Zanzibar Green Voice.

Zanzibar Green Voice. Celebrating flowers,plants �nature and hands on farming through education ,sustainable and gardening

27/08/2026

Safari hii ilianza kwa kuchimba visiki vya Bougainvillea.

Sasa nimevihifadhi bustanini, vikiwa chini ya ardhi, vinasubiri hatua inayofuata: kupandwa katika vyombo maalum vya udongo wa mfinyanzi, vilivyobeba sura na historia ya utamaduni wa Mzanzibari.

Ngalawa, Chano na Kasiki — vyombo vya asili vinavyobeba sehemu ya historia na utamaduni wa Zanzibar.

Safari ya Bougainvillea Bonsai inaendelea… 🤗

26/08/2026

Wapenzi wangu ninaandaa channel ya TV inayolenga kuzungumzia mimea, mazingira, kilimo, maarifa ya asili na urithi wetu wa mimea.

Kati ya majina haya mawili, lipi unaliona linafaa zaidi?

1. 🌿 Zanzibar Mimea TV
2. 🌿 Zanzibar Botanical TV

Ahsante sana.

Grace 🌱Binti asili🌳

25/08/2026

Je, Afrika Bado Inaenzi Mboga Zake za Asili?

Kutoka katika Kijiji cha Muungoni, Wilaya ya Kusini Unguja, Bi. Saada Khamis alinishirikisha kumbukumbu kuhusu mboga ambazo kizazi chake kilizijua vizuri.

24/08/2026

Maganda ya karanga 🥜 na maganda ya mpunga 🌾 yako za vizuri, hayawi taka tena—yanageuka kuwa sehemu ya udongo wenye rutuba kwa ajili ya kupandia mimea.
♻️ Tunarudisha mabaki ya kilimo ardhini, tunalisha udongo na tunapanda kwa njia ya asili. 🌿
Taka za leo, rutuba ya kesho. 🌱💚

24/08/2026

Wazanzibar waliujua tangu zamani… 🌱
Lakini leo umekuwa mgeni kwa kizazi hichi

Blue Vervain au Verbena hastata
Mmea wenye historia, matumizi na maarifa ya asili yanayostahili kujulikana.

Tutailinda asili kwa nguvu zote!🌳🌿🪵

17/08/2026

Karibu ununue Hibiscus 🌺 kubwa

17/08/2026

Na sasa naanza project ya Bougainvillea Bonsai Forest Msitu wa Bonsai kabisa! 🌳

🌿 Single Bonsai ni TZS 1M
🌳 Bonsai Forest ni TZS 3M
🌳 Forest ya mashina 8 ni TZS 5M

Sasa tusubiri muda ufanye kazi yake…
this is going to be a living art piece. 🌿



Kumbukumbu la Torati 28:12:🙏🏿

10/08/2026

Mmea huu niliupanda hapa bustanini ukiwa mdogo sana. Leo hii umeustawi na kuwa mmoja wa mimea inayovutia katika bustani yangu.

Hapa Zanzibar tunaujua k**a Mpamba Wake, na una historia katika matumizi ya jadi ya jamii.

Scientific name: Lippia javanica

Kila mmea una safari yake na mmea mdogo unaweza kuwa na hadithi kubwa.

10/08/2026

BLUE GUAVA 👉 Mpera wa Safari ya Mabadiliko

Ni Mpera aina ya Blue Guava, ambao mwanzoni niliotesha katika shamba langu lililopo Mtule, Zanzibar.

Sasa ni mmea wa pili katika bustani hii ambao unaanza safari ya kuelekea kwenye mabadiliko na ubunifu wa kisanaa — baada ya Bonsai Bougainvillea. 🌳

Kila mmea una hadithi yake, na wakati mwingine bustani si mahali pa kupanda tu… bali ni mahali pa kuipa mimea nafasi ya kubadilika na kuonyesha uzuri wake kwa namna mpya. 🔥

Jina la kisayansi: Psidium guajava

08/08/2026

FIDDLEWOOD 🌿 SABATO DEDICATION

Mti mdogo wenye maua meupe yenye harufu nzuri, uliowasili Bustanini kwangu kutoka mbali—lakini leo umekuwa sehemu ya hadithi yangu ya upendo kwa mimea na uumbaji wa Mungu.

* Citharexylum spinosum*
🌿 Family: Verbenaceae
👉Native: Caribbean, Panama & Northern South America
🤍 Fragrant white flowers

Sabato njema. 🌿 May we always find time to pause, breathe and appreciate the beauty of creation.

Address

Jambiani Village
Zanzibar

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Zanzibar Green Voice. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share