21/08/2024
NGASSA CUP YAENDELEA KATA YA ITUNDURU
Mashindano ya 'NGASSA CUP' yanayodhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Igunga Mh. Nicholaus George Ngassa yameendelea leo tarehe 21/08/2024 katika Kata ya Itunduru.
Wananchi waliojitokeza kwa wingi wameshuhudia mechi ya nusu fainali ya kwanza, iliyozikutanisha timu ya Kijiji cha Kagongwa dhidi ya timu ya Kijiji cha Mibuyumiwili katika uwanja wa Shule ya Msingi Itunduru. Hadi dakika 90 zinahitimishwa na mwamuzi, timu ya Kijiji cha Kagongwa imeibuka na ushindi wa goli 1 - 0 dhidi ya ya timu ya Kijiji cha Mibuyumiwili.
Mashindano hayo yataendelea kesho tarehe 22/08/2024 ambapo kutakuwa na mechi ya nusu fainali ya pili, mechi hiyo kali na inayosubiriwa kwa shauku itazikutanisha timu ya Kijiji cha Itunduru dhidi ya timu ya Kijiji cha Mwabalaturu. Mechi itacheza kuanzia saa 10:00 Jioni katika Uwanja wa Shule ya Msingi Itunduru.