18/03/2022
Usichukulie poa nyumba ni choo. Ujenzi wa vyoo bora na matumizi sahihi yatasaidia kutokuwepi na homa za matumbo na maradhi mengine yanayoendezwa na kutapakaa hovyo kwa kinyesi.
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa inawakumbusha wananchi wote kuwa suala la vyoo bora na matumizi sahihi ni lazima wakati wote ili kuwezesha kaya zote kuwa katika hali ya usafi wa Mazingira.
Timu za afya zinaendelea kupita na kukagua kila kaya ili kubaini wanaokiuka na kuvunja sheria ama kukaidi agizo la Ujenzi wa vyoo bora.