08/09/2026
Watumishi Wapya Wizara ya Habari Wanolewa Misingi ya Utumishi wa Umma
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetoa mafunzo kwa Watumishi wapya walioajiriwa wizarani hapo kwa lengo la kuwajengea uelewa kuhusu misingi, taratibu, na maadili ya Utumishi wa Umma.
Akifungua mafunzo hayo leo Septemba 08, 2026 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Methusela Ntonda amewataka watumishi hao kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia weledi, uadilifu, nidhamu na uwajibikaji, akisisitiza umuhimu wa kuifahamu vyema Sheria, Kanuni na Taratibu zinazoongoza utumishi wa umma.
Amesema, mafunzo hayo ni sehemu muhimu ya kuwaandaa ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kutoa huduma bora kwa wananchi.