24/10/2016
ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA.
(JICHO LA TOFAUTI)
Hivi kwa nini tunazani kwamba "ELIMU NI MUHIMU ZAIDI KULIKO VINGINE??"
Karibu tena mdau wa page yetu ili tuweze kujifunza na kupeana dondoo mbalimbali za kimaisha ili tuweze kujitambua.
Tuanze basi mada yetu kwa kujiuliza tu swali hili:-
Kwanini tunalazimika kuwa na elimu?
Au tunasoma ili iweje??
Majibu ya haraka haraka tunayoweza kupata katika msingi wa swali hili ni:-
Tunasoma ili tuwe na maisha mazuri.
Tunasoma ili tupate kazi na ujira mzuri.
Tunasoma ili kutengeneza maisha ya baadaye. n.k
Yote haya yanaweza kuwa majibu sahihi kulingana na mtazamo wa mtu binafsi.
Sasa basi, ebu tuingie kwa pamoja kiundani zaidi kutambua thamani ya elimu kwa binadamu.
Elimu ni k**a afya tu. Ni kitu muhimu tu k**a afya ili binadamu aweze kukua na kupanua mawazo yake kulingana na mazingira yanayomzunguka.
Tunahiitaji Elimu kwa sababu ya Kuitawala dunia. Pia ni Amri tunayopewa hata katika vitabu vya Kidini BIBLIA/ MSAHAFU. Enendeni duniani mkaitawale dunia.
Sasa unawezaje kuitawala Dunia wakati huijui dunia??
Ili uweze kuitawala dunia ni lazima kupambana na mazingira yanayokuzuia kufikia yale unayotamani kuyafikia kimaisha.
Na kazi ya elimu ni moja tu ambayo ni kuviondoa vikwazo hivyo.
Kwa mfano:-
Binadamu tumeumbwa na njaa, ili uweze kuitibu njaa yako ni lazima upate chakula kilichopikwa vizuri.
Je, Ungejuaje leo kwamba, eti ukichukua nyanya ukachanganya na kitunguu na kuweka chumvi kidogo, utapata ladha Fulani itakayokuwezesha kuiona thamani ya chakula chako k**a kusingekuwa na mtu aliyekufundisha au kukuelekeza??
Hiyo ni elimu.
Ungejuwaje leo kwamba kuiba ni dhambi endapo husingefundishwa hivyo??
Hiyo pia ni kazi ya elimu.
Kwa hiyo tunapozungumzia elimu atuzungumzii kitu kikubwa sana cha kutisha, Bali tunazungumza kuhusu TIBA ya asili ya akili ya mwanadamu.
Hvyo Tunaposema kwamba Elimu ni Ufunguo wa maisha tunamaanisha kwamba, ili uweze kufanya jambo lolote hapa duniani ni lazima uwe na uelewa juu ya jambo lenyewe. Na uelewa huo hauji hivi hivi tu bila kupata mtu wa kukufundisha na kukuelewesha, ndiyo tafsili ya elimu.
Sasa tena jiulize:-
Kuna watu wangapi wamesoma lakini maisha yao hadi sasa hayaeleweki??
Maana yake ni nini??
Hapa inamaanisha kwamba, wapo baadhi ya watu wanaidhani kwamba kusoma au kupata elimu ndio mafanikio yenyewe. La hasha!! Yaani unakuta mtu anachanganya elimu na mafanikio akizani kwamba ni kitu kimoja.
Elimu ni Uelewa wa Jambo fulani.
Bali mafanikio hutokana na faida ya kile ulichokielewa wakati unafundishwa. Lakini utayaona mafanikio endapo tu utatenda kwa umakini yale uliyoyaelewa baada ya kufundishwa (UJUZI).
Fikiria k**a umepata shahada ya udaktari alafu uk**aliza masomo yako ukakaa tu nyumbani bila kutumia taaluma uliyonayo katika kuwa hudumia wengine, lakini ukawa unajivunia mafanikio ya kupata shahada tu; unadhani shahada hiyo inaweza kukuletea mafanikio hapo ulipo?
Misingi ya Elimu ni hii-
Elewa, kisha hudumia wengine kwa lile ulichokielewa. Hapo ndipo utayaona mafanikio.
WITO
Wito wangu kwenu hasa kwa wazazi na walezi; URITHI pekee utakaoweza kumfanya mwanao aweze kumudu maisha ndani ya ulimwengu huu ni ELIMU. ni usimpe mtoto wako Mali kwani kwa kufanya hivyo ni kumuangamiza akiwa bado angali hai.
NB;
Endelea kutembelea ukurasa wetu wa Vission family tz, ili kujiifunza mambo mbali mbali ya kimaisha yatakayo kufanya uimarike kiakili.
Ni katika kuelekea kwenye kampeni yetu ya VISSION FAMILY FURSA.
NIWATAKIE SIKU NJEMA ILIYOJAA BARAKA TELE.
By. GEOFREY CHIRWA