majuto Kalolo (NLD).

Wengine ni Ndugu. Bernard George Mwingira (DP), Ndugu. Burton Emilyo Chetenge (NCCR-Mageuzi), Ndugu. Mbalinga Christian Thomas (N.R.A), Ndugu. Mark Isdory Mhemela (AAFP), Ndugu. Nassim Yahaya Upete (CUF), Ndugu. Mwaka Lameck Mgimwa (TLP), Ndugu. Asma Abdallah Othman (UMD), Ndugu. Maimuna Martin Lumato (ADC) na Ndugu. Daudi Issa Masasi (CHAUMMA).

Akizungumza baada ya uteuzi huo, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo hilo, Ndugu. Caroline Ang’wen Otieno amesema kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Tume, kampeni kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Ismani pamoja na kata 12 za Tanzania Bara zitaanza kesho tarehe 11 hadi 31 Mei, 2026 na uchaguzi utafanyika siku ya Jumatatu tarehe 01 Juni, 2026.

“Baada ya hatua hii ya uteuzi, kinachofuata ni kubandika fomu za uteuzi eneo la wazi kwa ajili ya kuwapa fursa ya kuweka pingamizi wale wanaoruhusiwa kuweka pingamizi kwa mujibu wa sheria. Baada ya saa 24 kupita na endapo hakutakuwa na pingamizi wagombea hao 17 wataendelea na kampeni kuanzia kesho tarehe 11 hadi 31 Mei, 2026 na uchaguzi utafanyika tarehe 01 Juni, 2026,” amesema.

KIBALI KWA TAASISI NA ASASI KUTOA ELIMU NA UANGALIZI WA UCHAGUZI!
01/05/2026

KIBALI KWA TAASISI NA ASASI KUTOA ELIMU NA UANGALIZI WA UCHAGUZI!

Address

Dodoma
41107

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share