Darasa huru la Sheria Mbali Mbali Za Nchi Yetu Tanzania.

Darasa huru la Sheria Mbali Mbali Za Nchi Yetu Tanzania. tunajifunza Sheria pamoja na Mambo mbali mbali yanayohusiana na sheria za nchi Yetu pamoja na msaada wa kisheria

JE, WAJUA?Kwa mujibu wa kifungu cha 8 cha Kanuni ya Adhabu (The Penal Code), Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania kutokujua ...
30/07/2020

JE, WAJUA?
Kwa mujibu wa kifungu cha 8 cha Kanuni ya Adhabu (The Penal Code), Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania kutokujua sheria hakuwezi kumwondolea hatia mtuhumiwa. Utaratibu huu hutumika katika mataifa yote pale ambapo shauri linasikilizwa mahak**ani au katika vyombo vingine vyenye hadhi ya kimahak**a (Quasi-Judicial bodies).

Utaratibu huu hutumika katika masuala yote ya kisheria, ikujumuisha pia mashauri ya madai. Kwa hiyo, ni wajibu wa kila mtu katika jamii kujua sheria, angalau zile zinazozunguka maisha yake ya kila siku, ili inapotokea kwamba ameingia katika mgogoro basi ujuzi alionao umsaidie. Hakuna anayehurumiwa kwa kigezo cha kutokujua Sheria.

Je kuna sheria ya mtoto Tanzania ? Tanzania inayosheria ya mtoto iliyotungwa na Bunge na kutiwa saini na rais wa Jamhur ...
19/07/2020

Je kuna sheria ya mtoto Tanzania ? Tanzania inayosheria ya mtoto iliyotungwa na Bunge na kutiwa saini na rais wa Jamhur ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2009 . Sheria hiyo inatambuliwa k**a Sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009.
Je mtoto ni nani ? Kwa mujibu wa kifungu namba 4(1) ya sheria ya mtoto . Mtoto ni mtu yeyote aliye chini ya miaka kumi na nane (18).

*LEO TUZUNGUMZIE UGAIDIUgaidi ni mfumo wa kulenga mabadiliko ya kisiasa kwa kutisha watu kwa njia ya vurugu au mauaji. M...
17/07/2020

*LEO TUZUNGUMZIE UGAIDI
Ugaidi ni mfumo wa kulenga mabadiliko ya kisiasa kwa kutisha watu kwa njia ya vurugu au mauaji. Matendo ya kigaidi yanatisha kwa sababu watu wanajeruhiwa au kuuawa. Watendaji wa ugaidi kwa kawaida ni vikundi au watu wasio na cheo au nafasi rasmi.

Mara nyingi si rahisi kutofautisha kati ya magaidi, wapinzani wa uhuru au watu wanaoendesha vita ya msituni. Hata jeshi rasmi za serikali zinaweza kutumia mbinu za kigaidi lakini kwa kawaida hawahesabiwi kati ya magaidi.

*UGAIDI NA TAFSIRI KATIKA SHERIA YA KUZUIA UGAIDI SURA YA 19 YA MWAKA 2002.

Tafsiri na kuzuiwa kwa vitendo vya ugaidi.kifungu cha

4.-(1) Hapana mtu yeyote katika Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania nahapana raia wa Tanzania aishiye nje ya Jamhuri ya Muungano akayeruhusiwa kufanyakitendo cha kigaidi na mtu yeyote atakaye fanya hivyo atakuwa ametenda kosa la jinai.
(2) Mtu atatenda kosa la kigaidi ikiwa kwa nia ya ugaidi atatenda au hatatenda kitendo ambacho-
(a) kinaweza kufanya uharibifu mkubwa kwa nchi au shirika
la kimataifa; au
(b) kimekusudiwa au kinaweza kusemekana kuwa kimekusudiwa-
(i) kutishia uma kwa kiwango kikubwa;
(ii) kuilazimisha Serikali kufanya au kutokufanya kitendo
chochote;
(iii) kudhoofisha au kuharibu kwa kiwango kikubwa misingi ya kisiasa, kikatiba, kiuchumi au miundo ya kijamii ya nchi au shirika la kimataifa; au
(iv) kuishawishi Serikali hiyo au shirika hilo la kimataifa; au
(c) kinahusisha au kusababisha, kulingana na mazingira-
(i)shambulio kwa maisha ya mtu ambalolinaweza kusababisha kifo;
(ii) shambulokwa uadilifu wa mtu;
(iii) utekaji wa mtu.

