Halmashauri ya wilaya ya Kalambo

Halmashauri ya wilaya ya Kalambo Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Halmashauri ya wilaya ya Kalambo, Government Organization, S. l. p 03, Kalambo.

Mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Dkt.Lazaro Komba ameikabidhi Kombe,Ng’ombe na seti moja ya jezi timu ya mpira wa ...
27/10/2025

Mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Dkt.Lazaro Komba ameikabidhi Kombe,Ng’ombe na seti moja ya jezi timu ya mpira wa miguu ya Mtapenda kutoka kata ya Mbuluma wilayani humo baada ya kuibuka na ushindi katika michezo ya ligi kuu ngazi ya wilaya ambayo ilikuwa ikiendelea kutimua vumbi katika uwanja wa Kateka kata ya Matai na kushirikisha timu 32.

Awali akikabidhi zawadi kwa timu zilizofanya vizuri kwenye michezo hiyo mkuu wa wilaya hiyo Dkt.Lazaro Komba ametumia fursa hiyo kuwataka vijana kujikita kwenye michezo ambayo itawawezesha kuimarisha afya na kuonesha vipaji vyao kwani michezo ni ajira.

Aidha ametumia fursa hiyo kuwataka vijana kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29-2025 ili kuchagua viongozi wanao wataka kwa maslahi ya jamii na Taifa kwa ujumla na kusisitiza kuwapuuza watu wanao shawishi vurugu na maandamano kupitia mitandao ya kijamii.

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu wilayani humo Ndugu Ajuaye Kaduma, amesema michezo hiyo itakuwa endelevu na kwamba timu ya Mtapenda FC kutoka kata ya Mbuluma imeshika nafasi ya kwanza na kuzawadiwa Kombe, Ng’ombe na seti moja ya jezi,Mshindi wa pili ilikuwa timu ya Maize Fc kutoka kata ya Mkali ambayo ilipata seti moja ya jezi na fedha shilingi elfu Hamsini (50,000/=) ikifuatiwa na timu White star kutoka kata Mkowe ambayo ilizawadiwa seti ya jezi na fedha shilingi elfu ishirini (20,000/=).

Michezo hiyo imedhaminiwa na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kalambo pamoja na Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU na kushirikisha timu 32 kutoka kata 23 za wilaya hiyo.

WASIMAMAZI 1,703 WA VITUO WAPATIWA MAFUNZO JIMBO LA KALAMBO.Tume huru ya uchaguzi katika jimbo la Kalambo mkoani Rukwa i...
27/10/2025

WASIMAMAZI 1,703 WA VITUO WAPATIWA MAFUNZO JIMBO LA KALAMBO.

Tume huru ya uchaguzi katika jimbo la Kalambo mkoani Rukwa imehitimisha utoaji mafunzo ya kuwajengea uwezo Makarani waongozaji wapiga kura,wasimamizi wasaidizi wa vituo na wasimamizi wasaidizi wa vituo wapatao 1,703 ambao watasimamia uchaguzi katika vituo 408.

Msimamzi wa uchaguzi jimbo la Kalambo Ndugu Ramadhani Mabula ametumia fursa hiyo kuwataka wasimamizi hao kufahamu kuwa uchaguzi ni mchakato unaojumuisha hatua na taratibu mbalimbali za kikatiba na kisheria ambazo hupaswa kufuatwa na kuzingatiwa hasa katika ngazi za vituo husika.

‘’nachukua fursa hii kuwasaa kuwa, Pamoja na uzoefu ambao baadhi yenu mnao katika uendeshaji wa uchaguzi,msiache kusoma Katiba,sheria, kanuni,taratibu, miongozo na maelekezo yanayotolewa na tume. Alisema Mabula.

Aidha alitumia fursa hiyo kuwataka wasimamizi kuzingatia maadili ikiwemo kuzingatia viapo kwa kutunza siri na kujitoa au kutokuwa wanachama wa vyama vya siasa katika kipindi chote cha uchaguzi.

Kwa upande wake afisa uchaguzi katika Halmshauri hiyo Ndugu Laulent Kapimpiti alitumia fursa hiyo kuwataka wasimamizi hao kuzingatia utekezaji wa majukumu, matakwa na masharti ya sheria ya uchaguzi ili kuepuka kuonekana kuwajibika kwenye mamlaka nyingine tofauti na tume katika kipindi hiki cha uchaguzi.

.VIONGOZI WA DINI WILAYANI KALAMBO WATOA WITO KWA WAUMINI KUPUUZA WATU WANAO HAMASISHA VURUGU NA MAANDAMANO KUPITIA MITA...
26/10/2025

.
VIONGOZI WA DINI WILAYANI KALAMBO WATOA WITO KWA WAUMINI KUPUUZA WATU WANAO HAMASISHA VURUGU NA MAANDAMANO KUPITIA MITANDAO YA KIJAMII.

Viongozi mbalimbali wa dini mkoani Rukwa wametoa wito kwa waumini wao juu kuwapuuza watu wanao shawishi kupitia mitandao ya kijamii ili kufanya vurugu na maandamano wakati wa uchaguzi mkuu na badala yake wajitokeze kutimiza haki yao ya kikatiba kwa kuwachagua viongozi wanao wataka kwa maslahi ya jamii na Taifa kwa ujumla.

