24/10/2023
NAUNGA MKONO UTEUZI WA PAUL MAKONDA KUWA MWENEZI WA CCM TAIFA.
Idara ya itikadi na uenezi ndio moyo wa Chama Cha Mapinduzi kutokana na majukumu nyeti ya idara hiyo ambayo kwa mujibu wa katiba ya CCM ina majukumu makuu manne ambayo ni pamoja na kueneza itikati,falsafa misingi na sera za CCM,Kusimamia uendeshaji wa vyombo vya habari vinavyomilikiwa na CCMu,Kusimamia na kuratibu mafunzo ya makada ,viongozi na wanachama wa CCM na kusimamia masuala ya mawasiliano na uhamasishaji wa umma.
K**a mwana CCM naunga mkono kuondolewa kwa Dada yetu Sofia Mjema katika nafasi hiyo na ninaunga mkono uteuzi wa Paul Makonda aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam kuwa Mwenezi mpya kwani Sofia Mjema alishindwa kabisa kufanya kazi za uenezi kutokana na ukweli kuwa tokea alipoteuliwa kuwa Mwenezi alikuwa akifanya kazi moja tu ya uMC Kwenye mikutano ya Katibu Mkuu ndugu Daniel Chongolo pamoja na kufanya press baada ya vikao vikuu vya CCM k**a vile k**ati kuu na Halmashauri kuu ya taifa.
Mikutano hiyo ni muhimu sana katika kukijenga na kukiimarisha chama lakini kwasisi tunaokijua Chama hatukutegemea Mwenezi wa taifa kufanya majukumu hayo pekee.
Kushindwa kwa Sofia Mjema kunatokana na ukweli kuwa siyo mwana CCM kindakindaki na hivyo hakuwahi kuandaliwa tofauti na Paul Makonda ambaye amekulia ndani ya CCM na hivyo inaijua vyema sera ya ujamaa na kujitegemea vilevile ni wazi kuwa uongozi ndani ya Chama cha siasa na uongozi serikalini ni vitu viwili tofauti kwani Chama cha siasa kuna vionjo vyake na k**a hujui vionjo hivyo basi uongozi utakushinda hivyo katika makala haya sina nia mbaya ya kumchafua Dada yetu Sofia Mjema na ninamtakia mafanikio makubwa katika wadhifa wake mpya.
Paul Makonda ana uwezo mkubwa wa kutawala jjukwaa na ana uwezo wa kujenga hoja ,sifa muhimu sana katika kutekeleza majukumu ya idara hiyo.
Hatahivyo Paul Makonda ana deni kwa wana CCM na baadhi ya Watanzania kutokana na kuhusishwa na baadhi ya matukio yaliyotokea wakati wa utawala wa awamu ya tano hivyo anapaswa aweze kutulia na aonyeshe uwezo wake kwani k**a kiongozi ameonyesha kuwa haogopi kuchukua maamuzi na huwa haogopi kulaumiwa.
Kwakuwa tunaelekea katika uchaguzi mkuu naamini kuwa Paul Makonda atakisaidia vizuri Chama chetu katika kubuni mpango mkakati wa kunadi mafanikio ya serikali ya awamu ya sita kwani hivi sasa japo serikali ya COM inayoongozwa na Dr Samia Suluhu Hassan inafanya mambo mazuri kwa wananchi lakini wananchi wengi hawajui mambo hayo kutokana na ukweli kuwa hawaelimishwi vya kutosha.
Mwisho,K**a mwana CCM nitatoa natoa ushauri kwa Mwenezi wetu mpya kila wakati nitakapoona inafaa ili kuiboresha idara hiyo nyeti na mpaka sasa nimeandaa maandiko kadhaa ambayo ni
Umuhimu wa kurudisha kitengo cha Propaganda
Madarasa ya itikadi na
Mpango mkakati wa kunadi mafanikio ya serikaliya awamu ya sitakupitia mitandaoya kijamii
Kidumu Chama Cha Mapinduzi
Mwandishi wa makala haya Otieno Peter Baraka ni kada wa CCM anayepatikana kwa namba
0629883024