(3) Kitendo kitatafsiriwa kuwa ni ugaidi kwa mujibu wa Sheria hii ikiwa kitendo au tishio la kitendo ambacho-
(a) kinahusisha majeraha makubwa kwa mtu;
(b) kinahusisha uharibifu mkubwa wa mali;
(c) kinahatarisha maisha ya mtu;
(d) kinaasababisha hatari kubwa kwa afya au usalama wa uma au sehemu ya uma;
(e) kinahusisha utumiaji wa silaha za moto au milipuko;
(f) kinahusisha utolewaji kwenye mazingira au sehemu yake au kusambaza au kuiweka jamii au sehemu ya jamii katika
(i) hatari yoyote, miali au viini hatarishi;
(ii) kemikali za sumu;
(iii) viumbe maradhia au ajenti wa kibaologia au sumu;
(g) kimeundwa au kimedhamiriwa kivuruge mifumo ya kompyuta au utoaji wa huduma inayohusiana moja kwa moja na mitambo ya mawasiliano, huduma za kibenki au za kifedha, usafiri au mitambo mingine muhimu;
(h) kimeundwa au kimedhamiriwa kuvuruga utoaji wa huduma muhimu za dharura k**a vile polisi, ulinzi wa raia au huduma za kitabibu;
(i) kinahusisha kuleta hatari kwa usalama wa taifa au usalama wa uma, na kudhamiriwa , au kwa jinsi kilivyo,
kinaweza kuonekana kuwa kimedhamiria -
(i) kuutisha uma au sehemu ya uma;
(ii) kuilazimisha Serikali au shirika la kimataifa kufanya au kuacha kufanya kitendo chochote, na kinatendwa kwa madhumuni ya kuonesha au kuunga mkono kitendo ambacho ni ugaidi kwa mujibu wa Sheria hii.

(4) Kitendo ambacho-
(a) kitavuruga huduma zozote;
(b) kimefanyika kuonyesha kupinga, kudhihirisha au kugoma kufanya kazi,hakitachukuliwa kuwa ni kitendo cha ugaidi kwa mujibu wa kifungu hiki,
ikiwa hakijadhamiriwa kuleta madhara yaliyotajwa katika aya, (a), (b), (c), au (d) ya kifungu kidogo cha (3).

*****Siku ya kesho tutazungumzia makala nyeti sana lakini haitakuwa nje ya sheria, plz naomba suport ya ku share makala hiyo

*JE WAJUA KUPIGA PICHA MAITI AU  MAJERUHI WA AJALI NI KOSA KISHERIA NA UNAWEZA FUNGWA?Kwa mujibu wa kifungu namba 162 ch...
16/07/2020

*JE WAJUA KUPIGA PICHA MAITI AU MAJERUHI WA AJALI NI KOSA KISHERIA NA UNAWEZA FUNGWA?

Kwa mujibu wa kifungu namba 162 cha Sheria ya Kanuni za Adhabu k**a ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 ni kosa kisheria kwa mtu yeyote kupiga picha maiti, watu waliokufa au waathirika wa uhalifu au matukio mabaya k**a vile ajali bila kuwa na kibali cha polisi au chombo chenye mamlaka kisheria.

Sheria hiyo pia inapiga marufuku kusambaza picha hizo kwa njia yeyote ya mawasiliano (ikiwemo mitandao ya kijamii k**a vile Whatsaap, Facebook, Instagram nk) bila kuwa na kibali cha police au chombo chenye mamlaka kisheria.

Mtu yeyote atayevunja sheri hii atakabiliwa na adhabu ya faini isiyopungua Shilingi milioni moja au kifungo cha miezi kumi na miwili (12) au vyote kwa pamoja.

