Serengeti Yetu

Serengeti Yetu Serengeti District is located on the Eastern part of Mara region. The District is one of the six District Councils constitute Mara region. Karibuni

Halmashauri Serengeti yaendesha zoezi la chanjo ya Kichaa cha MbwaOfisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ...
22/08/2026

Halmashauri Serengeti yaendesha zoezi la chanjo ya Kichaa cha Mbwa

Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kupitia Idara ya Kilimo na Mifugo kwa kushirikiana na wadau wa Rabies Free Tanzania imeendesha zoezi la utoaji wa chanjo kwa Mbwa na Paka katika eneo la Serengeti Mjini ikiwa ni hatua ya kuzuia na kudhibiti ugonjwa hatari wa kichaa cha mbwa.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo lililofanyika Agosti 22, 2026, Afisa Mifugo wa Halmashauri Bw. Mesiaki Lukumay amesema Halmashauri inalenga kuchanja jumla ya mbwa na paka 45,460 katika Kata zote 30 za Wilaya ya Serengeti. Amesisitiza kuwa chanjo hiyo si tiba kwa mnyama ambaye tayari ameambukizwa kichaa cha Mbwa bali ni kinga dhidi ya ugonjwa huo.

Amesema zoezi hilo ni endelevu kutokana na upatikanaji wa chanjo kupitia Halmashauri pamoja na wadau hatua inayolenga kuhakikisha ugonjwa wa kichaa cha mbwa unatokomezwa katika Wilaya ya Serengeti.

Kwa upande wake Meneja Msaidizi wa Programu ya Rabies Free Tanzania Bw. Machunde Bigambo, amesema hadi sasa jumla ya Mbwa na Paka 11,200 wamechanjwa katika Kata 18, huku akieleza kuwa chanjo hiyo inalenga kuzuia ugonjwa huo kuenea kwa wanyama na hatimaye kuwaambukiza binadamu.

Bw. Machunde amesisitiza kuwa kichaa cha mbwa ni ugonjwa hatari ambao unapotokea huwa hauna tiba. Hivyo amewataka wananchi kuhakikisha Mbwa na Paka wao wanapatiwa chanjo kwa wakati ili kujikinga na ugonjwa huo.

Aidha amewashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kuwaleta Mbwa na Paka wao kwa ajili ya chanjo, pamoja na kuishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kwa ushirikiano mkubwa katika kufanikisha zoezi hilo.

DC SERENGETI AZINDUA  CHANJO YA POLIO AWAMU YA TATUMkuu wa Wilaya ya Serengeti Mhe. Angelina Marco Lubela amezindua kamp...
22/08/2026

DC SERENGETI AZINDUA CHANJO YA POLIO AWAMU YA TATU

Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Mhe. Angelina Marco Lubela amezindua kampeni ya utoaji chanjo ya polio awamu ya tatu huku watoa huduma za afya na wahamasishaji wakitakiwa kutimiza wajibu wao kwa kuhakikisha watoto wote wanaolengwa wanafikiwa na kupata chanjo.

Akizindua zoezi hilo Agosti 21, 2026, amesema zoezi hilo linatarajiwa kufanyika kuanzia Agosti 27 hadi 30, 2026 kwenye Vijiji vyote 78 na Kata zote 30 kwa lengo la kuwafikia watoto wote ambao hawakupata chanjo katika awamu zilizopita kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa chanjo.

“Watoa huduma za afya na wahamasishaji kutoka makundi mbalimbali ya kijamii kila mmoja atimize wajibu wake ili watoto walio chini ya miaka 10 ambao hawajapata chanjo waweze kufikiwa,” amesema Mhe. Lubela.

Muuguzi Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Faustine Nyeura amesema zoezi hilo linafanyika tena mkoani Mara kutokana na kuwepo kwa idadi ya watoto ambao hawakupata chanjo katika awamu zilizopita. Amesema watahakikisha watoto wote wanaostahili wanapatikana na kupewa kinga akisisitiza kuwa polio ni miongoni mwa magonjwa yanayoweza kuzuilika kwa chanjo.

“Tutahakikisha watoto wote wanaostahili kupata chanjo wanapatikana na kupewa kinga katika awamu hii maana polio ni miongoni mwa magonjwa yanayoweza kuzuilika kwa chanjo. Kwa hapa nchini, mgonjwa wa mwisho alipatikana mwaka 1996,” amesema.

