28/08/2026
KATA 15 ZAWASILISHA TAARIFA ZA MAENDELEO KASULU TC
Katika kuchochea maendeleo ya Halmashauri ya Mji Kasulu, Kata zote 15 za zimewasilisha taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika kikao cha Madiwani na Wakuu wa Idara kilichofanyika katika Ukumbi wa Fatina H. Raay.
Taarifa hizo zimeainisha hatua mbalimbali zilizofikiwa katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo ikiwemo masuala ya uchumi, afya, elimu, usalama, usafi wa mazingira na utoaji wa huduma za kijamii kwa wananchi.
Akizungumza katika kikao hicho, Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu Therezia Mtewele, amesisitiza umuhimu wa uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu na kuwataka viongozi katika ngazi za Kata kuendelea kuhamasisha wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Mwl. Vumilia J. Simbeye ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa viongozi wa Kata na wadau mbalimbali katika kuhakikisha miradi na shughuli za maendeleo zinatekelezwa kwa ufanisi na kwa kuzingatia mahitaji ya wananchi.
Madiwani wamepokea taarifa hizo na kusisitiza umuhimu wa kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri ili kuchochea utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.