Clement Mdiu

Clement Mdiu Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Clement Mdiu, 100 Kasulu, Sumbawanga.

THAMANI ya mwanadamu ni ndogo sana imeambatanishwa kwenye pumzi,na hii pumzi kazi yake kwa mwanadamu huwa ni kumpeleleza...
24/12/2018

THAMANI ya mwanadamu ni ndogo sana imeambatanishwa kwenye pumzi,na hii pumzi kazi yake kwa mwanadamu huwa ni kumpeleleza kwa kila TENDO jema ama baya analolitenda hii ikiwa ni kwa siri ama kwa uwazi!...
Hebu leo tena tuujue huu ukweli ninaokuletea online kwenye madhabahu huru ya FOCOAA2™.
Tupate PICHA ya ukweli wenyewe Hapa...Mithali 20:29"pumzi ya mwanadamu ni taa ya BWANA; Hupeleleza yote yaliyomo ndani yake."

+

Waebrania 4:13"wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake,lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu".
Mwenye kuzijua siri za mwanadamu kwa hali zote ni MUNGU tu peke yake kwa sababu yeye ndiye mwenye dhamana ya uhai wa mwanadamu!

Siri zote huitwa siri zikiwa pa mwanadamu lakini siri huwa si siri zikiwa mbele za MUNGU ambapo huitwa "utupu".
Maana ya utupu kwa lugha yakinifu ni "kuwa WAZI".

Kazio la kuwa wazi mbele za MUNGU ni hili hapa ...Mithali 15:3"Macho ya BWANA yako kila mahali; Yakimchunguza na ."
Haya ndiyo mambo murua ninayoyaweka wazi bila hata kuogopa cho chote!
Namaliza kwa kukiri hivi ..siri ni yako ila mbele za Mungu inaitwa ni utupu...
Na palipogemwa na mgema pameliwa na dumunzi.
Asanteni!
©Rev.Mdiujr® FOCOAA2™.

NAOMBENI KUKIWASILISHA KIPAWA CHA SIRI CHA MUNGU NDANI YANGU KWA USIKU HUUKUTOKA KONA ZA FOCOAA2™"Ukiona unaungwa mkono ...
03/01/2018

NAOMBENI KUKIWASILISHA KIPAWA CHA SIRI CHA MUNGU NDANI YANGU KWA USIKU HUU
KUTOKA KONA ZA FOCOAA2™
"Ukiona unaungwa mkono na WATU wengi wasiokufahamu SURA YAKO WALA MAKAZI YAKO wala usiowafahamu wewe TAMBUA wazi kuwa ndani yako kuna UTAJIRI mwingi sana wa ki-MUNGU uliomo ndani yako unaowafanya washawishike wawe wafuasi kwa HIARI zao wenyewe,Na ndiyo kusema hawawi tu wafuasi wako bali wananufaika na hekima iliyomo tayari ndani yako".
KILA SIKU WANAJIFUNZA KILE UNACHOKIANDIKA HUKO NDIKO KI-MUNGU!
UWEPO WAKO NI FAIDA KWA WATU WENGINE!
HIVYO ACHA KUKATA TAMAA ,HEBU SONGA MBELE KUNA WATU NYUMA YAKO WANAJIFUNZA MAMBO MAPYA KUTOKA KWAKO, AMBAYO UNAWAWEZESHA KUPIGA HATUA KILA SIKU NA MAISHA KWAO YANAONEKANA KUWA YA MAANA KWA SABABU TU YA UWEPO WAKO!
2018 FANYA ZAIDI NA KUWA MBUNIFU KUWEZESHA WENGINE KUISHI KIAMANI ZAIDI!. ASANTENI.
"*©Rev.Mdiujr®, FOCOAA2™**

Endelea kumcha Mungu! Epukana na kiburi cha KUWADHARAU watu walio hai!kumbuka maisha yako siri yake ipo kwa watu hao hao...
07/08/2017

Endelea kumcha Mungu! Epukana na kiburi cha KUWADHARAU watu walio hai!kumbuka maisha yako siri yake ipo kwa watu hao hao unaowadharau wewe kwa kuwaita kwa kigezo yakuwa hawajasoma au hata kuwanenea yakuwa ni washamba! Duuh hebu uwe unajichelewesha kutamka chochote unachokielewa au hata kutokielewa usiwe wa kwanza kutoa majibu ya mambo ya wengine!
***®ev.Mdiujr, FOCOAA2***

