SIDO Simiyu

SIDO Simiyu Kwa sasa SIDO Simiyu tunatoa huduma zifuatazo:
1. UENDELEZWAJI WA TEKNOLOJIA:
- Ushauri wa kiufundi:

Ndugu wajasiriamali, rafiki zangu na watanzania kwa ujumla nawashukuru sana kwa kufuatilia ukurasa wetu wa SIDO Simiyu. ...
19/06/2020

Ndugu wajasiriamali, rafiki zangu na watanzania kwa ujumla nawashukuru sana kwa kufuatilia ukurasa wetu wa SIDO Simiyu. Endeleeni kutufuatilia na kuwakaribisha pia rafiki zetu ili wapate kujua SIDO inafanya nini na fursa mbalimbali nao pia waweze kufaidi. Tupo kwa ajili yenu. 🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿Asanteni sana.

Hapa chini ni picha ya majengo ya kituo cha mafunzo na uzalishaji (TPC) cha SIDO Simiyu kilichoko Luguru, Wilaya ya Itilima (4km) toka ofisi ya SIDO Mkoa. Kituo hiki kimekarabatiwa kwa msaada wa mamlaka ya Elimu Tanzania- (Tanzania Education Authority), kupitia mfuko wa kuendeleza ujuzi (Skills Development Fund). Kituo hiki kitatumika kutoa mafunzo ya bidhaa za ngozi kwa wajasiriamali wote wa Mkoa wa Simiyu. Mafunzo yataanza mwanzoni mwa mwezi wa Julai na tayari tumesajili washiriki toka wilaya zote za mkoa kwa kushirikiana na uongozi wa halmshari zetu.hata hivyo bado kuna nafasi chache kwa wilaya za Bariadi vijijini, bariadi mjini na Maswa. Hivyo kwa wanaotoka halmashauri hizi na uko kwenye sekta hii au una ndoto ya kujiendeleza kupitia zao la ngozi unakaribishwa kuja kujiandikisha katika ofisi za SIDO Mkoa zilizoko Kidurya, nje kidogo ya mji wa bariadi. Ofisi iko barabarani (Bariadi - Maswa) Kilomita 10 toka Bariadi mjini.

Kuna vyumba vingine vitatumiwa na wajasiriamali kuzalisha, hivyo mnakaribishwa pia kupata eneo kwa ajili ya kuweka viwanda vidogo. Karibuni sana.

30/01/2020

Wakati wa mafunzo hayo, wanawake wajasiriamali wa Mkoa wa Simiyu walijawa na furaha kubwa sana baada ya kujua kwamba SIDO ni kati ya taasisi ambazo zinatoa mada kwenye mafunzo yao. video hii inaonyesha akina mama wakiimba wimbo wa kuelezea SIDO jinsi ilivyo na mtandao nchi nzima wakati wa kumkaribisha Afisa wa SIDO ili atoe mada mojawapo. Ilikuwa ni furaha kubwa sana. Hata hivyo waliomba SIDO iwezeshwe ili iweze kuwafikia wajasiriamali hata vijijini ili kuweza kupeleka ari ya viwanda vijijini.

05/10/2019

Karibuni kwenye maonyesho ya wajasiriamali ya SIDO Taifa yanayofanyika Singida mjini kwenye viwanja vya Bomberdier kuanzia 04/10 hadi 09/1/2010

31/05/2019
Hiki ni kiwanda cha chaki kilichoko Maswa Mkoani Simiyu. SIDO Simiyu ilifanya ziara kiwandani hapo tarehe16/05/2019.
20/05/2019

Hiki ni kiwanda cha chaki kilichoko Maswa Mkoani Simiyu. SIDO Simiyu ilifanya ziara kiwandani hapo tarehe16/05/2019.

23/04/2019
SHIRIKA LA KUHUDUMIA VIWANDA VIDOGO, SIDO             SIMIYUUTANGULIZIShirika la kuhudumia viwanda vidogo, SIDO ni shiri...
23/04/2019

SHIRIKA LA KUHUDUMIA VIWANDA VIDOGO, SIDO SIMIYU
UTANGULIZI
Shirika la kuhudumia viwanda vidogo, SIDO ni shirika la umma lililoanzishwa kwa sheria ya Bunge No.28 ya mwaka 1973. Shirika hili liko chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara na linasimamiwa na bodi ya shirika ambayo huteuliwa na serikali, ambapo mwenyekiti huteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wajumbe wa bodi huteuliwa na Waziri mwenye dhamana na viwanda. Mtendaji Mkuu wa shughuli za kila siku za shirika ni Mkurugenzo Mkuu ambaye anasaidiwa na wakurugenzi wanne k**a ifuatavyo:
1. Mkurugenzi wa Utawala na Fedha
2. Mkurugenzi wa Uendelezwaji Teknolojia na Viwanda
3. Mkurugenzi wa Mafunzo na Tawala za Mikoa
4. Mkurugenzi wa Masoko na Uwekezaji.
SIDO ina ofisi katika kila mkoa wa Tanzania bara na ofisi hizi ziko chini ya Mkurugenzi Mkuu kupitia kwa Mkurugenzi wa mafunzo na tawala za Mikoa.
Kwenye ngazi ya Mikoa kuna watalaam k**a ifuatavyo:
Meneja wa Mkoa ambaye ndiyo msimamizi wa kazi zote, mkoani kwa niaba ya mkurugenzi mkuu.
Chini yake kuna wataalamu k**a ifuatavyo:
i. Afisa Ufundi
ii. Afisa Mwendeleza biashara na mafunzo
iii. Afisa Mikopo
iv. Mhasibu
v. Meneja wa karakana (kwa baadhi ya mikoa)
Ofisi ya SIDO Simiyu imezinduliwa rasmi tarehe 02/01/2018 na Disemba mwaka 2018, SIDO Simiyu ilihamia kwenye jengo lake la ofisi lililoko eneo la viwanda Isanga, mjini Bariadi.

HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA SIDO SIMIYU
1. UENDELEZWAJI WA TEKNOLOJIA:
• Ushauri wa kiufundi: jinsi ya kupata teknolojia na mashine mbalimbali, mpangilio wa jengo la kiwanda na mazingira yake, mahitaji muhimu kwa ajili ya kuanzisha kiwanda, namna ya kuboresha kiwanda chako, uzalishaji wa tija nk.
• Kuwahilisha teknolojia mbalimbali
• Uinjikaji wa mashine (machines installation)
• Kutafuta teknolojia mbalimbali hapa ndani na nje ya nchi na kuifikisha teknolojia hizo kwa wajasiriamali wenye uhitaji
• Kutoa mafunzo za kuzalisha bidhaa mbalimbali: uzalishaji bidhaa za ngozi, kusindika ngozi, usindikaji bidhaa za kilimo, batiki, sabuni na viosheo, mishumaa, chaki nk.
2. UENDELEZWAJI BIASHARA:
• mafunzo ya biashara yanatolewa ili kuwawezesha wajasiriamali kuendesha biashara zao kitaalam: jinsi ya kupata wazo la biashara, jinsi ya kuanza biashara, jinsi ya kuendeleza biashara, uandikaji wa mpango wa biashara, masoko, vyanzo vya mitaji nk.
• Kuunganishwa na taasisi za kihuduma k**a TBS, TFDA, GS1, BRELA nk.
• Uimarishaji vikundi
• Usajili wa majina ya biashara na kampuni na kupata mistari milia (barcodes)
3. HUDUMA ZA MASOKO NA UWEKEZAJI:
• SIDO Simiyu ina eneo la ekari 25 katika eneo la viwanda Isanga, mjini Bariadi na tayari ofisi imejengwa na ipo kwenye hatua za kuanza ujenzi wa majengo kwa ajili viwanda eitha, wajasiriamali wana nafasi pia kuyajenga majengo ya viwanda na kuyatumia kwa muda mpaka warejeshe hela zao na kisha kuendelea kuyatumia kwa kulipa kodi. Wajasiriamali wanakaribishwa kuwekeza kwenye viwanda vya mazao ya kilimo(pamba, alizeti na karanga, mazao ya nafaka, dengu/mbaazi/choroko nk), madini, chuma/bati, vipuri, mashine nk).
• Tunandaa maonyesho ya bidhaa za wajasiriamali wa kitanzania ambapo maonyesho ya kanda ya Ziwa yatafanyika Shinyanga Mei na Maonyesho ya SIDO kitaifa yatafanyika Geita, Octoba.
4. HUDUMA YA KIFEDHA: Tunatoa Mikopo kwa ajili ya biashara ndogo na za kati na kipaumbele chetu ni uzalishaji/viwanda.


KARIBUNI NYOTE KWA HUDUMA ZILIZOTUKUKA

MAWASILIANO:
MENEJA WA SIDO,
MKOA WA SIMIYU,
P.O.BOX 379,
BARIADI
MOBILE:
0754800500 - Meneja SIDO Mkoa
0754093932 - Afisa Ufundi wa SIDO Mkoa
0754315585 - Afisa Mwendeleza Biashara SIDO Mkoa

Ni maonyesho ya ATAPE yaliyofanyika hapa Bariadi kuanzia tarehe 17/04 mpaka 21/04/2019 katika viwanja vya Kusekwa Sekond...
23/04/2019

Ni maonyesho ya ATAPE yaliyofanyika hapa Bariadi kuanzia tarehe 17/04 mpaka 21/04/2019 katika viwanja vya Kusekwa Sekondari. Picha nyingine ni mwonekano wa ofisi ya SIDO Simiyu.

10/03/2019

SIDO Simiyu itaendesha mafunzo ya utengenezaji bidhaa za ngozi (leather crafting) katika majengo yake yaliyoko kata ya Luguru, wilaya ya Itilima. Mafunzo ni ya siku tano kuanzia tarehe 18/03 hadi 22/03/2019.

Address

Isanga
Stone Town
EASTAFRICA

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when SIDO Simiyu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to SIDO Simiyu:

Share