HW Mbinga

HW Mbinga Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.

Taarifa kwa Umma.Lipa kodi na tozo za Serikali kwa ustawi wa taifa.
03/09/2026

Taarifa kwa Umma.

Lipa kodi na tozo za Serikali kwa ustawi wa taifa.

MKURUGENZI MBINGA DC AKUTANA NA WADAU WA MAKAA YA MAWE, ASISITIZA ULIPAJI WA USHURU NA MADENI YA SERIKALI ​Mkurugenzi Mt...
01/09/2026

MKURUGENZI MBINGA DC AKUTANA NA WADAU WA MAKAA YA MAWE, ASISITIZA ULIPAJI WA USHURU NA MADENI YA SERIKALI

​Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, ndugu Joseph Kashushura amefanya kikao kazi na wawakilishi wa makampuni na wadau wa maendeleo wanaojishughulisha na usafirishaji wa makaa ya mawe Wilayani hapo, huku akiwataka kuhakikisha wanalipa ushuru wa Halmashauri kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo.

​Katika kikao hicho kilichofanyika leo tarehe 01 Septemba, 2026 kilicholenga kuimarisha ushirikiano na uboreshaji wa ukusanyaji wa mapato ya ndani, Mkurugenzi Kashushura amesisitiza kuwa usafirishaji wa rasilimali hiyo lazima uendane na uwajibikaji wa kisheria ili kuiwezesha Halmashauri kutimiza wajibu wake kwa wananchi.

Kashushura ameeleza kuwa makampuni yote yanayojisajili na kufanya shughuli za usafirishaji wa makaa ya mawe yanatakiwa kuwasilisha ushuru halali wa Halmashauri kwa wakati kuepuka kulimbikiza madeni.

"Nimewaita hapa kuwambusha madeni ya ushuru mnayodaiwa muanze  kuyalipa mara moja kulingana na taratibu zilizowekwa ili nasi tutekeleze miradi ya maendeleo."Alisisitiza Kashushura

Kashushura alifafanua kuwa mapato yanayokusanywa kupitia ushuru huo ndiyo msingi mkuu unaoiwezesha Serikali kupitia Halmashauri kujenga na kuboresha miundombinu ya afya, elimu, maji, na barabara kwa ajili ya wananchi wa Mbinga.

Mkurugenzi Kashushura aliongeza kuwa Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji kwa kuboresha miundombinu lakini haitasita kuchukua hatua za kisheria kwa kampuni zitakazokiuka taratibu za ulipaji wa kodi na ushuru.

​Wadau na wawakilishi wa makampuni hayo wameahidi kushirikiana kwa karibu na Halmashauri ili kuhakikisha taratibu zote za kisheria zinatekelezwa na madeni yanayodaiwa yanalipwa kwa wakati.

#

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, ndugu Joseph Kashushura, Timu ya Menejimenti na watumishi wote w...
29/08/2026

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, ndugu Joseph Kashushura, Timu ya Menejimenti na watumishi wote wanakupongeza Mhe. Deogratius John Ndejembi kwa kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kazi na Utu Tunasonga Mbele

#
#
#
#

MADIWANI WATAKIWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KUINUA UFAULU WA WANAFUNZI SHULENI ​Na Suzana NdosiKatibu Tawala Wilaya ya Mbinga...
28/08/2026

MADIWANI WATAKIWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KUINUA UFAULU WA WANAFUNZI SHULENI

​Na Suzana Ndosi
Katibu Tawala Wilaya ya Mbinga (DAS), ndugu Pendo Ndumbaro, ametoa wito kwa madiwani wote kushiriki kikamilifu katika kuimarisha na kupandisha kiwango cha ufaulu wa wanafunzi katika shule za Msingi na Sekondari, akisisitiza kuwa elimu ndiyo msingi mkuu wa maendeleo.

Ametoa wito huo leo tarehe 28 Agosti, 2026 kwenye kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya nne 2025/2026 kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri.

" Mbinga DC tuko vizuri kwenye maeneo mengine kwenye elimu tu ndipo panahitaji juhudi za pamoja kuongeza ufaulu. "Alieleza Ndumbaro.

​Aidha, Ndumbaro ameeleza kuwa Halmashauri tayari imeonyesha jitihada kubwa za makusudi kwa kufanya ziara na kutembelea shule kwa ajili ya kukagua mazingira ya ujifunzaji na kufuatilia maendeleo ya taaluma. Hata hivyo, amebainisha kuwa ushirikiano wa karibu kutoka kwa madiwani katika ngazi za kata utaongeza chachu ya kuleta matokeo bora zaidi kwenye mitihani ya kitaifa.

