15/07/2026
Tulifanya ukaguzi na tathmini ya maendeleo ya ujenzi wa Soko la Mwanda ili kujiridhisha na ubora wa kazi iliyotekelezwa na mkandarasi. Kwa sasa, shughuli za mwisho za ukamilishaji zinaendelea ili kuhakikisha wananchi wa Mwanda wanapata mazingira salama na bora ya kufanya biashara.
Serikali ya Kaunti ya Taita Taveta itaandaa kikao cha umma kwa lengo la kuwachagua wajumbe wa Kamati ya Usimamizi wa Soko na kuwahamasisha wananchi kuhusu namna bora ya kulitumia soko hilo k**a fursa ya kukuza biashara zao, kuongeza kipato cha familia na kuchochea maendeleo ya uchumi wa eneo letu.
Soko hili ni uwekezaji muhimu unaolenga kuboresha huduma za biashara, kuimarisha uchumi wa wananchi na kuendelea kufungua fursa za maendeleo katika Wadi ya Mwanda/Mgange.
Shukrani za dhati kwa Mustahiki Gavana H.E Dr. Andrew Mwadime - Wakujaa, EGH, Governor Taita Taveta County , mwakilishi wadi Anselm Mwana Wa Chao , idara ya biashara pamoja na washikadau wote walioshirikiana kufanikisha mradi huu. Ama kwa hakika pamoja tunawezafika mbali.