18/07/2026
TAMASHA LA WASANII LAFANYIKA SHELUI KUELEKEA MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU
Tamasha la wasanii limefanyika tarehe 18 Julai, 2026 katika ukumbi wa Wembele, Shelui likiwakutanisha wasanii mbalimbali kutoka ndani ya Wilaya ya Iramba likiwa ni tamasha maalumu la kuelekea mapokezi ya Mwenge wa Uhuru yanayotarajiwa kufanyika tarehe 24 Julai 2026. tamasha hilo lilikuwa jukwaa la kuonesha vipaji vya wasanii wa ndani kupitia muziki, ngoma na maigizo.
Mbali na burudani, tamasha hilo lilitumika kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za mapokezi ya Mwenge wa Uhuru, huku likiendelea kuibua vipaji, kuimarisha mshik**ano wa jamii na kukuza sanaa na utamaduni wa Wilaya ya Iramba.