Tawi La MwembeTayari/CCM

Call Contact the organization

Tawi La MwembeTayari/CCM KARIBU KATIKA UKURASA RASMI WA TAWI LA MWEMBE TAYARI, KATA YA MKUZA| WILAYA KIBAHA MJINI| MKOA PWANI

*MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI KIBAHA MJINI MWL. MWAJUMA AMIR NYAMKA ASHIRIKI HALFA YA KUFUNGA MAFUNZO KWA WALIMU WA...
30/06/2026

*MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI KIBAHA MJINI MWL. MWAJUMA AMIR NYAMKA ASHIRIKI HALFA YA KUFUNGA MAFUNZO KWA WALIMU WA CCM LEO*

Leo Mwalimu Mwajuma Nyamka ameshiriki hafla ya kufunga mafuzo maalumu kwa walimu wa Chama cha Mapinduzi, yaliyolenga kuimarisha uwezo wa uongozi, malezi ya wanachama, kuendeleza maadili, itikadi, maadili na uzalendo pamoja na misingi ya chama.

Akizungumza katika hafla hiyo Ndg.Bi Mwl. Mwajuma Nyamka alisisitiza kuwa walimu ndio hazina ya chama, nguzo ya malezi kwa wanachama, na daraja muhimu kuendeleza misingi ya umoja, sera na historia ya Chama cha Mapinduzi, na mageuzi mbalimbali ya kimifumo ndani ya chama. Alilisitiza walimu wa chama (makada) wana wajibu mkubwa wa kujenga kizazi chenye uelewa, nidhamu na uwajibikaji na uzalendo wa kweli.

Aidha aliwataka wahitimu wa mafunzo hayo kwenda kuwa mabalozi wa umoja, mshik**ano na maendeleo katika maeneo yao, wakitumia maarifa waliyoyapata kuimarisha chama, utendeaji na kuongeza ufanisi katika shughuli za chama na kusimamia kwa vitendo utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi pamoja na kuendeleza Tunu za Muungano.

Nguvu ya Chama ipo chetu ipo katika elimu, umoja na mshikamno.

*CCM MOJA KIBAHA MOJA*
CCM CHAMA CHA WATU, CHAMA CHA USHINDI

Hazikuwa mbio za bendera tu, bali zilikuwa ni ishara ya uongozi madhubuti, uwajibikaji, utii na uzalendo wa kweli kwa Ch...
27/06/2026

Hazikuwa mbio za bendera tu, bali zilikuwa ni ishara ya uongozi madhubuti, uwajibikaji, utii na uzalendo wa kweli kwa Chama na Jumuiya inayotambua wajibu wake wakati wote. Katika nyakati ambazo hofu na mashaka yalitaka kuingia mioyoni mwa baadhi ya askari, ukak**avu, busara na uthubutu vilionekana wazi kupitia Mkuu wa Kikosi cha Ardhini, Ndugu Ramadhani Kazembe.

Baada ya kupokea amri kutoka kwa Mkuu wa Vikosi, Bi. Mwajuma Amir Nyamka, bila kusita wala kuyumbishwa na mazingira, alisimama imara k**a askari mwenye nidhamu ya hali ya juu, akaongoza kikosi kwa weledi mkubwa na kuhakikisha kuwa bendera ya Chama inaendelea kupepea kwa fahari katika milingoti yake. Kitendo hicho hakikuwa tu utekelezaji wa amri, bali kilidhihirisha moyo wa kujitolea, uaminifu na mapenzi ya dhati kwa Chama.

Ramadhani Kazembe ameendelea kujijengea sifa ya kuwa kiongozi mwenye unyenyekevu, mtii wa mamlaka halali, mwenye uwezo wa kuhamasisha wenzake na mwenye uthabiti katika nyakati za changamoto. Ni aina ya viongozi wanaoamini kuwa mafanikio ya taasisi yanatokana na nidhamu, mshik**ano na kutanguliza maslahi ya Chama mbele ya maslahi binafsi.

Kwa hakika, askari wa aina ya Ramadhani Kazembe ni hazina adimu sana katika zama hizi. Ni watu ambao hawapatikani kwa wingi na wakati mwingine historia hulazimika kusubiri miaka mingi kupata mtu mwenye mchanganyiko wa ujasiri, uaminifu, unyenyekevu na uwezo wa kutekeleza majukumu kwa ufanisi k**a wake. Hivyo ni wajibu wa kila mmoja kumthamini, kumlinda na kumuunga mkono ili aendelee kuwa mfano bora kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Hongera Ndugu Ramadhani Kazembe kwa kuendelea kuwa alama ya utii, uwajibikaji, uzalendo na uongozi wa vitendo. Watu wa aina yako ndiyo nguzo zinazofanya taasisi na jumuiya zetu ziendelee kusimama imara hata katika nyakati ngumu. Bendera imeendelea kupepea si kwa sababu ya upepo pekee, bali kwa sababu kuna watu jasiri na waaminifu walio tayari kuibeba kwa heshima na kuilinda kwa gharama yoyote.