14/07/2020

*KOSA LA JINAI.
Je, wajua kuhusu kosa la jinai, aina na adhabu zake? Basi ungana nasi katika makala yetu..

Kosa la jinai ni tendo lolote ambalo limekatazwa kwa sheria, ambapo mtu yeyote
akilitenda anakuwa ameikosea Jamhuri. Katika makosa ya jinai, mlalamikaji anakuwa ni
Jamhuri, ikiwakilishwa na mwendesha mash*taka wa Serikali. Mtu binafisi aliyedhurika
kwa tendo lakijinai siye anayesh*taki mahak**ani.Yeye anabakia kuwa ni shahidi tu,
nani marachache kwamba Mahak**a inaweza kuagiza kulipwa fidia kwa mtu
aliyedhuriwa na tendo la kijinai.
Katika Makosa ya Jinai, mtu anaye patikana na hatia huadhibiwa, na anayeonekana
hana hatia huachiwa huru.

*ADHABU ZA KOSA LA JINAI
Adhabu za makosa ya Jinai ni pamoja na :kuachiwa kwa
masharti, kifungo cha nje, faini, kifungo gerezani kwa muda maalum, kifungo cha
maisha na kunyongwa hadi kufa.
Makosa ya aina hii ni pamoja na wizi, mauaji, kumiliki silaha kinyume cha sheria,
ubakaji, kutozingatia sheria za barabarani,nk. Makosa yote ya Jinai sharti yawe
ya meandikwa katika sheria mbalimbali. Hatahivyo, kwa nchi ya Tanzania, makosa
mengi ya Jinai yametajwa katika Kanuniya Adhabu (Suraya16yaSheriazaTanzania).
Mtu anayefikishwa mahak**ani kwa kosa la jinai huitwa mtuhumiwa kwa muda wote
baada ya kuk**atwa, kupelekwa kituo cha polisi na hata wakati wa kujitetea
mahak**ani. Akishapatikana na hatia huitwa mhalifu, na akiadhibiwa kwa kifungo
gerezani huitwa mfungwa.

*VITU VINAVYO KAMILISHA KOSA LA JINAI.
Kimsingi, kosa lolote la jinai linakamilishwa na vitu viwili; tendolenyewe lililo katazwa,
na nia ovu ya kutekeleza tendo hilo. Mahak**a inaposikiliza shauri lolote la jinai
hutafuta kujiridhisha iwapo mambo yote hayo mawili yamethibitika kutokea. Katika
mchakato wa kuthibitisha mambo hayo upande wa mash*taka na ule wa utetezi
husikilizwa kwa makini, mashahidi huitwa mahak**ani na wakati mwingine, ikibidi,
vidhibiti mbalimbali huwasilishwa mbele ya mahak**a ilikuthibitisha kwamba kweli
tendo lililo haramishwa lilitokea, na aliyelitenda alifanya hivyo kwa makusudi.
ITAENDELEA....

MIRATHI YA KIISLAMUHii kwa watanzania wote ambao itadhihirika kuwa wameacha mila na desturi zao na ambao Uislamu huwaong...
24/05/2020

MIRATHI YA KIISLAMU

Hii kwa watanzania wote ambao itadhihirika kuwa wameacha mila na desturi zao na ambao Uislamu huwaongoza katika vipengele vyote vya maisha yao ya kila siku, pamoja na watu wengine ambao si wazawa lakini ni waislamu hupaswa kutumia sheria ya kiislamu katika mirathi yao.

NI MUHIMU KUZINGATIA kuwa, katika sheria ya kiislamu, marehemu anaruhusiwa kuacha wosia kwa theluthi moja tu (1/3) ya mali yake kwa amtakaye. Theluthi mbili (2/3) ya mali yake lazima ifuate utaratibu wa sheria za kiislamu yaani irithiwe na warithi wake

MGAWO WA URITHI KATIKA SHERIA YA KIISLAMU ni k**a ifuatavyo;-
1. Mjane /wajane wasiozidi wanne hupata 1/8 ya mali ya marehemu k**a marehemu ameacha watoto. K**a hakuacha watoto wajane watapata ¼ ya mali iliyoachwa na marehemu.
2. Watoto wa kiume 2/3.
3. Watoto wa k**e 1/3.
4. Wazazi / ndugu 1/6 ya salio baada ya kuondoa fungu la mjane/wajane.

