Tanzania Dairy Board

Tanzania Dairy Board Ukurasa rasmi wa Bodi ya Maziwa Tanzania

TANZANIA MWENYEJI WA MKUTANO WA 10 WA WATAALAM WA MIFUGO BARANI AFRIKA 2029Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa Mkutan...
13/08/2026

TANZANIA MWENYEJI WA MKUTANO WA 10 WA WATAALAM WA MIFUGO BARANI AFRIKA 2029

Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 10 wa Wataalam wa Mifugo Barani Afrika (10th All Africa Conference on Animal Agriculture – AACAA), unaotarajiwa kufanyika mwaka 2029 nchini Tanzania.

Uamuzi huo umefikiwa tarehe 12 Agosti 2026 na wanachama wa Jumuiya ya Wataalam wa Mifugo Barani Afrika (All Africa Society of Animal Production – AASAP) wanaoshiriki Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya hiyo unaofanyika mjini Abuja, Nigeria, kuanzia tarehe 9 hadi 13 Agosti 2026.

Wanachama wa AASAP wamekubaliana kuichagua Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo baada ya kuvutiwa na juhudi na maendeleo yanayofanywa nchini katika kuendeleza Sekta ya Mifugo, pamoja na fursa zilizopo katika maeneo ya utafiti, teknolojia na ubunifu wa mifumo ya uzalishaji wa mifugo.

Kabla ya uamuzi huo, Dkt. Titus Eliamoni Lyatuu, ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Wataalam wa Mifugo Tanzania (TSAP) na mwakilishi wa Tanzania katika mkutano huo, aliwasilisha utayari wa Tanzania katika kuandaa na kuendesha mkutano huo mkubwa wa kimataifa. Dkt. Lyatuu alieleza kuwa Tanzania ina fursa mbalimbali za tafiti na maendeleo katika Sekta ya Mifugo ambazo zinaweza kuwa sehemu muhimu ya mijadala ya wataalam kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika.

Aidha, Dkt. Lyatuu alieleza vivutio na fursa mbalimbali zinazopatikana nchini Tanzania, ikiwemo mashamba na mifumo mbalimbali ya ufugaji, vivutio vya utalii, utamaduni wa Watanzania, amani na usalama, pamoja na mazingira mazuri ya uongozi na usimamizi wa Sekta ya Mifugo kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Uchaguzi wa Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo unatarajiwa kutoa fursa kwa wataalam, watafiti, taasisi za elimu na utafiti, wafugaji, sekta binafsi na wadau mbalimbali wa Sekta ya Mifugo kutoka Afrika na nje ya Afrika kukutana, kubadilishana uzoefu, kujadili matokeo ya tafiti na kuweka mikakati ya kuendeleza Sekta ya Mifugo barani Afrika.

Katika maandalizi kuelekea mkutano huo, TSAP imejiandaa kushirikisha wadau mbalimbali wa Sekta ya Mifugo na Uvuvi, pamoja na taasisi nyingine zinazohusiana na maendeleo ya sekta hiyo, ili kushirikiana katika maandalizi na kuhakikisha mkuta

TDB YAANDIKA HISTORIA NANENANE 2026, YATWAA TUZO MARA TATU MFULULIZODODOMABodi ya Maziwa Tanzania (TDB) imeandika histor...
11/08/2026

TDB YAANDIKA HISTORIA NANENANE 2026, YATWAA TUZO MARA TATU MFULULIZO

DODOMA

Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) imeandika historia kwa kutwaa tuzo kwa mara ya tatu mfululizo katika kundi la Bodi za Mazao ya Kilimo na Mifugo wakati wa Maonesho ya Wakulima Nanenane 2026 yaliyofanyika katika Viwanja vya Dkt. John Samwel Malecela, Nzuguni jijini Dodoma.

Tuzo hiyo iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akihitimisha Maonesho ya Nanenane Agosti 08, 2026, ikiwa ni ishara ya kutambua ubora na ufanisi wa TDB katika kushiriki na kutoa huduma kwa wananchi na wadau wa Tasnia ya Maziwa.

Tuzo hiyo imekuja baada ya TDB kushiriki kikamilifu katika maonesho hayo kwa kutoa elimu na huduma mbalimbali kwa wananchi na wadau, ikiwemo elimu kuhusu uzalishaji wa maziwa salama na yenye ubora, usindikaji na uongezaji thamani, matumizi ya teknolojia, usajili wa shughuli za maziwa pamoja na fursa za uwekezaji na biashara katika mnyororo wa thamani wa Tasnia ya Maziwa.

