Presidential Delivery Bureau - Zanzibar

Presidential Delivery Bureau - Zanzibar Presidential Delivery Bureau (PDB) is an institution under President's Office - State House, Zanzibar

RAIS MWINYI:MKOPO WA BILIONI 240 KUTUMIKA KATIKA MIRADI YA KIMKAKATI
26/05/2025

RAIS MWINYI:MKOPO WA BILIONI 240 KUTUMIKA KATIKA MIRADI YA KIMKAKATI

02/05/2024

Pongezi na hongera za PDB kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kutokana na kazi nzuri na kuisaidia Wizara hiyo katika miradi yake ya vipaumbele.

31/03/2024
SOKO LA UHAKIKA ZAO LA MWANI ZANZIBARRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi  ...
20/02/2024

SOKO LA UHAKIKA ZAO LA MWANI ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amemhakikishia Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. David Concar na ujumbe wake kuwa Serikali ya Zanzibar iko tayari kushirikiana na Nutri-Sun Limited kutoka Uingereza katika kukamilisha mradi wa kiwanda cha kuchakata mwani kilichopo Chamanangwe, Pemba ambacho kukamilika kwake kutawanufaisha kwa kurahisisha kupata soko la uhakika.

Katika salamu zake naye Balozi wa Uingereza nchini Mhe. David Concar amemweleza Rais Dk. Mwinyi kwamba mipango ya kupata mashine na teknolojia ya kuchakata mwani imekamilika hivyo ifikapo mwishoni mwa mwaka 2024 kiwanda hicho kitaanza kuzalisha “Carrageenan” ambayo itatatumika kwa matumizi ya viwanda vya chakula na matibabu.

Aidha, Bi. Marisa Drew kutoka benki ya Standard Chartered alimhakikishia Rais Dk. Mwinyi upatikanaji endelevu wa fedha ambazo zitatumika kununulia mashine na zao la mwani, kiwanda hicho kitawawezesha wakulima wa mwani hasa wanawake na vijana kujikwamua kiuchumi.

Rais Dk.Mwinyi amekutana na ujumbe huo leo tarehe: 19 Februari 2024 Ikulu Zanzibar.

RAIS DK.MWINYI AKUTANA NA UONGOZI WA CRDB. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwin...
20/02/2024

RAIS DK.MWINYI AKUTANA NA UONGOZI WA CRDB.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela  na ujumbe wake Ikulu Zanzibar tarehe: 20 Februari 2024.

Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali itadumisha ushirikiano na mahusiano na benki ya CRDB.

Mkutano huo pia umehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum na Wakurugenzi mbalimbali wa Serikali kutoka Wakala wa Serikali Mtandao Zanzibar, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar na Taasisi ya Afisi ya Rais Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini.

🗓️20 Februari 2024

📍Ikulu , Zanzibar

The collaboration between PDB and TBI: The PDB CEO Professor Mohammed Hafidh Khalfan met TBI leaders in Zanzibar at PDB ...
20/02/2024

The collaboration between PDB and TBI:
The PDB CEO Professor Mohammed Hafidh Khalfan met TBI leaders in Zanzibar at PDB offices. The TBI Chief reassured PDB of its commitment to continue supporting the latter in delivering the best possible services and supporting PDB.

Taasisi ya Afisi ya Rais Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini (PDB) imeendelea kuandaa na kuratibu Mafunzo Ma...
08/02/2024

Taasisi ya Afisi ya Rais Ufuatiliaji na Usimamizi wa Utendaji Serikalini (PDB) imeendelea kuandaa na kuratibu Mafunzo Maalum ya Mawasiliano na Habari ya "PR and Communication Technical Skills" kwa Maafisa Habari na Uhusiano wa Umma zaidi ya 30 kutoka Taasisi za mbalimbali za Serikali kwa kushirikiana na Chuo cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).

Mafunzo hayo yanayohusu ujuzi wa "Uandishi na Uwasilishaji wa Taarifa Kitaalamu (PR Writing & Presentation Skills) na Usanifu na Uhariri wa Picha na Video (Editing and Graphics Designing skills) yalifunguliwa mwezi huu wa Februari, 2024 na Afisa Mtendaji Mkuu wa PDB, Profesa Mohammed Hafidh Khalfan. Mafunzo hayo yanayoendeshwa na SUZA yalianza mwanzo kwa Wizara za Vipaumbele mwezi wa Septemba, 2023 kwa Unguja na Oktoba kwa upande wa Pemba, 2023. Aidha Mafunzo k**a hayo kwa Taasisi za Serikali upande wa Maafisa wa Pemba yatafanyika mwezi wa Aprili, 2024.

Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo Maafisa Habari na Uhusiano wa Umma wa Serikali ili kuimarisha ujuzi wao na kusaidia kuwa na wigo mpana na mzuri zaidi wa kutoa taarifa na kuandaa makala na vipindi kwa mafanikio ya Serikali na pia katika kutoa taarifa za matukio ya shughuli za Taasisi zao husika.

Taasisi ya PDB itaendelea kushirikiana na kuisaidia Serikali katika utekelezaji wa miradi ya vipaumbele na katika kutoa taarifa za mafanikio ya Serikali katika sekta mbalimbali hasa maeneo ya vipaumbele.

Zanzibar yaendelea kufanya vizuri katika utalii ambapo Meli ya kitalii MSC POESIA- Imewasili katika Bandari ya Zanzibar ...
08/02/2024

Zanzibar yaendelea kufanya vizuri katika utalii ambapo Meli ya kitalii MSC POESIA- Imewasili katika Bandari ya Zanzibar ikiwa na watalii zaidi ya 2149 kutoka mataifa mbali mbali amabo wameshuka na kutemebele vivutio katika Kisiwa Cha Unguja

Mwenyewekiti wa Bodi ya Shirika la Bandari Zanzibar (ZPC) Akiungana na Mkurugenzi Mkuu wa ZPC pamoja na Mwenyekiiti wa Bodi ya Kamishemi ya Utalii wameongoza mapokezi ya Meli hio.

Shule ya Sekondari Maziwa ya Ng'ombe iliyopo Kisiwani Pemba. Hiyo ni kazi kubwa na nzuri ya Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwe...
08/02/2024

Shule ya Sekondari Maziwa ya Ng'ombe iliyopo Kisiwani Pemba. Hiyo ni kazi kubwa na nzuri ya Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Hongera Zanzibar. Hongera wananchi wote wa Zanzibar na Tanzania.
13/01/2024

Hongera Zanzibar. Hongera wananchi wote wa Zanzibar na Tanzania.

Address

Zanzibar
P.O.BOX2422

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Presidential Delivery Bureau - Zanzibar posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Presidential Delivery Bureau - Zanzibar:

Share