LEO 01/06/2026 Mwenyekiti wa Tawi la Mwembe Tayari, Bi. Hadija Kondo Kombe akiongozana na wajumbe wa k**ati ya siasa ya ...
01/06/2026

LEO 01/06/2026 Mwenyekiti wa Tawi la Mwembe Tayari, Bi. Hadija Kondo Kombe akiongozana na wajumbe wa k**ati ya siasa ya Tawi, walifanya ziara ya kikazi kukutana na uongozi wa Serikali ya Mtaa wa Mkuza chini ya Bw. Dickson Abisai Maula

Lengo la ziara hiyo lilikuwa kujionea utekelezaji wa Ilani, kutathimini maendeleo yaliyofikiwa katika mtaa huo pamoja na kubadilishana mawazo kuhusu njia bora za kuimarisha ushirikiano katika ya Chama na Serikali ya Mtaa ili kuongeza kasi ya maendeleo na ustawi wa wananchi wa Mkuza.

Katika mazungumzo hayo, Viongozi hao walijadili maswala mbalimbali ya maendeleo yanayogusa maisha ya wananchi, huku wakisisitiza umuhimu wa mshik**ano, uwajibikaji na ushirikishwaji wa wananchi katika utekelezaji wa miradi na shughuli za maendeleo.

Ziara hii ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea kikao cha Halmashauri kuu ya Tawi, ambapo taarifa za utekelezaji wa majukumu mbalimbali na maendeleo ya Tawi zitawasilishwa kwa ajili ya tathimini na kupanga mikakati ya kuendelea kuwatumikia wananchi kwa ufanisi zaidi.

Maendele ya wananchi yanaitaji ushirikiano wa karibu kati ya Chama, Serikali na Wananchi wenyewe. Tukiwa pamoja tunaweza kufanikisha mengi zaidi kwa ajili ya mkuza yetu.

Imetolewa Na;
Katibu Siasa Uenezi
Tawi la Mwembe Tayari
Emanuel Kaombwe

TAARIFA KWA UMMA
25/03/2026

TAARIFA KWA UMMA

SAVE THE DATE.. ZOEZI LA KUPATA KITAMBULISHO/NAMBA YA NIDA SASA LIMEREJEA KWENYE KATA YAKO MANISPAA YA KIBAHA. PONGEZI Z...
23/03/2026

SAVE THE DATE.. ZOEZI LA KUPATA KITAMBULISHO/NAMBA YA NIDA SASA LIMEREJEA KWENYE KATA YAKO MANISPAA YA KIBAHA. PONGEZI ZIMFIKIE MKUU WA WILAYA NICKSON SAIMON (NIKI WA PILI) KWA KUHAKIKISHA SERIKALI YA DR SAMIA SULUHU HASSAN INAENDELEA KUWAHUDUMIA WANANCHI KWA UKARIBU ZAIDI

๐Ÿ”ฅ KIBAHA MJINI ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ’ช๐Ÿพ VIJANA TUNASONGA MBELE!Kesho Jumamosi tarehe 31/01/2026, tunafikia KILELE CHA MBIO ZA BENDERA ๐Ÿ“ Viwan...
30/01/2026

๐Ÿ”ฅ KIBAHA MJINI ๐Ÿ”ฅ
๐Ÿ’ช๐Ÿพ VIJANA TUNASONGA MBELE!

Kesho Jumamosi tarehe 31/01/2026, tunafikia KILELE CHA MBIO ZA BENDERA

๐Ÿ“ Viwanja vya Ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha Mjini

Ni siku ya umoja, mshik**ano na uthibitisho wa nguvu ya vijana ndani ya Chama chetu.

Vijana wa CCM tuko tayari kulinda misingi ya taifa na kusukuma mbele maendeleo ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟโœŠ๐Ÿพ

๐Ÿ“ก Tukio litarushwa LIVE kupitia:
๐Ÿ”ด Facebook
๐Ÿ”ด Instagram

๐Ÿ—ฃโ€œTUMECHAGUA UMOJA NA AMANI KWA MAENDELEO YA TAIFA LETUโ€ ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ
๐Ÿ“ฃ Karibuni nyote โ€“ vijana, wanachama na wananchi!
CCM OYEE! VIJANA OYEE!