Wameyabainisha hayo wakati wa ibada ya Jumapili na kusisitiza waumini kuendelea kuombea uchaguzi mkuu ili uweze kufanyika kwa amani na utulivu na kubainisha kuwa wao na serikali ni kituo kimoja hivyo ni jukumu lao kuhakikisha amani na upendo wakati wa uchaguzi vinatamalaki.

Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Ndugu Shafi Mpenda amefanya mazungumzo na viongozi wa ...
06/10/2025

Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Ndugu Shafi Mpenda amefanya mazungumzo na viongozi wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa na afya (TUGHE) ofisini kwake.

Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa imeanzisha utaratibu maalumu wa kutoa mafunzo kwa wataalamu wa bajeti amba...
06/10/2025

Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa imeanzisha utaratibu maalumu wa kutoa mafunzo kwa wataalamu wa bajeti ambayo yatawawezesha kuandaa mpango na bajeti wenye tija na utakao endana na hali halisi ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo.

Akiongea kupitia kikao cha kuwajengea uwezo wataalamu wa bajeti, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndugu Shafi Mpenda, amesema lengo ni kuwawezesha wataalamu kuwa na uwezo wa kundaa bajeti zinazotekelezeka ,uhalisia na shirikishi.
‘’Mpango na bajeti ni nyezo kuu ya utekelezaji wa dira na mikakati ya maendeleo ya Taifa, Mashirika, pamoja na Taasisi binafsi kwani bila mpango Madhubuti na bajeti inayotekezeka hata ndoto nzuri hubaki kwenye karatasi.’’alisema Mpenda.

Aidha aliwataka kuutumia ujuzi watakao upata kuutumia katika kuongeza chachu ya kuhakikisha rasilimali chache zinakuwa kwenye mpango na kutumika kwa tija, uwazi na uwajibikaji na kusisiza elimu hiyo kuwafikia wataalamu wote hadi ngazi ya Vijiji na Kata.

Hata hivyo mafunzo hayo yanajumuisha wakuu vitengo na Divisheni pamoja na wataalamu wa bajeti kwa ngazi ya Halmashauri.www.kalambodc.go.tz

01/10/2025
27/09/2025

Mkuu wa wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Dkt. Lazaro Komba amesema maandalizi ya kuupokea Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2025 wilayani humo yamekamilika kwa kiwango cha kuridhisha na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mapokezi hayo k**a ishara ya mshik**ano na kuunga mkono juhudi za maendeleo.

Amesema wilaya inatarajia kuupokea Mwenge wa Uhuru 30 Septemba 2025 na utakimbizwa kilometa 183.4 kwa kukagua miradi 11 yenye thamani ya shilingi billion 1.9.

Mwenge wa Uhuru uliwashwa kwa mara ya kwanza juu ya kilele cha mlima Kilimanjaro mwaka 1961 na kumulika ndani na nje ya ...
26/09/2025

Mwenge wa Uhuru uliwashwa kwa mara ya kwanza juu ya kilele cha mlima Kilimanjaro mwaka 1961 na kumulika ndani na nje ya mipaka ili kuleta matumaini pale ambapo kuna kukata tamaa, upendo pale kwenye chuki na heshima pale kwenye dharau.

Aidha Halmashauri ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa ni miongoni mwa Halmashauri ambazo zimekuwa zikiupokea mwenge wa uhuru kila mwaka na kuukimbiza katika maeneo tofauti ,ambapo kwa mwaka 2025 mwenge wa uhuru Utazindua miradi na kuweka mawe ya msingi katika miradi 11.www.kalambodc.go.tz

26/09/2025

Mwenge wa Uhuru uliwashwa kwa mara ya kwanza juu ya kilele cha mlima Kilimanjaro mwaka 1961 na kumulika ndani na nje ya mipaka ili kuleta matumaini pale ambapo kuna kukata tamaa, upendo pale kwenye chuki na heshima pale kwenye dharau.

Aidha Halmashauri ya wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa ni miongoni mwa Halmashauri ambazo zimekuwa zikiupokea mwenge wa uhuru kila mwaka na kuukimbiza katika maeneo tofauti ,ambapo kwa mwaka 2025 mwenge wa uhuru Utazindua miradi na kuweka mawe ya msingi katika miradi 11.

Wananchi katika kijiji cha Matai asilia wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa wameadhimisha siku ya afya na lishe iliyokuwa na ...
25/09/2025

Wananchi katika kijiji cha Matai asilia wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa wameadhimisha siku ya afya na lishe iliyokuwa na lengo la kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya vyakula bora na vyenye virutubishi.

Afisa Lishe wilayani humo ndugu Robert Tepeli kupitia maadhimisho hayo amebainisha kuwa maadhimisho hayo yanafanyika katika vijiji 68 vya wilaya hiyo yakiwa na lengo la kutoa elimu katika jamii juu ya namna bora ya kundaa vyakula vyenye virutubishi kwa Watoto wenye umri chini ya miaka 5.

Address

S. L. P 03
Kalambo

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Halmashauri ya wilaya ya Kalambo posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share