01/09/2022
SOKO LA MAKTABA KIMTANDAO
MUHTASARI
Uuzwaji wa huduma za maktaba kwa watumiaji wake niswala ambalo bado nichanga sana nchini kwetu hususan katika utumiaji sahihi wa mitandao ya kijamii. Hii nikutokana na muamko mdogo na taaluma ndogo za wakutubi katika kutangaza huduma zao kwa jamii. Makala hii itakwenda kuangalia juu ya utumiaji wa mitandao ya kijamii katika kutangaza huduma za maktaba. Makala hii aidha itaangaza zaidi katika aina za mitandao ya kijamii , utumiaji sahihi wa mitandandao ya kijamii na changamoto za utumiaji mitandao ya kijamii inayotumika kutangaza soko la huduma za maktaba
DHANA YA MITANDAO YA KIJAMII MAKTABA
Maktaba inasemekana kua na umuhimu mkubwa kwa wanafunzi na watu wote ulimwenguni wenye kuhitaji taarifa na taaluma mbali mbali kwani maktaba imekusanya idadi kubwa ya machapisho ambayo ndio vyanzo vya taarifa ikiwemo vitabu majarida magazeti makamusi ramani na hata vipeperushi. Kwamujibu wa Fakas (2007) Maktaba ni mkusanyiko wa nyenzo, vitabu au vyombo vya habari vinavyofikika kwa urahisi kwa matumizi na si kwa madhumuni ya kuonyesha tu. Maktaba Inawajibu wa kutoa habari sahihi zilizochapishwa ili kukidhi mahitaji ya mtumiaji kila siku. Machapisho hayo yote hukusanywa kutoka kwa wanasayansi na hata wanasanaa kutoka sehemu tofauti ulimwenguni wenye lengo kubwa la kusaidia watu mbali mbali wakiwmo watafiti, madaktari, wabunge na hata wanafunzi wa vyuo na skuli.
Uuzwaji wa huduma za maktaba zimekua zikikosa soko maridadi licha yakua ndio kichwa kikuu cha habari katika tafiti za wasomi wengi wa mambo ya ukutubi na masomo ya habari. Kwaupande mwengine bado wakutubi wameegemea zaidi katika kutangaza huduma zao kizamani hali hii inapelekea badhi ya huduma watowazo kushindwa kutambulikana na watumiaji wake.
Bila shaka machapisho yote yanopatikana maktaba lazima yanahitajika kutangazwa ili yaweze kujulikana na watumiaji wao wote. Soko la utangazwaji wa machapisho hayo yote ya maktaba yanahitaji utaalamu mkubwa sana la utangazaji kwa watumiaji wake wote.
Ni dhahiri kwamba Wakutubi wanaweza kutumia majukwaa ya mitandao ya kijamii kusambaza huduma zao za Maktaba kwa sababu wanafunzi wengi na watumiaji wa maktaba wanatumia mitandao ya kijamii kila wakati kuwasiliana, kujifunza au kushiriki maarifa na marafiki au familia zao. kwamujibu wa Fakas (2007) amesema kwamba mitandao ya kijamii k**a jukwaa la mtandao linaloruhusu watumiaji kufanya maingiliano ya kijamii, kushiriki na kushiriki katika mawasiliano. Kwa hiyo, mitandao ya kijamii inaruhusu watumiaji kuingiliana, kuwasiliana na kushiriki aina tofauti za yaliyomo k**a vile picha, picha, ujumbe, video, sauti kwa kutaja machache tu, kwenye mtandao. Fakas (2007) ameengeza kwamba Uuzaji wa huduma za maktaba kwenye mitandao ya kijamii ni njia sahihi ya maktaba kutangaza, bidhaa na huduma zake za machapisho kupitia teknolojia za mtandao 2.0. Kwa kutumia maktaba za mitandao ya kijamii zinaweza kushirikiana na wateja wao na kuwawezesha kushiriki katika utengenezaji wa bidhaa za maktaba.