NI MUHIMU KUZINGATIA kuwa,
1. Watoto nje ya ndoa hawarithi k**a hawakuhalalishwa wakati marehemu akiwa hai au kuwepo wosia unaowapa urithi.
2. Iwapo mtu si mwislamu haruhusiwi kurithi mali ya mwislamu hata k**a mtu huyo ni mke wa marehemu au watoto

*VIGEZO VINAVYOFIKIWA ILI MTOTO ASIYE NA UMRI WA MTU MZIMA AWEZE KUTOA USHAHIDI MAHAKAMANI .-Kwanza, ni muhimu ithibitik...
03/05/2020

*VIGEZO VINAVYOFIKIWA ILI MTOTO ASIYE NA UMRI WA MTU MZIMA AWEZE KUTOA USHAHIDI MAHAKAMANI .
-Kwanza, ni muhimu ithibitike kwamba mtoto huyo anaelewa maana na uzito wa kula kiapo kabla ya kutoa ushahidi.
-Pili, ni muhimu mahak**a ijiridhishe kwamba mtoto huyo anaelewa vema maswali anayoulizwa wakati wa kutoa ushahidi.

JE, MSHTAKIWA ANAUWEZO WA KUTOA USHAHIDI DHIDI YA MSHTAKIWA MWENZAKE AMBAYE WANASHTAKIWA KWA KUTENDA KOSA KWA PAMOJA?
-Ndiyo, mshtakiwa anauwezo wa kutoa ushahidi dhidi ya mshtakiwa mwenzake katika kosa Hilo hilo ambalo yeye ni mshtakiwa.

JE, KUNA KIGEZO CHOCHOTE CHA KUPIMA UZITO WA USHAHIDI NA UAMINIFU WA SHAHIDI?
-Hapana, hakuna kigezo rasmi kinachotumika kupima uzito wa ushahidi na uaminifu wa ushahidi mahak**ani isipokuwa, ni jukumu la upande ambao unapingana na shahidi huyo kuhoji kwa umakini na kuonesha iwapo shahidi huyo anapaswa kuaminiwa ama la.

*HAKI ZA MTUHUMIWA WAKATI WA KUKAMATWA1. Kumtaka mtu anayemtia nguvuni ajitambulishe kwa jina, cheo, sehemu anayofanyia ...
03/05/2020

*HAKI ZA MTUHUMIWA WAKATI WA KUKAMATWA

1. Kumtaka mtu anayemtia nguvuni ajitambulishe kwa jina, cheo, sehemu anayofanyia kazi na sababu za kumk**ata. Mara nyingi utaratibu umekuwa ni kuonyesha kitambulisho cha kazi

2. Kutumia lugha inayofahamika/kueleweka kwa mtuhumiwa katika kueleza sababu za kutiwa kwake nguvuni.

3. Kutoteswa, kupigwa au kufanyiwa unyanyasaji/udhalilishaji wa aina yeyote wakati akiwa mikononi mwa polisi au mtu aliyemk**ata wakati ametii amri.

4. Kupewa nafasi ya kutoa taarifa kwa mwanasheria wake, ndugu au jamaa zake kuhusiana na kutiwa kwake nguvuni.

5. Kutonyang’anywa/kupokwa kwa mali zake halali wakati wa kutiwa nguvuni au baada ya kutiwa nguvuni.

6. Kupatiwa matibabu au huduma ya kwanza k**a ni mgonjwa au ameumia wakati wa zoezi la uk**ataji.

7. Kupatiwa dhamana toka kwa polisi kabla ya kupelekwa mahak**ani kwa makosa yanayodhaminika.

8.kukaa kimya

Address

Moshi

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Darasa huru la Sheria Mbali Mbali Za Nchi Yetu Tanzania. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Darasa huru la Sheria Mbali Mbali Za Nchi Yetu Tanzania.:

Share

Category