Maendeleo ya Vijana Zanzibar

Maendeleo ya Vijana Zanzibar Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Maendeleo ya Vijana Zanzibar, Social service, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar/Migombani Zanzibar, Zanzibar.

Idara ya Maendeleo ya Vijana Zanzibar imedhamiria kuimarisha uratibu na utoaji wa Taarifa mbali mbali zinazohusu Ustawi na Maendeleo ya Vijana Nchini, Taarifa hizo zinajumuisha shughuli na matukio yanayotekelezwa na Wizara, Wadau na Vijana wenyewe.

14/07/2025
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imetiliana saini hati ya Makubaliano (MOU) na Campuni ya Haryana State El...
13/07/2025

Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imetiliana saini hati ya Makubaliano (MOU) na Campuni ya Haryana State Electronics Development Corporation (Hartron) ya Maryana Nchini India kwa ajili ajili ya kuendeleza Vijana wa Zanzibar.

Utiaji Saini huo, umefanywa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, imetiwa saini na Katibu Mkuu wake bi Fatma Hamad Rajab na kwa upande wa Kampuni ya Harton, imetiwa saini na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Dk. Ganesan Jagadesan.

Viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo walihudhuria na Balozi wa India Nchini na Ujumbe wake ambao ulifanyika katika Ukumbi wa Wizara hiyo Migombani Wilaya ya Mjini.

Akizungumza katika Utiaji Saini wa Makubaliano hayo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Vijana, Utamaduni na Michezo Fatma Hamad Rajab amesema lengo ni kusaidia Vijana, kupata mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) na Vifaa mbalimbali.

Aidha amesema hali hiyo itatoa fursa mbalimbali kwa vijana ikiwemo kuwaunganisha pamoja, kupata ajira na kuweza kufanya kazi kwa Ufanisi.

Kwa uapande wake Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Haryana State Electronics Development Corporation kutoka India Dk. Ganesan Jagadesan ameahidi kufuata maelekezo yalimo katika Mkataba huo wa Maridhiano ili kuwasaidia Vijana wa Zanzibar.

Address

Wizara Ya Habari, Vijana, Utamaduni Na Michezo Zanzibar/Migombani Zanzibar
Zanzibar

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Maendeleo ya Vijana Zanzibar posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category