​Katika hatua nyingine, Pendo Ndumbaro amempongeza Mkurugenzi Mtendaji pamoja na timu yake ya wataalamu kwa kazi kubwa  iliyotukuka ya ukusanyaji wa mapato ya ndani, ambapo Halmashauri imefanikiwa kuvuka lengo na kufikia asilimia 120 huku akisisitiza juhudi ziongezwe katika kubuni vyanzo vipya vya mapato ikizingatiwa kuwa Halmashauri hiyo imeongezewa makisio ya makusanyo hadi kufikia bilioni 14 mwaka 2026/2027.

​Pamoja na mafanikio hayo ya kifedha, amepongeza pia hatua za haraka zilizochukuliwa katika kutatua kero za miundombinu ya barabara kwa kuzichonga na kuziweka katika hali inayopitika kwa urahisi muda wote. Hatua hiyo inarahisisha usafirishaji wa wananchi, bidhaa, na huduma mbalimbali za kijamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.

Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, Mhe. Desderius Haule, ametoa wito wa kuharakishwa k...
28/08/2026

Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, Mhe. Desderius Haule, ametoa wito wa kuharakishwa kwa utekelezaji wa uwekezaji katika maeneo yote yanayomilikiwa na halmashauri hiyo kwa kujenga miradi ya kimkakati itakayoongeza mapato.

Mhe. Haule ameeleza hayo leo tarehe 28 Agosti, 2026 katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2025/2026 ambapo amemuelekeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kuonana mara moja na Katibu Tawala wa Mkoa ili kushughulikia upatikanaji wa vibali vinavyohitajika ili utekelezaji wa miradi hiyo uanze bila kuchelewa.

​Akifafanua kuhusu maeneo hayo, Mhe. Haule alibainisha kuwa sehemu kubwa ya ardhi hiyo ipo ndani ya eneo la Halmashauri ya Mbinga Mji, jambo linalotoa fursa kubwa ya kiuchumi. Alieleza kuwa uwekezaji ukifanyika katika maeneo hayo, Halmashauri ya Mji nayo  itanufaika kwa kiasi kikubwa kupitia ushuru wa majengo pamoja na kodi nyingine za kisheria.

​"Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania anasisitiza kila Halmashauri iwe na uwekezaji ili kuongeza mapato. Mbinga DC tunataka miradi ya kimkakati itakayoiletea Halmashauri yetu faida." Alisisitiza Mhe. Haule.

Aidha, Mwenyekiti aliwataka Waheshimiwa Madiwani kurejea kwenye Kata zao na kuwapa wananchi taarifa sahihi kuhusu miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita.

Mhe. Haule alitumia fursa hiyo kuwapongeza wajumbe wa kamati zote za Baraza la Madiwani kwa ushirikiano mzuri waliouonyesha pamoja na Menejimenti ya Halmashauri katika mwaka wa fedha wa 2025/2026, hatua iliyofanikisha utekelezaji wa majukumu ya halmashauri kwa ufanisi.

28/08/2026

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, ndugu Joseph Kashushura ameeleza kuwa Halmashauri hiyo imekusudia kurekebisha barabara zilizoharibika kwa kuzichonga.

Ameyasema hayo leo tarehe 28 Agosti, 2026 katika Kikao cha Baraza la Madiwani robo ya nne mwaka wa fedha 2025/2026 kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri makao makuu.

Sambamba na hilo, alibainisha kuwa Serikali imetoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya shule huku akitoa wito kwa Waheshimiwa Madiwani kutoa ushirikiano hususani ya nguvu ya wananchi wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo ili kuwezesha kukamilika kwa wakati na kwa bajeti iliyopangwa.

Kimkakati

MBINGA DC YAFUZU KUINGIA NUSU FAINALIVijana barobaro wa Mbinga DC wameendelea kufanya vizuri katika mchezo wa mpira wa m...
27/08/2026

MBINGA DC YAFUZU KUINGIA NUSU FAINALI

Vijana barobaro wa Mbinga DC wameendelea kufanya vizuri katika mchezo wa mpira wa miguu na kufuzu kuingia nusu fainali baada ya mechi ya vuta ni kuvute kati ya Mbinga DC na Ushetu DC na kutoka bila bila.

Kisha Mbinga DC kuwachapa Ushetu mikwaju ya penalt 03-02 na kupata tiketi ya kufuzu kuingia nusu fainali.

Kongole kwa vijana.

Mbinga DC sio vibonde wenu.

