Panda Miti Kibiashara (Participatory Plantation Forestry Programme-PFP 2) ni programu ya maendeleo inayotekelezwa kwa pamoja kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya Finland kwa makubaliano yaliyofikiwa kati yao mwezi Mei mwaka 2013. Lengo kuu la Programu ya Panda Miti Kibiashara ni kuongeza kipato vijijini kutokana na kupanda miti kitaalamu kwa kutumia mbegu bora na kuhudumia mashamba ya mi
ti ipasavyo kwa kuzingatia mipango ya Matumizi ya Endelevu ya Ardhi
Programu hii ambayo ilianza mwezi Januari mwaka huu inatekelezwa katika wilaya sita za Nyanda za Juu Kusini. Wilaya hizo ambazo ziko katika mikoa ya Njombe, Iringa na Morogoro ni Njombe, Ludewa, Makete, Mufindi, Kilolo na Kilombero. Wadau wakubwa wa Programu hii ni Wizara ya Maliasili na Utalii, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania na Halmashauri za Wilaya zilizoko katika eneo la Programu. Wengine ni Vikundi vya Wakulima wa Miti (Tree Growers Associations - TGAs), Mashirika ya Kimataifa, Asasi zisizo za Serikali, Watu binafsi, Sekta Binafsi, Makampuni binfasi na Taasisi za Elimu na Utafiti. Fursa ya kupata mafanikio ni dhahiri kwa kuwa inakadiriwa kuwa mahitaji ya mazao ya misitu kutoka kwenye mashamba ya miti yaliyopo nchini yanategemewa kuongezeka kutoka mita za ujazo milioni 1.5 na kufikia 3.7 ifikapo 2025. Kitakachosababisha ongezeko hilo ni maendeleo ya kiuchumi nchini Tanzania, ongezeko la idadi ya watu na watu wengi kuhamia mijini. Programu inawahamasisha wananchi waishio vijijini kupanda miti kibiashara ili waitumie fursa hiyo ya ongezeko la mahitaji ya miti kujiongezea kipato. Uwezo wa kufikia lengo kuu la Programu ni mkubwa kwa kuwa katika Nyanda za Juu Kusini kuna udongo unaofaa kukuza miti, mvua za kutosha, ardhi ya kutosha na wakazi wake wanapenda kupanda miti. The Governments of Tanzania and Finland are jointly implementing the Participatory Plantation Forestry Programme (PFP 2) following an agreement made in May 2013. The main goal of the programme is to increase rural income through proper forest management skills, the use of forest quality seeds and taking into consideration sustainable land use planning. The PFP 2 is being implemented in six (6) Districts of the Southern Highland Regions of Njombe, Iringa and Morogoro. The specific Districts include, Njombe, Makete, Ludewa, Mufindi, Kilolo and Kilombero. The implementation started in January 2013
The key stakeholders of the programme are: The Ministry of Natural Resources and Tourism, Tanzania Forest Service Agency and the respective District councils in the Programme area. Other stakeholders are International Organizations, Tree Growers, Non Governmental Organizations, Community Based Organizations, the private sector, research and training institutions. The identified success factor of the programme are that the market demand of forestry products from plantation forests is expected to increase from 1.5 to 3.7 million cubic metres of round wood by the year 2025. During such period Tanzania shall experience more populations increase, improved economy and mass mitigation to towns and cities. The programme encourages the rural population to get involved in commercial tree growing and processing to increase their income since there is great market demand of forest products. It is anticipated that tree growing will be successful in the Southern Highlands due to existing suitable soils, reliable rainfall, available undeveloped land and above all the communities in the industrious people and have demonstrated the traditional of linking trees.