AINA ZA MITANDAO YA KIJAMII INOTUMIKA MAKTABA
Katika kutambua umihimu wa mitandao ya kijamii nadani ya maktaba zifuatazo ni aina za mitandao ya kijamii inayopatikana vizuri na kutumika kwa kubadilishana maarifa juu ya kujifunza namna ya kutoa huduma za maktaba na kusambaza taarifa na taaluma kwa kutumia rasilimali za TEHAMA.
BLOGU
Blogu pia inajulikana k**a Weblog ambayo ni mtindo wa jarida la mtandaoni au tovuti ya habari ambayo huonyesha maelezo kwa mpangilio wa kimatukio, huku machapisho au mada ya hivi punde ikionekana kwanza au juu kabisa. Aidha Kurasa za blogu ni majukwaa ya wavuti ya mitandao ya kijamii ambapo mwandishi au kikundi cha waandishi na wasomaji au watazamaji hushiriki maoni yao kuhusu somo au mada hata habari kadri itakavyotumika, Ekoja 2011) Blogi pia inaweza kutumika katika kukuza huduma za maktaba k**a vile uhamasishaji wa utumiaji maktaba, usambazaji habari, kutoa taswira ya jengo la maktaba , kuwasiliana na watumiaji wake wa ndani na nje ya maktaba, na kutangaza juu ya kuwasili kwa nyenzo mpya na kukuza ujuaji wa nyenzo zinazopatikana kwenye mkusanyiko wa maktaba . Pia Wasimamizi wa maktaba wanaweza kukuza huduma za maktaba k**a vile saa za ufunguzi, matukio maalum ya maktaba, majadiliano ya mtandaoni juu ya mada iliyo orodheshwa na pia kutangaza matukio yanofanyika makataba k**a vile sherehe katika eneo lao jamii, sherehe, michezo, (Ekoja, 2011).
FACEBOOK
Facebook ni jukwaa la mitandao ya kijamii ambalo huwezesha mwingiliano wa kijamii kati ya watumiaji. Facebook huruhusu watumiaji kuunda kikundi chenye utambulisho wa kipekee ambapo wanachama wanaweza kuingiliana na kushiriki ujumbe, picha na hata nyenzo walipoingia. Wahudumu wa maktaba wanaweza kutumia Facebook kukuza huduma ya Maktaba k**a vile kukaribisha ukurasa wa nyumbani wa maktaba (Fakas, 2007), kutangaza saa za kufungua na kufunga maktaba, maeneo yanayotoa huduma za makataba, habari za tovuti ya maktaba, nyenzo mpya zilizopatikana na mwingiliano wa wanafunzi wa darasa katika majadiliano juu ya masomo maalum.Ukurasa wa Facebook unaweza kutumika k**a kituo cha kuunganisha kwa watumiaji wake wa maktaba na wasimamizi wa maktaba wanaweza pia kumkumbusha mtumiaji kupitia uchapishaji wa habari zilizochapishwa na picha zenye ujumbe ujumbe na picha za rasilimali zinazopatikana kwenye maktaba.
WHATSAPP
WhatsApp pia ni moja katika majukwaa ya mitandao ya kijamii yenye ujumbe wa bure papo hapo na sauti juu huduma za simu. Ujumbe wa maandishi wa papo hapo, simu za sauti, simu za video, hati na huduma za kutuma media zote zinapatikana kwenye jukwaa hili (Fakas, 2007) Wasimamizi wa maktaba wanaweza kutuma ujumbe papo hapo kwa watumiaji na kupata majibu ya papo hapo kwa haraka juu ya habari ambayo inahitaji uangalizi wa watumiaji wa Maktaba pia inaweza kuwasilishwa kwa watumiaji, hata vyanzo vya taarifa na nyenzo zinaweza kutumwa kwa watumiaji wakati wowote na hata nje ya Maktaba saa za kazi.
