06/12/2025
NAIBU KATIBU MKUU ATOA WITO KWA WAANDISHI WA HABARI KUIMARISHA MAPAMBANO DHIDI YA UDHALILISHAJI WA WANAWAKE NA WATOTO.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ndugu Khatib Mwadini Khatib ametoa wito kwa waandishi wa habari kuongeza juhudi katika kuelimisha jamii kuhusu madhara ya udhalilishaji wa wanawake na watoto na kusema jukumu hilo ni sehemu muhimu ya ulinzi na ustawi wa makundi hayo.
Akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wake kuripoti habari za ukatili na udhalilishaji wa kijinsia Naibu Katibu Mkuu amesema ongezeko la matukio ya udhalilishaji wa watoto na wanawake, ikiwamo unyanyasaji wa kimwili, kingono, kihisia na mtandaoni ni janga linalolikabili taifa na kurejesha nyuma maendeleo ya nchi.
Amesema udhalilishaji wa watoto unaathiri mustakabali wao kwa kuwasababishia msongo wa mawazo, kuharibu afya ya akili, kukosa fursa za elimu na kujiamini, hivyo juhudi za pamoja zinahitajika kulinda haki zao.
Amesema Udhalilishaji wa watoto kwa njia ya mtandao umeongezeka kwa kasi na kupelekea watoto kukabiliwa na vitisho, maudhi yasiyofaa, upotoshaji na mifano mibaya kupitia mitandao ya kijamii na michezo ya mtandaoni, hivyo wazazi na walezi wanapaswa kuwa macho na kufuatilia matumizi ya mtandao ya watoto wao.
Amebainisha kuwa katika mafunzo hayo, washiriki wataelekezwa kuhusu Mpango wa Kitaifa wa Mapambano Dhidi ya Ukatili na Udhalilishaji (NPA-VAWC) Zanzibar, unaotekelezwa na wadau mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari.
Hatahivyo amesisitiza kuwa vyombo vya habari vina nafasi kubwa katika kuibua matukio, kuelimisha jamii na kuhamasisha hatua madhubuti dhidi ya ukatili.
Kwa upande wao, wataalamu kutoka wizara na wadau wa maendeleo ya watoto wamesema elimu ya mara kwa mara kwa jamii, uangalizi wa karibu wa watoto, pamoja na kuripoti matukio ya udhalilishaji ni miongoni mwa hatua muhimu za kupunguza vitendo hivyo.
Naibu Katibu Mkuu aliwataka washiriki kutumia mafunzo hayo kuboresha uandishi unaolenga kuleta mabadiliko chanya katika jamii.
Mafunzo hayo ya siku moja yamewashirikisha waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali yamefanyika katika ukumbi wa UNWOMEN Kinazini Zanzibar hiyo ukiwa ni kuelekea maadhimisho ya siku 16 za