Naye Msimamizi wa Taifa wa Zoezi la Chanjo Caster Thobias amesisitiza umuhimu wa kuwafikia watoto katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu ikiwemo stendi,sokoni,kanisani,shule na maeneo mengine. Aidha, amesisitiza maeneo ambayo ni magumu kufikika Wilayani Serengeti kupewa kipaumbele ili kuhakikisha watoto wote wanaostahili wanapata chanjo na kulindwa dhidi ya ugonjwa wa polio.

DED Serengeti awahimiza Watumishi kujiendeleza kielimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Maulid ...
21/08/2026

DED Serengeti awahimiza Watumishi kujiendeleza kielimu

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Maulid Madeni (PhD)akiwa ameambatana na timu ya Utumishi na baadhi ya wataalam wa Halmashauri ameendelea na Clinic ya Kusikiliza na Kutatua Kero za Watumishi katika Kata 10 iliyofanyika Agosti 20,2026 katika Ukumbi wa Serengeti Nuru uliopo Serengeti High School.

Katika clinic hiyo watumishi wamewasilisha kero mbalimbali zikiwemo upandishwaji wa madaraja kwa walimu, madai ya fedha za likizo, kutokupitishwa Kwa wakati majukumu yao kwenye mfumo wa PEPMIS , pamoja na kutolipwa fedha za uhamisho huku baadhi ya kero zikijibiwa papo kwa hapo na keeo nyingine zikichukuliwa kwa ajili ya uchambuzi na ufumbuzi wa majibu sahihi.

Akizungumza katika clinic hiyo Dkt. Madeni amewataka watumishi kutokata tamaa na badala yake kujiendeleza kielimu ili kuongeza uwezo na kuwa na fursa za kushika nafasi mbalimbali serikalini.

“Mwenye Diploma aongeze Degree, mwenye Degree aongeze Masters na mwenye Masters aendelee mpaka PhD. Kesho mnaweza kuwa wabunge, naibu mawaziri na viongozi mbalimbali." amesema Dkt Madeni.

Aidha, amewaelekeza viongozi wakiwemo Watendaji kata Waratibu wa Elimu na Waganga Wafawidhi kusikiliza kero za watumishi na kuziwasilisha Ofisi ya Mkurugenzi kwa ajili ya hatua zaidi. Pia ameagiza kufanyika kwa msawazoi wa walimu ili shule za vijijini zenye upungufu zipatiwe walimu kwa kuzingatia mahitaji.

Clinic hii ni sehemu ya jitihada za serikali katika kuendelea kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili watumishi, ikiwa ni hatua ya kuboresha mazingira na utendaji kazi wao. Zoezi hili linatarajiwa kuwa endelevu katika Kata mbalimbali za Halmashauri ili kuhakikisha kero za watumishi zinasikilizwa na kufanyiwa kazi kwa wakati.

JOSHO LA MIFUGO GENTAMOME KUPUNGUZA CHANGAMOTO KWA WANANCHI.Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mhe. Ayubu ...
15/08/2026

JOSHO LA MIFUGO GENTAMOME KUPUNGUZA CHANGAMOTO KWA WANANCHI.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mhe. Ayubu Mwita Makuruma amesema josho la Gantamome litasaidia wafugaji kupunguza kutembea umbali mrefu Kwa ajili ya kufata huduma hiyo, pia amesema matumizi sahihi ya majosho yatasidia kudhibiti magojwa ya mifugo na kuongeza tija katika sekta hiyo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Agosti 15,2026 katika Kijiji cha Gantamome kilichopo Kata ya Busawe Mhe. Makuruma ambaye pia Diwani wa Kata ya Busawe amesema josho hilo ni miongoni mwa majosho Matano yaliyogharimu jumla ya shilingi milioni 115 ikiwa ni fedha kutoka mapato ya ndani ya Halmashauri.

Mhe. Makuruma ameongeza kuwa ameridhishwa na utekelezaji wa mradi huo uliokamilika kwa asilimia 100 ikiwa ni ahadi aliyokuwa ameitoa Kwa wananchi na pia ameishukuru Serikali na wananchi kwa ushirikiano uliowezesha kukamilika kwa mradi huo.

Kwa upande wake Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Bi. Masinde Nyabibi amewahimiza wananchi kuutunza mradi huo na kusimamia mapato ya josho kwa uwazi ili kusaidia uendeshaji wake ikiwemo ununuzi wa dawa na mahitaji mengine.

