05/09/2026
Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Wajumbe wa Bodi wakipatiwa mafunzo kuhusu taratibu za ununuzi wa umma katika utekelezaji wa Programu ya Uhimilivu wa Athari za Mabadiliko ya Tabianchi, SCALE Program.
Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa The Brean of Sau Inn Beach Hotel, Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja, yakilenga kuwajengea uwezo wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ili kufanya maamuzi yanayohusiana na michakato ya ununuzi wa umma katika utekelezaji wa programu hiyo.
Katika mafunzo hayo, washiriki wamepatiwa uelewa kuhusu umuhimu wa kuzingatia Sheria ya Ununuzi wa Umma, kanuni na taratibu zake, pamoja na miongozo ya Benki ya Dunia katika utekelezaji wa shughuli za ununuzi.
Pia mafunzo hayo yanatarajiwa kuongeza ujuzi na uwezo wa Wajumbe wa Bodi na Wakurugenzi katika kusimamia shughuli za ununuzi kwa ufanisi, uwazi na kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa.
Aidha, ujuzi huo utasaidia katika utekelezaji bora wa Programu ya SCALE pamoja na miradi mingine inayotekelezwa na Serikali.
π 05 Sept, 2026
π Jambiani, Zanzibar.