Baraza la Michezo la Taifa

  • Home
  • Baraza la Michezo la Taifa

Baraza la Michezo la Taifa Baraza la Michezo la Taifa (BMT)
"Michezo ni Afya, Michezo ni Ajira"

SERIKALI YAHAKIKISHA KUENDELEA KUZIWEZESHA TIMU ZA TAIFA KUFANYA VIZURI KIMATAIFASerikali imeahidi kuendelea kuziwezesha...
14/07/2026

SERIKALI YAHAKIKISHA KUENDELEA KUZIWEZESHA TIMU ZA TAIFA KUFANYA VIZURI KIMATAIFA

Serikali imeahidi kuendelea kuziwezesha timu za taifa zinazoshiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa ili kuhakikisha zinafanya vizuri na kuiletea Tanzania heshima.

Kauli hiyo ilitolewa Julai 13, 2026, na Afisa wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Oscar Zabron, wakati alipoitembelea Timu ya Taifa ya Judo kambini Ukonga, jijini Dar es Salaam, inayojiandaa kushiriki Mashindano ya Jumuiya ya Madola.

Oscar amesema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kila timu ya taifa inayoshiriki mashindano ya kimataifa inapata maandalizi bora na mazingira wezeshi ya kufanya vizuri.

Aidha, amewahimiza wachezaji kuitumia kikamilifu kambi ya maandalizi kwa kufanya mazoezi kwa bidii na kuzingatia maelekezo ya makocha, akisisitiza kuwa ushindi watakaoupata utakuwa ni fahari ya Watanzania wote.

"Serikali itaendelea kuziwezesha timu za taifa ili zifanye vizuri katika mashindano ya kimataifa.

Tunawaomba muweke nguvu katika mazoezi na kufuata maelekezo ya makocha, kwani ushindi mtakaoupata ni wa Watanzania wote," amesema Oscar.

Timu ya Taifa ya Judo inaendelea na maandalizi ya mwisho ikiwa na matumaini ya kuiwakilisha vyema Tanzania na kuwania medali katika Mashindano ya Jumuiya ya Madola yatakayofanyika Glascow, Scotland.

Kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Serikali imeratibu na kugharamia mahitaji muhimu ya kambi, ikiwemo malazi, chakula na posho kwa wachezaji, ili kuwawezesha kufanya maandalizi katika mazingira bora kuelekea mashindano hayo.
1m

BMT YAADHIMISHA SIKU YA MICHEZO SABASABA KWA MBIO ZA POLEWatumishi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Wizara ya Habari...
14/07/2026

BMT YAADHIMISHA SIKU YA MICHEZO SABASABA KWA MBIO ZA POLE

Watumishi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, pamoja na Kikundi cha Jogging cha Temeke, leo Julai 12, 2026, wameshiriki mbio za pole zilizoanzia Uwanja wa Benjamin Mkapa na kuhitimishwa katika Viwanja vya Sabasaba.

Shughuli hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya BMT kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026), ikiwa na lengo la kuhamasisha wananchi kushiriki michezo kwa ajili ya afya, ustawi na maendeleo ya sekta ya michezo nchini.

BMT YAONESHA NJIA YA AFYA BORA KUPITIA MAZOEZI SABASABA 2026Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limeendelea kuhamasisha jam...
14/07/2026

BMT YAONESHA NJIA YA AFYA BORA KUPITIA MAZOEZI SABASABA 2026

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limeendelea kuhamasisha jamii kuzingatia afya bora kupitia ushiriki wa mazoezi ya viungo katika Siku ya BMT, iliyofanyika ndani ya Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026).

Hamasa hiyo iliongezeka baada ya Klabu ya Temeke Jogging and Sports Club kuiunga BMT kushiriki mazoezi mbalimbali ya viungo katika Kijiji cha Wizara ya habari Utamaduni Sanaa na Michezo Sabasaba 2026 hatua iliyovutia wananchi wengi kujumuika na kujifunza umuhimu wa kufanya mazoezi mara kwa mara.

Kupitia shughuli hiyo, BMT imeendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu nafasi ya michezo na mazoezi katika kuboresha afya, kuzuia magonjwa yasiyoambukiza na kuimarisha ustawi wa jamii, sambamba na kuhamasisha Watanzania kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi k**a sehemu ya maisha ya kila siku.

WANANCHI WAFURIKA BANDA LA BMT, WASHIRIKI MICHEZO YA JADI NA MINGINEYOWananchi wamejitokeza kwa wingi kushiriki michezo ...
14/07/2026

WANANCHI WAFURIKA BANDA LA BMT, WASHIRIKI MICHEZO YA JADI NA MINGINEYO

Wananchi wamejitokeza kwa wingi kushiriki michezo mbalimbali, ikiwemo michezo ya jadi, katika banda la Baraza la Michezo la Taifa (BMT) lililopo kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba 2026), ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya BMT.