Kwa upande wao wananchi wameishukuru Serikali pamoja na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Kwa kuona adha waliyokuwa wakiipita Kwa kipindi Cha muda mrefu na kuwasogezea hukuduma karibu.

WAZIRI WA MIFUGO AZINDUA VYUMBA VIWILI VYA MADARASA SHULE YA MSINGI IGINA, ATOA WITO WA KUENDELEA KUWEKEZA KATIKA ELIMU....
13/08/2026

WAZIRI WA MIFUGO AZINDUA VYUMBA VIWILI VYA MADARASA SHULE YA MSINGI IGINA, ATOA WITO WA KUENDELEA KUWEKEZA KATIKA ELIMU.

Waziri wa Mifugo, Mhe. Balozi Dkt.Bashiru Ally Kakurwa amefanya ziara wilayani Serengeti Agosti 13,2026 na kuzindua vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Msingi Igina vilivyojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 50 ikiwa ni mapato ya ndani ya Halmashauri.

Akizungumza katika hafla hiyo Mhe. Bashiru ameipongeza Halmashauri kwa kuendelea kuwekeza katika sekta ya elimu na kueleza kuwa elimu ndiyo msingi wa maendeleo ya taifa na nguzo muhimu katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

"Matatizo mengi yanayoikabili jamii chanzo chake ni ujinga, na suluhisho lake ni elimu. Tunapaswa kuendelea kuwekeza katika elimu ili kuandaa watoto na vijana waadilifu, wazalendo na wachapakazi watakaolifikisha taifa letu katika maendeleo endelevu." amesema Mhe.Bashiru.

Akizungumza Katika uzinduzi huo amewapongeza walimu nchini kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kufundisha na kulea kizazi cha sasa na kijacho huku akiitaka jamii kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.

Mhe. Bashiru pia amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuboresha miundombinu ya elimu kwa kuhakikisha hakuna upungufu wa madawati, matundu ya vyoo na walimu.Ameelekeza viongozi wa mikoa, wilaya, Halmashauri na shule kuweka mkazo katika kutatua changamoto hizo ili kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto.

Kuhusu uhaba wa walimu Mhe.Waziri amesema Serikali inaendelea na jitihada za kuajiri walimu kadri rasilimali zinavyoruhusu huku akielekeza ajira mpya kuelekezwa zaidi katika shule zenye upungufu mkubwa wa walimu na kusisitiza umuhimu wa kufanya tathmini ya mgawanyo wa walimu ili kuhakikisha kunakuwepo na uwiano unaofaa katika shule zote.

Ziara hii imeonesha dhamira ya Serikali ya kuendelea kuimarisha sekta za elimu, vijana na maendeleo ya jamii kwa ujumla, huku ikisisitiza ushirikiano kati ya Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na wananchi katika kufanikisha maendeleo endelevu.

Karibu Wilayani Serengeti Mhe.Balozi Dkt.Bashiru Ally Kakurwa, Waziri wa Ufugaji na Uvuvi.
12/08/2026

Karibu Wilayani Serengeti Mhe.Balozi Dkt.Bashiru Ally Kakurwa, Waziri wa Ufugaji na Uvuvi.

"Tambua Soko Ongeza Tija, Kutekeleza Dira 2050"
08/08/2026

"Tambua Soko Ongeza Tija, Kutekeleza Dira 2050"

"Tambua Soko Ongeza Tija Kutekeleza Dira ya 2050"
08/08/2026

"Tambua Soko Ongeza Tija Kutekeleza Dira ya 2050"

"Tambua Soko Ongeza Tija Kutekeleza Dira 20250"
08/08/2026

"Tambua Soko Ongeza Tija Kutekeleza Dira 20250"

Matukio mbalimbali Katika picha wakati Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026 ulivyotembelea,kuzindua na kuweka jiwe la msingi Kat...
05/08/2026

Matukio mbalimbali Katika picha wakati Mbio za Mwenge wa Uhuru 2026 ulivyotembelea,kuzindua na kuweka jiwe la msingi Katika miradi Saba ya Maendeleo yenye thamani ya shilingi Bilioni 1.5 Wilayani Serengeti.

Address

P. O BOX 176
Musoma
MARA

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Serengeti Yetu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Serengeti Yetu:

Shortcuts

Share