TWITTER
Hii ni programu ndogo ya kublogi, kuweka wafanyikazi na wafadhili kusasishwa juu ya shughuli za kila siku, k**a mikusanyiko inayosasishwa mara kwa mara. Watumiaji wanaweza kutumia jukwaa hili kuandika kwa ufupi ujumbe au sasisho la hali.Twitter ni mtandao wa habari za wakati halisi na jukwaa la mitandao ya kijamii ambapo watumiaji huchapisha na kuingiliana na ujumbe. Urahisi wa kuchapisha, kuingiliana na kushiriki habari juu ya jukwaa hili limeifanya kuwa jukwaa muhimu sana kwa wasimamizi wa maktaba kufikia na kuingiliana nao watumiaji wa maktaba (Waddell na Barnes, 2012). Taarifa juu ya kwenda na majibu ya watumiaji unaweza kutweet kwa urahisi wa kila mtu.
LINKEDIN
Wasimamizi wa maktaba wanaweza kupata wateja waliounganishwa na wataalamu katika uwanja wao mahususi unaowavutia kupitia LinkedIn. Wasimamizi wa maktaba wanaweza kutumia jukwaa hili kutoa huduma maalum k**a vile Usambazaji Mkakati wa Taarifa (SDI). Waddell na Barnes, (2012) aliongeza kuwa Katika maktaba zimechukua fursa ya tovuti hii kuchapisha, kalenda, zana za utafutaji za katalogi, na vipengele vya blogu ili wanafunzi kuboresha uwepo wao.
MATUMIZI YA MITANDAO YA KIJAMII KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA MAKTABA
Kuwezesha Mawasiliano ya Njia Mbili yenye ufanisi kwa watumiaji wake wa maktaba
Majukwaa ya mitandao ya kijamii huunda jukwaa zuri la maoni kutoka kwa watumiaji wa Maktaba na Wasimamizi wa maktaba wanaweza kuathiri vyema watumiaji wao wanapopata majibu kutoka kwao juu ya huduma na matumizi ya maktaba. Villodo, (2012).ameongeza kua Mitandao ya kijamii husaidia wasimamizi wa maktaba kufuatilia maoni ya watumiaji wa maktaba na kutoa ufafanuzi kuhusu masuala yoyote yanayowahusu.
Mitandao ya kijamii pia hutumika katika kuongeza Watumiaji na Matumizi mazuri ya Maktaba
Maktaba sasa iko mwenyeji kwenye Facebook, shughuli za mtumiaji yeyote kwenye kurasa za maktaba zinaweza kutazamwa na hata kutembelewa na marafiki waliounganishwa na mtumiaji huyo. Wakati wowote mtumiaji wa Maktaba anapotoa maoni au chapisha kwenye kurasa za maktaba, watu wengine waliounganishwa na mtumiaji huyo wataona na kujua shughuli na huduma zinazotolewa na Maktaba na hii inaweza kuwahamasisha wengine wajiunge na watumiaji wa Maktaba. Pierson, (2011) amesisitiza kua Maoni na machapisho ya kublogi na kutwiti yanaweza pia kutangazwa mtandaoni na zote mbili Watumiaji wa maktaba na mtumiaji mwingine yeyote wa mtandao anayetaka huduma zinazotolewa na Maktaba inaweza kutazama.
Mitandao ya kijamii pia hutumika katika kuokoa Gharama ya utangazwaji wa huduma za maktaba
Gharama ya kujiandikisha na kuwezesha majukwaa ya mitandao ya kijamii ni ya chini kabisa na muda mwengine ni bure kabisa Villoldo, (2012) amesema kwamba gharama ya usajili wa maktaba katika mitandao ya kijamii ni ndogo sana hivyo wakutubi wanaweza kukuza huduma za Maktaba kwa kutumia majukwaa ya mitandao ya kijamii na pia inaweza kufikia watumiaji wao na mamilioni ya yaliyokusudiwa na watumiaji watarajiwa ndani ya kundi la karibu na ndani ya dunia.