MADIWANI WATAKIWA  KUSIMAMIA MATUMIZI YA FEDHA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya...
27/08/2026

MADIWANI WATAKIWA  KUSIMAMIA MATUMIZI YA FEDHA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mhe. Desderius Haule amewataka madiwani kuendelea kusimamia kwa karibu matumizi ya fedha na utekelezaji wa miradi ya maendeleo inaayotekelezwa kwenye Kata zao, ikiwa ni msingi muhimu wa kuharakisha maendeleo ya wananchi.

Mhe. Haule ameyasema hayo leo Agosti 27, 2026 kwenye kikao cha uwasilishaji wa taarifa za  utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika kipindi cha robo ya nne ya mwaka wa fedha 2025/2026.

Aidha,  Mhe. Haule amesisitiza  madiwani kuendelea kusimamia kwa karibu matumizi ya fedha na utekelezaji wa miradi inayotumia fedha za ndani.

Kwa upande mwingine, Mhe. Adolf Komba, Diwani wa kata ya Ngima ameishukuru Serikali na uongozi wa Halmashauri ya Mbinga DC  kwa kupeleka mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari utakaogharimu takribani Shilingi 560,000,000 kutoka Serikali kuu.

“Kata ya Ngima haikuwa na Shule ya Sekondari kwa muda mrefu, mradi huu umejibu kilio cha Wananchi” -Alisema Mhe. Komba

Katika kipindi cha Aprili hadi Juni 2026, Madiwani wameeleza utekelezaji wa shughuli mbalimbali zinazolenga kuboresha huduma na ustawi wa wananchi, ikiwemo maendeleo ya miundombinu, elimu, afya, maji, kilimo na huduma nyingine za kijamii na kiuchumi huku wakiomba Serikali iweze kuboresha miundombinu ya barabara kuwaondolea adha wananchi hususani kipindi hiki cha mavuno.

MBINGA DC YAWAKUMBUSHA WADAU WA NYAMA  KUSHIRIKIANA NA WATAALAMU KUIMARISHA USALAMA WA BIDHAA.Mkuu wa Divisheni ya Kilim...
26/08/2026

MBINGA DC YAWAKUMBUSHA WADAU WA NYAMA  KUSHIRIKIANA NA WATAALAMU KUIMARISHA USALAMA WA BIDHAA.

Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhandisi Evance Haule, amewataka wadau wa sekta ya nyama wakiwemo wachinjaji, wamiliki wa mabucha, na wauza nyama kudumisha ushirikiano wa karibu na wataalamu wa mifugo ili kuimarisha ubora na usalama wa bidhaa hiyo kwa jamii.

​Wito huo umetolewa wakati wa kikao kazi leo tarehe 26 Agosti, 2026 kilichowakutanisha wadau hao katika ukumbi wa Halmashauri kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya usimamizi, uendeshaji, na uzingatiaji wa sheria katika mnyororo wa thamani wa nyama.

Mhandisi Haule amewataka wadau hao kuzingatia kuuza nyama ambayo imepimwa na kukaguliwa na mtaalamu wa mifugo aliyethibitishwa. Hatua ambayo ni muhimu ili kuhakikisha nyama inayomfikia mlaji inafaa kwa matumizi ya binadamu.

Aidha, wadau wamekumbushwa kuongeza umakini katika usafi wa maeneo ya kuchinjia, vyombo vya usafirishaji, na mabucha ili kuepusha hatari ya milipuko ya magonjwa.

Mhandisi Haule alisisitiza  wadau wote kuhakikisha wana vibali vyote vinavyotakiwa kwa mujibu wa sheria pamoja na kulipa ushuru wa Halmashauri kwa wakati ili kuchangia maendeleo katika jamii.

Aidha, Afisa Mifugo, ndugu Haruna Masige alieleza kuwa ni muhimu wadau hao kuwa na viongozi ambao watakuwa na jukumu la kuimarisha umoja miongoni mwao pamoja na kuhusika katika kutatua changamoto qanazokabiliana nazo kwa kushirikiana na viongozi wa Halmashauri. 

Wadau waliteua wajumbe kadhaa na kupiga kura ambapo ndugu Hance Patrick Turuka kutoka Amani Makoro alichaguliwa kuwa Mwenyekiti, ndugu Zandati John Mdegela kutoka Mapera kuwa Mwenyekiti Msaidizi, ndugu Patrick.      kutoka Mkumbi Katibu, ndugu Baltazary B Nchimbi wa Ukata Katibu Msaidizi na Baraka Mbena wa Kigonsera kuwa Mtunza Hazina.

26/08/2026

Address

Kiamili/Kigonsera
Mbinga

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when HW Mbinga posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to HW Mbinga:

Shortcuts

Share