Akizungumza baada ya kutangazwa kwa ushindi huo, Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania, Prof. George Msalya, amesema tuzo hiyo ni matokeo ya juhudi za pamoja za watumishi wa TDB katika kuhakikisha Taasisi inatoa huduma bora na yenye manufaa kwa wananchi.

Amesema mafanikio hayo yanaongeza wajibu kwa Bodi kuendelea kuboresha huduma, kuimarisha ushirikiano na wadau na kuhakikisha Tasnia ya Maziwa inakuwa na mchango mkubwa katika lishe, ajira, kipato na uchumi wa Taifa.

Ushindi huo wa mara ya tatu mfululizo umeifanya TDB kuendelea kujijengea nafasi ya kipekee katika Maonesho ya Nanenane, huku ukiwa ni ishara ya dhamira ya Bodi katika kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

TDB inaendelea kuhamasisha wadau kuzalisha kwa tija, kuongeza thamani ya maziwa na kutumia fursa za soko ili kuendeleza Tasnia ya Maziwa, sambamba na kaulimbiu ya Nanenane 2026 isemayo “Tambua Soko, Zalisha kwa Tija Kutekeleza Dira 2050.”

NANENANE 2026: TDB YATOA ELIMU, HUDUMA NA KUFUNGUA FURSA ZA TASNIA YA MAZIWADODOMABodi ya Maziwa Tanzania (TDB) imetumia...
11/08/2026

NANENANE 2026: TDB YATOA ELIMU, HUDUMA NA KUFUNGUA FURSA ZA TASNIA YA MAZIWA

DODOMA

Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) imetumia Maonesho ya Wakulima Nanenane 2026 kuwa jukwaa muhimu la kuwafikia wananchi na wadau wa Tasnia ya Maziwa kwa kutoa elimu, huduma na taarifa kuhusu fursa mbalimbali zinazopatikana katika mnyororo wa thamani wa maziwa, hatua inayolenga kuongeza tija, uwekezaji na matumizi ya maziwa salama na yenye ubora nchini.

Akizungumza wakati wa maonesho hayo yaliyofanyika katika Viwanja vya Dkt. John Samwel Malecela, Nzuguni, jijini Dodoma, Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania, Prof. George Msalya, amesema ushiriki wa TDB katika Nanenane ni sehemu ya utekelezaji wa jukumu la Bodi la kuwaelimisha wananchi na wadau kuhusu tasnia ya maziwa, pamoja na kuwaunganisha na fursa zilizopo katika Tasniahiyo.

Prof. Msalya amesema Tasnia ya Maziwa ina nafasi kubwa katika kuchangia uchumi wa Taifa kupitia uzalishaji, uongezaji thamani, ajira na biashara, huku akisisitiza umuhimu wa wadau kutumia fursa zilizopo katika mnyororo wa thamani wa maziwa kuanzia uzalishaji wa maziwa ghafi, ukusanyaji, usindikaji, ufungashaji, usafirishaji hadi masoko.

Amesema kupitia banda la TDB, wananchi na wadau wamepata elimu kuhusu uzalishaji wa maziwa salama na yenye ubora, usindikaji, matumizi ya teknolojia, usajili wa shughuli za maziwa, fursa za uwekezaji na biashara, pamoja na umuhimu wa matumizi ya maziwa katika kuboresha lishe na afya ya jamii.

“Nanenane ni fursa kubwa kwetu kuwafikia wananchi moja kwa moja. Tunatoa elimu kuhusu namna ya kuzalisha maziwa salama na yenye ubora, namna ya kuongeza thamani ya maziwa na pia tunawaeleza wadau kuhusu fursa zilizopo katika Tasnia hii,” amesema Prof. Msalya.

Aidha, Prof. Msalya amesema TDB imeendelea kuimarisha ushirikiano na wadau mbalimbali wa tasnia ya maziwa, wakiwemo wazalishaji, wasindikaji, wafanyabiashara, wawekezaji na taasisi za Serikali, kwa lengo la kujenga tasnia yenye tija, ushindani na uwezo wa kukidhi mahitaji ya soko.