"UKIMTUMAINI MUNGU  ATAZIDI KUWA NA WEWE, NAWE UTAZIDI  KUFANIKIWA SANA".DAUDI alitumaini sana Mungu katika harakati za ...
06/07/2017

"UKIMTUMAINI MUNGU ATAZIDI KUWA NA WEWE, NAWE UTAZIDI KUFANIKIWA SANA".
DAUDI alitumaini sana Mungu katika harakati za maisha yake chini ya jua;ndivyo na sisi tunapaswa kumtumainia Mungu katika harakati za maisha yetu hapa chini ya jua!
Soma hapa:1 Mambo ya Nyakati 11:9"Naye Daudi akaendelea, akazidi kuwa mkuu; kwa maana BWANA wa majeshi alikuwa pamoja naye".
Ili uweze kufanikiwa ni sharti uwe na sifa hii"BWANA wa majeshi awe pamoja nawe kwa kila jambo unalolifanya muda wowote ule"…
Na unapokuwa na UHAKIKA huu ya kuwa Mungu yuko pamojanawe hali ya kuinuliwa na MUNGU ni jambo dogo mbele zake!
Rejea:Yusufu jinsi alivyokuwa pamoja na Mungu na kufanikiwa mambo yote bila vikwazo ,
Mwanzo 39:23"Wala mkuu wa gereza hakuangalia neno lililoko mkononi nwa Yusufu;kwa kuwa BWANA alikuwa pamoja naye. BWANA akayafanikisha yote aliyoyafanya".
Mambo yote unayoyakusudia kuyafanya ukimtumainia Mungu hakika yote atayawesha tu!
Jambo la maana ni kuendelea kumtafuta Mungu na kumtumikia atatuwezesha yote! Amini hivyo!
Asanteni sana kwa USHIRIKIANO wenu mwema katika kuendelea kulisoma Neno la MUNGU katika kona hii ya FOCOAA2.
**FOCOAA2, Rev.Mdiujr***

Endelea  kubarikiwa mno mtu wa Mungu!
28/06/2017

Endelea kubarikiwa mno mtu wa Mungu!

Asante  hata kwa kusoma!
28/05/2017

Asante hata kwa kusoma!

Endeleeni kubarikiwa
27/05/2017

Endeleeni kubarikiwa

04/05/2017

Usiku mwanana!
**Rev.Mdiujr, FOCOAA2***

Ni wakati wa **FOCOAA2 Ministry**.Karibu katika mwza ya Neno la MUNGU, ikiwa watu wanakaribishana vyakula mbalimbali amb...
16/04/2017

Ni wakati wa **FOCOAA2 Ministry**.
Karibu katika mwza ya Neno la MUNGU, ikiwa watu wanakaribishana vyakula mbalimbali ambavyo watakula na kusahau K**a walikula vyakula husika!
Somo kuu:Mambo sita (6) anayoyachukia BWANA.
Kiukweli kuna watu hujisahau kabisa na wala hawajui k**a wanafanya machukizo mbele ya Mungu hasa juu ya Yale wanayoyafanya kila iitwapo leo,rejea Mithali 6: 16,17"kuna vitu sita anavyovichukia BWANA,Naam Viko saba vilivyo chukizo kwake.Macho ya kiburi, ulimi wa uongo, Na mikono imwagayo damu isiyo na hatia;Moyo uwazao mawazo mabaya; Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu; Shahidi wa uongo asemaye uongo; Naye apandaye mbegu za fitina kati ya ndugu.
Kwa ujumla haya ndiyo mambo sita (6) yalitajwa katika mithali na ambayo pia yanayasumbua maisha yetu hapa chini ya jua K**a vile:-
-macho ya kiburi,
-ulimi usemao uongo,
-mikono imwagayo damu isiyo na hatia,
-Moyo uwazao mawazo mabaya,
-Shahidi wa uongo asemaye uongo,
-mtu anayepanda mbegu za fitina kati ya ndugu.
Haya ndiyo mambo sita asiyoyapenda MUNGU ambayo ndiyo mambo wanaoyafanya wanadamu huku mioyoni mwao wakijipiga vifua ya kuwa wanampenda MUNGU lakini bado nafsi zao zikiwa bado gizani! Asanteni, nawatakieni tafakuri murua!**FOCOAA2 Ministry**,Rev.mdiujr

15/04/2017

Address

100 Kasulu
Sumbawanga

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Clement Mdiu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share