29/05/2026
Afisa Vijana wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Bi. Anna Tesha amewataka Vijana kuwa na nidhamu na Uadilifu katika Matumizi ya fedha wanazokopeshwa na Serikali kwani bila kufanya hivyo ni ngumu kufikia Malengo yao.
Ameyasema hayo Mwishoni mwa juma liliopita alipokua akizungumza na Vijana kwenye kikao cha Maelekezo na ujazaji wa Mikataba kwa Wanufaika wa Mkopo wa asilimia kumi ya Mapato ya ndani ya Halmashauri ambapo jumla ya Vikundi vya Vijana 37 vimepatiwa Mkopo wa fedha za Kitanzania Shilingi 1,242,423,500.
Bi. Tesha amesema kuwa kundi la Vijana ndio linaloongoza kwa kutofanya Marejesho kwa wakati hivyo inapelekea uaminifu kupungua dhidi yao.