20/08/2026
20/08/2026 Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO), Dkt. Petro Mboya amefungua mafunzo ya maoteo ya dawa na vifaa tiba yaliyofanyika katika Ukumbi Mkubwa wa Mikutano, Makao Makuu ya Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi
Mafunzo hayo yamewashirikisha Waganga Wafawidhi na Wafamasia kutoka vituo 51 vya kutolea huduma za afya katika Wilaya ya Kilindi, kwa lengo la kuwajengea uwezo katika kufanya maoteo sahihi ya mahitaji ya dawa na vifaa tiba.
Akifungua mafunzo hayo, Dkt. Mboya amesisitiza umuhimu wa kufanya maoteo sahihi kwa kuzingatia mahitaji halisi ya vituo vya afya, ili kuhakikisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa wakati na kuendelea kuboresha huduma za afya kwa wananchi.
Mafunzo haya ni sehemu ya jitihada za kuimarisha usimamizi wa dawa na vifaa tiba katika vituo vya afya na kuhakikisha wananchi wa Wilaya ya Kilindi wanapata huduma bora za afya.