Katika maonesho hayo, TDB pia imeendelea kutoa huduma za usajili na elimu kwa wadau, huku wataalamu wake wakitoa ufafanuzi kuhusu ubora na usalama wa maziwa, teknolojia za usindikaji, matumizi ya vimea k

09/08/2026





08/08/2026
📸 HABARI PICHAMaafisa wa Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) wakiwahudumia na kuwapatia elimu wadau pamoja na wananchi mbalimb...
08/08/2026

📸 HABARI PICHA

Maafisa wa Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) wakiwahudumia na kuwapatia elimu wadau pamoja na wananchi mbalimbali waliotembelea banda la TDB katika Maonesho ya Wakulima Nanenane 2026.

Wageni hao wamepata fursa ya kufahamu majukumu na huduma zinazotolewa na TDB, usalama na ubora wa maziwa, pamoja na fursa mbalimbali za uwekezaji na biashara katika tasnia ya maziwa.

TDB inaendelea kuwahudumia wananchi na wadau kwa kutoa elimu na taarifa muhimu kwa lengo la kuimarisha na kukuza tasnia ya maziwa nchini.




MaziwaSalama TambuaSokoZalishaKwaTija Dira2050

Afisa Masoko wa Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB), Bw. Said Isike, akitoa elimu kwa wadau wa Tasnia ya Maziwa kuhusu taratib...
08/08/2026

Afisa Masoko wa Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB), Bw. Said Isike, akitoa elimu kwa wadau wa Tasnia ya Maziwa kuhusu taratibu na umuhimu wa usajili wa shughuli za maziwa walipotembelea banda la TDB katika Maonesho ya Wakulima Nanenane 2026.

Katika maelezo yake, Bw. Isike amesisitiza umuhimu wa wadau kuzingatia taratibu za usajili ili kufanya shughuli zao kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazosimamia Tasnia ya Maziwa nchini. Elimu hiyo pia inalenga kuwasaidia wadau kufahamu huduma zinazotolewa na TDB na namna ya kuzifikia kwa urahisi.

TDB inaendelea kutoa elimu na huduma kwa wadau ili kuimarisha urasimishaji, ubora, usalama na maendeleo endelevu ya Tasnia ya Maziwa nchini.





MaziwaSalama TambuaSokoZalishaKwaTija Dira2050

Meneja wa Huduma za Masoko wa Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB), Bw. Joseph Semu, akitoa taswira ya fursa za uwekezaji katik...
08/08/2026

Meneja wa Huduma za Masoko wa Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB), Bw. Joseph Semu, akitoa taswira ya fursa za uwekezaji katika Tasnia ya Maziwa nchini kwa raia wa kigeni waliotembelea banda la TDB wakati wa Maonesho ya Wakulima Nanenane 2026.

Katika maelezo yake, Bw. Semu ameeleza fursa zilizopo katika mnyororo wa thamani wa maziwa, ikiwemo uzalishaji, ukusanyaji, uchakataji, uongezaji thamani, usambazaji na masoko, akisisitiza kuwa Tanzania ina fursa kubwa kwa wawekezaji katika kuendeleza tasnia ya maziwa na kuchangia ukuaji wa uchumi.

TDB inaendelea kuhamasisha uwekezaji katika tasnia ya maziwa kwa lengo la kuongeza tija, ajira, kipato na ushindani wa bidhaa za maziwa nchini.





MaziwaNiLishe TambuaSokoZalishaKwaTija Dira2050

TDB YAKABIDHI ATM YA MAZIWA KWA TAISH FARMBodi ya Maziwa Tanzania (TDB) imekabidhi ATM ya Maziwa kwa Taish Farm ya Singi...
07/08/2026

TDB YAKABIDHI ATM YA MAZIWA KWA TAISH FARM

Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) imekabidhi ATM ya Maziwa kwa Taish Farm ya Singida, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuongeza upatikanaji wa maziwa salama na yenye ubora, pamoja na kukuza matumizi ya maziwa na kuongeza thamani katika Tasnia ya Maziwa nchini.

Makabidhiano hayo yameshuhudiwa na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), yakionesha umuhimu wa ushirikiano wa wadau katika kuendeleza tasnia ya maziwa na kuboresha upatikanaji wa bidhaa bora kwa walaji.

TDB – Tukiimarisha Tasnia ya Maziwa kwa Maendeleo Endelevu.

07/08/2026



Address

Nyumba 300
Dodoma
P.O.BOX17029

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tanzania Dairy Board posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Tanzania Dairy Board:

Shortcuts

Share