03/12/2025
MANISPAA YA GEITA YASAMBAZA MBEGU ZA VIAZI LISHE KATIKA SHULE 41 KUBORESHA LISHE YA WANAFUNZI
Halmashauri ya Manispaa ya Geita imeanza rasmi zoezi la usambazaji wa mbegu za viazi lishe katika shule 41 za msingi na sekondari ndani ya manispaa hiyo. Zoezi hili linafanyika kwa lengo la kuimarisha lishe ya wanafunzi kupitia kilimo cha bustani na mashamba yanayomilikiwa na shule husika.
Mbegu zinazotolewa ni za aina ya Kabode, Jewel, Irene na Kakamega, ambazo zinatambulika kwa kuwa na virutubisho muhimu k**a vile vitamini A, madini ya chuma na nyuzinyuzi, vinavyosaidia katika ukuaji wa mwili na kuimarisha kinga ya mwili.
Mpango huu unatekelezwa k**a sehemu ya afua za lishe na mpango wa chakula shuleni, kwa lengo la kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi anapata angalau mlo mmoja wenye virutubisho anapokuwa shuleni. Hili linaenda sambamba na azma ya serikali ya kuboresha mazingira ya ujifunzaji na kupunguza changamoto za kiafya zinazotokana na lishe duni kwa watoto wa shule.
Zoezi hili linafanikishwa kupitia ushirikiano wa karibu baina ya idara za Afya, Kilimo na Elimu (Msingi na Sekondari), jambo linaloonesha nguvu ya mshik**ano wa kiutendaji katika kuhakikisha wanafunzi wanapata huduma bora na endelevu ya chakula shuleni.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Halmashauri ya Manispaa ya Geita