Mbunge Maulid Jimbo la Welezo

Mbunge Maulid Jimbo la Welezo Welezo kwanza

14/03/2024

Nimezifariji familia 4
zinazoishi katika Nyumba Moja inayomilikiwa na Bwana Ali Mohd
iliyoungua moto na kusababisha hasara kubwa ya vitu mbalimbali
kuunga na moto. na nimeziomba kuwa na subra katika kipindi hiki kigumu na watahakikisha uongozi wa Jimbo hilo Wanaka pamoja ili kuwapatia Msaada wa kupunguza ukali wa athari hiyo kubwa walioipata.

ajanga ya kuunguliwa na moto yanaweza kumpata mtu
yoyote hivyo ni vyema kwa jamii kuendelea kushirikiana katika kutoaCmsaada pale pale inapotokea sambamba na wananchi
kuzikatia bima nyumba zao ili kuweza kupata nafuu ya athari pale
inapotokea majanga moto.

Nimetoa mitungi ya Gesi kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Jimbo la Welezo ambazo nimepanga kuzigawa kwa...
10/03/2024

Nimetoa mitungi ya Gesi kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Jimbo la Welezo ambazo nimepanga kuzigawa kwa makundi mbalimbali ya wananchi kwa lengo kushajihisha wananchi kutumia nishati hiyo ya gesi .

Nimeshiriki kikao cha Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapindunzi Jimbo la Welezo  ambapo pia kulifanyika ugawaji wa kadi za Ki...
10/03/2024

Nimeshiriki kikao cha Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapindunzi Jimbo la Welezo ambapo pia kulifanyika ugawaji wa kadi za Kielektoniki za Chama cha Mapinduzi wa wanachama CCM wa matawi mbali mbali katika Jimbo hilo

Wananchi wa Wadi ya Welezo wametakiwa kumpigia kura mgombea wa Chama cha Mapindunzi CCM katika Uchaguzi mdogo wa Wadi ya...
16/10/2023

Wananchi wa Wadi ya Welezo wametakiwa kumpigia kura mgombea wa Chama cha Mapindunzi CCM katika Uchaguzi mdogo wa Wadi ya Welezo unaotarajiwa kufanyika Octobar 28 mwaka huu.

Hayo yameelezwa na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa NEC Amin Salmin Amour Juma wakati akizindua kampeni ya uchaguzi mdogo wa kiti cha udiwani wadi ya welezo katika viwanja vya Stella daraja Bovu.

Amesema Chama cha Mapindunzi kina kila sababu ya kushinda nafasi hiyo ya udiwani hivyo amewataka Wanachama wa CCM kujitokeze kwa wingi siku ya tarehe 28 Octoba kupiga kura ili kuipa ushindi ccm na kuendeleza utekelezaji wa ilani yake katika kuleta maendeleo kwa wananchi…

Viongozi mbalimbali wa CCM wamemuombwa kura za ndio mgombea huyo ili aweze kushinda nafasi hiyo na kuweza kushirikiana na viongozi wa CCM wa Jimbo hilo la Welezo katika kuwaletea maendeleo wananchi.

Akiomba kura za ndio Mgombea nafasi ya Udiwani kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abrahman Khamis Shabani amewaomba wananchi wa wadi hiyo kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 28 kwa kumchagua Ili aweze kuendelea kuwatumikia katika kuleta maendeleo

Hatua hiyo ya kufanyika Uchaguzi huo mdogo wadi ya Welezo imekuja kufuatia Diwani wa Chama cha Mapinduzi wadi hiyo kufariki Dunia

Katika hatua Nyengine Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa NEC Amin Salmin Amour Juma amepokea kadi 4 za Wananchama wa Chama cha ACT Wazalendo ambao wamehama chama hicho na kuhamia Chama cha Mapinduzi CCM .

16/10/2023

Vijana wanne warudisha kadi za ACT na kuhamia CCM katika Uzinduzi wa kampeni uchaguzi mdogo wadi ya Welezo

16/10/2023
“ Nimekabidhi mipira ya maji  kwa Wakaazi  wa Mtopepo Chem chem kwa lengo la kusogeza huduma ya maji safi na Salam ya ZA...
14/10/2023

“ Nimekabidhi mipira ya maji kwa Wakaazi wa Mtopepo Chem chem kwa lengo la kusogeza huduma ya maji safi na Salam ya ZAWA Katika maeneo yao wanayoishi ”

Wakaazi wa Mtopepo Chem chem wamemshukuru mbunge wa jimbo la Welezo kwa kuwapatia mipira ya Maji kwa ajili ya kusogeza huduma ya maji safi na Salama katika maeneo ya karibu na nyumba zao.
Wakizungumza mara baada ya kukabidhiwa mipira hiyo wananchi wanaoishi katika maeneo hayo Abdalla Saleh Othman na Tatu Kassim Silima wamesema kwa kipindi kirefu wamekosa huduma ya maji safi na Salama kutoka Zawa, hivyo kupatiwa kwa mipira hiyo kutasaidia huduma hiyo kuwafikia karibu na kuweza kuunga katika nyumba zao.

Wananchi hao wameelezea jitihada zinazochukuliwa na mbunge wa Jimbo la welezo ikiwemo kushirikiana katika kuwasogezea huduma ya umeme ambayo tayari imeshapatikana sambamba na kumuomba kuendelea kuwatatulia matitizo ambayo bado yamekuwa kikwazo kwa wananchi hao ikiwemo tatizo la kukosekana kwa kituo cha afya katika maeneo ya karibu.

Mbunge wa Jimbo la Welezo Mhe. Maulid Saleh Ali amesema ataendelea kushirikiana na wakaazi wa maeneo hayo katika kuhakikishasha wanayapatia ufumbuzi matatizo yanayowakabili ,sambamba na kuwasihi wananchi kuitunza miundo mbinu ya mipira hiyo pamoja na kujisajili katika mamlaka ya maji Zawa ili waweze kuungiwa huduma hiyo ya maji katika nyumba zao

Zaidi ya Shilingi Milioni nne Zimetumika katika kununulia Mipira hiyo ya Maji fedha ambazo zimetokana na Mfuko wa Jimbo hilo la Welezo.

Address

WELEZO
Zanzibar City

Telephone

+255679681321

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mbunge Maulid Jimbo la Welezo posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Mbunge Maulid Jimbo la Welezo:

Share