Mitandao ya kijamii pia hutumika katika Kuunda vikundi vya majadiliano baina ya wakutubi na watumiaji wake
wanafunzi wengi na wakufunzi wao huunda vikundi ambamo wanafanya majadiliano, kukutana na kushiriki habari kuhusu chuo kikuu.kwani wengi wao huufanya majadiliano na kupitia karatasi za mitihani iliyopita lakini pia wakufunzi wao hutumia mitandao ya kijamii ili waweze kutuma mada zao walizosomesha darasani.
CHANGAMOTO ZA UTUMIAJI WA MITANDAO YA KIJAMII MAKTABA
Kwaupande mwengine maktaba bado inakabiliwa na changamoto kubwa ya utumiaji wa mitandao ya kijamii ili kufikisha taarifa na huduma zake kwa watumiaji wake, hivyo zifuatazo ni changamoto ambazo huikumbumba maktaba katika kutumia mitandao ya kijamii.
Kukosekana kwa wataalamu wa kompyuta maktaba.
Hii nicnhagamoto kubwa inayoikumba maktaba katika kutumia mitandao ya kijamii hususan wanapotaka kubadilisha taarifa kutoka mfumo wa zamani kuja mfumo wasasa kwani huduma za kubadilisha na kuweka dijiti na rasilimali zinahitaji maarifa mengi juu ya kutumia kompyuta hivyo ikiwa kuna ukosefu wa utaalamu katika kompyuta kazi haitafanyika. Hata hivyo, Villoldo, (2012) amependekeza suluhisho la changamoto hii kwa msemo rahisi kwamba maktaba ya kitaaluma inapaswa kuajiri utaalam watafanya vizuri kusimamia na kudhibiti mfumo wa kompyuta kwa kutumia programu na mfumo wa kompyuta.
Ukosefu wa fedha kwa ajili ya teknolojia mpya
Upungufu wa fedha katika kutafuta teknolojia mpya ni changamoto inayokabili maktaba katika kutumia mitandao ya kijamii nakupelekea kushindwa kufikia hadhira wingi. Hii ni kwa sababu kupata teknolojia mpya kunahitaji kuwa na pesa nyingi ili kushughulikia kikamilifu mfumo wa kusambaza huduma kwa hadhira.
Ukosefu wa taaluma ya kusimamia na kuhifadhi kumbu kumbu za kielektronia
Ukweli nikwamba wakutubi wengi hawana taaluma yeyote ya kutumia mitandao ya kijamii kwenye kusambaza na kuhifadhi habari zao ndio mana wanashindwa kutumia ipaswavyo licha yakuwepo kwa mitandao hiyo katika ofisi zao na zinapatikana bure.
HITIMISHO
Bakare (2018) ameeleza kwamba katika utumiaji wa jukwaa la mitandao ya kijamiiunaweza kusimamia utoaji sahihi wa taarifa hususan katika kutangaza huduma za maktaba kwa watumiaji wake hali hii inapeleke zaidi kuvutia watumiaji na kuengeza taaluma ya kutambua juu ya huduma zitolewazo maktaba kwa watu wake kwani wakutubi wanapata nafasi ya kutangaza ulimwengu mzima juu ya vyanzo vya habari ambavyo vinaweza kutafutwa na kutumiwa pahali popote na muda wowote. Hii inaonsha kwamba mitandao ya kijamii nimuhimu sana ndani ya makataba katika kutangaza huduma zake kwa watumiaji wake hivyo wakutubi na watumiaji wake wanalazimika kuhama katika mfumo wa zamani kuja katika mfumo wa kisasa.
MAREJEO
Ekoja, I.I. (2011). Modern ICT Tools: Online Electronic Resources Sharing using Web 2.0 and its implications for library and information practice in Nigeria. Samara Journal of Information Studies, 11(1&2), 53 –58.
Fakas, M. (2007). Going where patrons are. American Libraries, 38(4), 27 – 32. Retrieved 24TH june,2011 from http://www.ebscohost.com from http://www.itc.conversationnetworking.
Villodo, M.A. (2012). How to mobilize your library at low cost. Liber Quarterly; the Journal of the Association of European Research Libraries, 22(2).