Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga

Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Tunatekeleza kwa vitendo,, Kazi iendelee

Tangazo la Kazi
27/10/2023

Tangazo la Kazi

Halmsahuri ya Manispaa ya Sumbawanga yaishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa mapokezi ya fedha zaidi ya bilioni 12 zina...
25/10/2023

Halmsahuri ya Manispaa ya Sumbawanga yaishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa mapokezi ya fedha zaidi ya bilioni 12 zinazokwenda kuboresha huduma za elimu na afya kwa Wananchi

Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga yaishukuru Serikali kwa mapokezi ya fedha zaidi ya bilioni 12 zinazokwenda kubores...
25/10/2023

Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga yaishukuru Serikali kwa mapokezi ya fedha zaidi ya bilioni 12 zinazokwenda kuboresha huduma za elimu na afya kwa Wananchi.

Halmsahuri ya Manispaa ya Sumbawanga yaishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa mapokezi ya fedha zaidi ya bilioni 12 zina...
25/10/2023

Halmsahuri ya Manispaa ya Sumbawanga yaishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa mapokezi ya fedha zaidi ya bilioni 12 zinazokwenda kuboresha huduma za elimu na afya kwa Wananchi.

Chama cha Mapinduzi (CCM)Wilaya ya Sumbawanga kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga kimeende...
21/10/2023

Chama cha Mapinduzi (CCM)Wilaya ya Sumbawanga kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga kimeendesha Bonanza kubwa la michezo mbalimbali katika Shule ya Sekondari Kizwite.

Bonanza hilo lililohusisha michezo ya kukimbia kwenye magunia, kuvuta kamba, mpira wa pete na mpira wa miguu lilifanyika tarehe 20 Oktoba, 2023 katika viwanja vya Shule ya Sekondari Kizwite kwa kuwakutanisha wanafunzi mashabiki wa Simba na Yanga wasichana na wavulana katika michezo hiyo.

Akizungumza katika hotuba yake ya ufunguzi wa Bonanza hilo lilioitwa Samia Day Bonanza Mgeni Rasmi Comrade Kombat ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kalambo aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alieleza kwamba watoto(wanafunzi) ndio hazina ya Taifa kwenye nyanha zote za maendeleo Nchini ikiwemo michezo hivyo lazima Serikali kupitia kwenye Shule iendelee kujenga misingi ya kuhakikisha wanafunzi wanashiriki kwenye michezo kikamilifu ili kuwaweka sawa kimwili, kujenga mahusiano, kuboresha afya zao na kuendeleza vipaji vyao.

Komba alikishukuru Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia kwa Katibu Mkuu wa Chama hicho Taifa Comrade Chongolo kwa kutoa zawadi ya jezi na kuelekeza kuwepo kwa bonanza na mashindano ya michezo alipotembelea katika Shule hiyo ya Sekondari Kizwite akiwa katika Ziara ya Ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho mwanzoni mwa mwezi Oktoba 2023.

Aidha akizungumza kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi Mkoa Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa Comrade Maufi ambaye alikuwa Mgeni Rasmi mwenza, alieleza umuhimu wa michezo kwa wanafunzi k**a inavyoelezwa kwenye Ilani ya Chama hicho na kuitaka Serikali kuendelea kuboresha miundombinu ya michezo katika Mkoa na kuhakikisha ushiriki wenye tija wa wanafunzi katika Sekta hiyo.

Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imeendesha Mafunzo kwa Watumishi wapya(Watendaji wa Mitaa na Vijiji) 45. Mafunzo h...
11/10/2023

Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga imeendesha Mafunzo kwa Watumishi wapya(Watendaji wa Mitaa na Vijiji) 45. Mafunzo hayo yaliyofanyika tarehe 10 Oktoba, 2023 katika Ukumbi wa Manispaa yaliendeshwa na Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali wa Halmashauri hiyo na yalijikita zaidi katika kusimamia ukusanyaji wa mapato, kufanya kazi kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni, kutatua kero za wananchi kwa wakati n.k

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi. Catherine Mashalla ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika Mafunzo hayo alisisitiza Watendaji hao kufanya kazi kwa upendo na mshik**ano, kuhudumia Wananchi wote kwa usawa bila kujali tofauti zao za kidini, kabila wala vyama vya siasa.

Bi. Mashalla pia alitumia mafunzo hayo kuwaelekeza Watendaji kwenda kusimamia utekelezaji wa miradi ya kisekta katika maeneo yao na kuhakikisha inakamilika kwa wakati na ikiwa na ubora na viwango vilivyowekwa.

29/04/2023
26/04/2023
26/04/2023
26/04/2023
26/04/2023
26/04/2023

Address

Ofisi Ya Mkurugenzi Manispaa, 06 Barabara Ya Mkoani, S. L. P 187, 55182 Sumbawanga
Sumbawanga
RUKWA

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 21:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 07:30 - 21:30
Friday 07:30 - 15:30

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga:

Shortcuts

Share