MBIO ZA BENDERA โ€“ MIAKA 49 YA CCM ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟUVCCM Kibaha Mjini, chini ya uongozi thabiti wa Mwenyekiti wa Vijana Ndugu Ramadhani...
13/01/2026

MBIO ZA BENDERA โ€“ MIAKA 49 YA CCM ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

UVCCM Kibaha Mjini, chini ya uongozi thabiti wa Mwenyekiti wa Vijana Ndugu Ramadhani Kazembe, wanakuletea Mbio za Bendera zenye lengo kubwa na la kizalendo ๐Ÿ’ช๐Ÿพ

Ni mbio za hamasa, umoja na mshik**ano, zikibeba ujumbe mzito wa:
โœ… Kutangaza na kuelimisha utekelezaji wa Ilani ya CCM
โœ… Kuhamasisha ushiriki wa vijana, wakina mama na wananchi wa rika lote
โœ… Kuadhimisha miaka 49 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi โ€“ chama cha ushindi, amani na maendeleo ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ

Mbio hizi si za kasi pekee, bali ni mbio za fikra, mshik**ano na uzalendo, zikilenga kuwakutanisha wananchi wote bila kujali umri wala jinsia, kushiriki kwa pamoja katika kujenga uelewa, moyo wa kujitolea na uzalendo kwa Taifa na Chama.
๐Ÿ”ฅ๐Ÿ™‹โ€โ™‚๏ธ Vijana jitokezeni kuonesha nguvu na ari ya kizazi cha sasa
๐Ÿ‘ฉWakina Mama mshiriki k**a nguzo muhimu ya jamii
๐Ÿ‘ด๐Ÿฝ๐Ÿง’๐Ÿพ Wazee na watoto โ€“ mkaribishwa kushuhudia na kushiriki shamrashamra
Kauli mbiu yetu: โ€œKULINDA NA KUJENGA UJAMAAโ€





๐Ÿ‘‰ CCM ni Historia, CCM ni Leo, CCM ni Kesho
Usikose kushiriki โ€“ Coming Soon!

Mwalimu Mwajuma AMIR Nyamka, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kibaha Mjini, anawatakia wana-CCM wote heri ya ...
23/12/2025

Mwalimu Mwajuma AMIR Nyamka, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kibaha Mjini, anawatakia wana-CCM wote heri ya Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya wenye baraka tele.
Tunawahimiza kuendelea kusherehekea sikukuu hizi kwa amani, upendo na mshik**ano wa dhati, tukidumisha maadili ya utu, heshima na umoja ambayo yameijenga CCM na Taifa letu kwa ujumla. Tuutumie Mwaka Mpya k**a fursa ya kuimarisha mshik**ano wetu, kuongeza bidii katika kuwatumikia wananchi, na kuendeleza mapambano ya maendeleo, haki na ustawi wa jamii. Umoja wetu ni nguvu yetu, tushik**ane, tushirikiane na kulinda amani ya nchi yetu kwa vitendo na maneno.



TAARIFA KWA UMMAKuhusu Ushiriki wa Meya Dkt. Nicas Mawazo katika Kikao cha Kazi cha Mkuu wa Mkoa na Ziara za Kimaendeleo...
19/12/2025

TAARIFA KWA UMMA

Kuhusu Ushiriki wa Meya Dkt. Nicas Mawazo katika Kikao cha Kazi cha Mkuu wa Mkoa na Ziara za Kimaendeleo

Meya wa Jiji, Dkt. Nicas Mawazo, ameshiriki katika kikao cha kazi kilichoongozwa na Mkuu wa Mkoa, kilicholenga kufanya tathmini ya utekelezaji wa ahadi za siku 100 za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Katika kikao hicho, Meya alieleza mafanikio yaliyopatikana pamoja na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya jiji, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali ya Mkoa, Halmashauri na taasisi nyingine za umma ili kuhakikisha malengo ya Rais yanafikiwa kwa ufanisi.

Aidha, Meya alikutana na Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa ajili ya kujadili hali ya miundombinu ya barabara, hususan utekelezaji wa miradi ya ujenzi na ukarabati wa barabara, pamoja na mikakati ya kuboresha usafiri kwa wananchi.

Katika kuendelea na majukumu yake, Dkt. Mawazo alifanya ziara katika kituo cha afya kilichopo mkoani, ambapo alipata fursa ya kujionea maendeleo ya huduma za afya, miundombinu iliyopo, pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili wahudumu wa afya. Meya alisisitiza umuhimu wa kuboresha huduma za afya ili kuendana na mahitaji ya wananchi na kuongeza ufanisi wa utoaji huduma.

Meya alihitimisha kwa kuahidi kuendelea kushirikiana na wadau wote wa maendeleo kuhakikisha miradi inayotekelezwa inaleta tija kwa wananchi na kuendana na maelekezo ya Serikali ya Awamu ya Sita.

Address

MBELA Road
Kibaha

Opening Hours

Monday 11:00 - 20:00
Wednesday 11:00 - 20:00
Friday 11:00 - 20:00
Sunday 11:00 - 20:00

Telephone

+255718596679

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tawi La MwembeTayari/CCM posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Tawi La MwembeTayari/CCM:

Shortcuts

Share