Washiriki walipata fursa ya kujifunza na kushiriki michezo hiyo huku wakihamasishwa kufanya mazoezi mara kwa mara, kuenzi michezo ya jadi na kutambua fursa mbalimbali zinazotokana na sekta ya michezo kwa maendeleo ya taifa.

14/07/2026

Serikali imeahidi kuendelea kuziwezesha timu za taifa zinazoshiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa ili kuhakikisha zinafanya vizuri na kuiletea Tanzania heshima.

Hayo yamesemwa leo, Julai 13, 2026, na Afisa wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Oscar Zabron, wakati alipoitembelea Timu ya Taifa ya Judo kambini, jijini Dar es Salaam, inayojiandaa kushiriki Mashindano ya Jumuiya ya Madola.

14/07/2026

Makamu wa Rais wa Chama cha Judo Tanzania (JATA), Andrew Mlugu, ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuiunga mkono Timu ya Taifa ya Judo kwa kugharamia kambi ya maandalizi inayoendelea Ukonga, jijini Dar es Salaam.

Mlugu amesema hatua ya Serikali kuwekeza katika maandalizi ya timu imeongeza ari na morali kwa wachezaji, jambo linalowapa nguvu ya kuendelea kufanya mazoezi kwa bidii kuelekea Mashindano ya Jumuiya ya Madola.

14/07/2026

Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Judo, Ibrahim Hamisi,amesema maandalizi mazuri yaliyowezeshwa na Serikali yamewapa wachezaji ari, kujiamini na utayari wa kuingia kwenye mashindano wakiwa na lengo la kupeperusha vyema bendera ya Tanzania.

14/07/2026

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Judo, Omary Mgoe, amesema kikosi hicho kinaingia kwenye Mashindano ya Madola kikiwa na morali ya juu na imani kubwa ya kufanya vizuri kwa kuwania medali.

Mgoe amesema maandalizi yaliyofanyika yamewajengea wachezaji uwezo na kujiamini, huku akisisitiza kuwa lengo kuu ni kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kupitia mchezo wa judo.

UNISOKA YALENGA KUKUZA VIPAJI VYA WANAFUNZI WA VYUOMeneja wa Mradi wa mashindano ya mpira wa miguu kwa wanafunzi wa vyuo...
11/07/2026

UNISOKA YALENGA KUKUZA VIPAJI VYA WANAFUNZI WA VYUO

Meneja wa Mradi wa mashindano ya mpira wa miguu kwa wanafunzi wa vyuo (UNISOKA), Jumanne Fadhili, amesema mashindano hayo yameanzishwa kwa lengo la kuibua na kukuza vipaji vya wanafunzi wa vyuo, ili kuwapa fursa ya kuonesha uwezo wao na hatimaye kusajiliwa na klabu zinazoshiriki ligi mbalimbali nchini.

Jumanne amesema huu ni msimu wa kwanza wa UNISOKA ukihusisha vyuo vya Dar es Salaam, huku maandalizi yakiendelea kupanua mashindano hayo msimu ujao kwa kushirikisha vyuo kutoka mikoa yote ya Tanzania. Pia amebainisha kuwa waandaaji wanatarajia kuanzisha ligi ya wanawake kuanzia msimu ujao.

Aidha, ameishukuru Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa mchango wake katika kufanikisha usajili wa mashindano hayo, pamoja na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kwa ushirikiano wake katika uratibu wa ligi hiyo.

Katika mchezo uliochezwa jana Julai 10, 2026, Chuo cha Ustawi wa Jamii (ISW) kiliibuka na ushindi wa bao 4-2 dhidi ya Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Kigamboni (KICCOHAS).

10/07/2026

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Andrew Boniface Rhobi, ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuisapoti Timu ya Taifa ya Riadha kuelekea mashindano ya kimataifa.

Rhobi ametoa wito kwa wadau wa riadha na Watanzania kwa ujumla kuendelea kuiunga mkono timu hiyo, akisisitiza kuwa ushirikiano na sapoti ya wananchi ni chachu ya kuongeza morali na kuleta mafanikio kwa taifa.

Address

MKAPA STADIUM, 2nd Floor, DAR ES SALAAM

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Baraza la Michezo la Taifa posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Organization

Send a message to Baraza la Michezo la Taifa:

Shortcuts

  • Want your organization to be the top-listed Government Service?

Share